Jinsi wanaume walivyokwepa jukumu la msingi la kutongoza

Jinsi wanaume walivyokwepa jukumu la msingi la kutongoza

AdorableL

Member
Joined
May 25, 2024
Posts
33
Reaction score
59
True story;
Screenshot_20241204_173120_iHappy.jpg
 
Ungesema tu kwa Kiswahili “unataka nini kifayike ili tuweze kusongesha gurudumu letu la mapenzi mbele” ungeeleweka japo maswali ya toka lini tumekuwa wapenzi nk nk yangekuwepo but ujumbe ungeenda direct kwa muhusika.

Sasa ”relationship”,kibiashara,kindugu au nini?wanawake wenyewe hawa wa kibongo watajifanya hawakuelewi ubaki unang’aa macho
 
jaribu kuwa muelewa

hapo katupia ndoano sema amekosa misamiati sahihi

yawezekana ujuzi wake wa ngeli ni mdogo

anajitutumua kwa kufosi
Hata kama jamani, yaani baada tu ya salamu mtu anauliza jinsi ya kuimarisha penzi? Penzi lipi hata hakujui jina ndio kwanza umempa namba.....? Wanaume msikwepe majukumu. Kutongozwa kuna raha yake. Aseme basi hata " dada naomba tuwe wapenzi"
 
Nilichogundua na wewe unamtaka, ila uwasilishaji ndio umekutoa kwenye reli.
Sasa mwambie akutongoze vizuri, au mtongoze wewe, mnasema 50/50
Ndio maana nimeleta hoja mbele yenu wananzengo, hii ya kujibu tu "hi" eti ghafla umeshakuwa mpenzi wa mtu inatisha,
 
Daaah aisee we mpe mbinu za kustrengthen mahusiano yenuuu 😅😅😅😅 anajua akikutongoza utamkataqq kwa mara ya Kwanzaa ndo maana anajenga chemistry tu🏋️🏋️🏋️😉
 
Hata kama jamani, yaani baada tu ya salamu mtu anauliza jinsi ya kuimarisha penzi? Penzi lipi hata hakujui jina ndio kwanza umempa namba.....? Wanaume msikwepe majukumu. Kutongozwa kuna raha yake. Aseme basi hata " dada naomba tuwe wapenzi"
yaani anavyosema 'strengthen' inawezekana kabisa hamaanishi 'imarisha' bali anamaanisha apandishwe cheo kutoka rafiki hadi mpenzi

kiingereza lugha sumbufu kwa wengi, misamiati ni hapa

lakini kama unamuelewa mkubalie dada huna cha kupoteza

ukimchunguza sana bata hutomla
 
Back
Top Bottom