Kwahiyo Watanzania wote huwa mnaenda China hamtumii Ali Baba?
Naona wengi mnamtowa akili mleta mada lakini Mimi naona Yuko Sahihi.
Naweza kufanya biashara na
Mshana Jr Bila hata kuonana naye, naamini Mshana hawezi kuharibu reputation yake JF Kwa sababu ya biashara ya million hata kama anatumia I'd bandia.
Kuna namna ya kufanya biashara na mtu usiyemjuwa na ukawa salama tu.
Hivi Leo nimuagize kitu
Kiranga Marekani cha dola 500 akimbie I'd na heshima kubwa aliyonayo hapa JF Kwa sababu ya dola 500?
Kwa mifano hii michache nadhani mtaelewa kwamba dunia tuliopo individuals huwezi kutumia letter of credit ya benki kupata huduma, na supplier hawezi kudeliver service Bila pesa yake, kwahiyo ni wajibu wako kufanya biashara na watu Sahihi na namna ya kupata watu Sahihi Zipo.
Anacholalamika mleta mada hata Japan kulikuwa kinafanyika, kwenye internet unapostiwa gari lakini huoneshwi dosari zake, walipokuja Be forward wamefanya mapinduzi kama gari ina scratch wanakuonesha kabisa ndio sababu ya Be forward kuliteka soko, uadilifu.