Jinsi watu wa mikoani tunavyofanyiwa tunapoagiza bidhaa toka kwa watu wa Dar es Salaam

Acha kuwadanganya wengine.
Sasa nidanganye nini Mkuu, nachokwambia ndio ukweli labda mleta mada anafanya na watu ambao sio waaminifu, lakini mimi nimefanya nao karibia kumi na zaidi sijawahi agiza nikatapeliwa hela, kuna watu online business ndo ajira zao kwahiyo kuzingua ni kazi ila sikatai wengine sio waaminifu ila mimi mpaka sasa sijawahi tapeliwa.
 
Mkuu huu ni ukweli Mtupu, na nashukuru umelieleza hapa

KAMWE sintanunua bidhaa hasa nguo kutoka Kariakoo na Sinza Dsm kwsbb wauzaji wengi ni MATAPELI

Mimi niliagiza suti ya dogo ya harusi, na alichagua suti nzuri tu ya sh. 230,000/= yaani suti, kizibao, shati na tai...

Kilichotokea wakambadilishia shati na tai, wakampa zingine

Wapumbavu sana hawa
 
Ungewataja na hao waliokuuzia ili uokoe na wengine,

Mimi huwa naagiza vitambaa lkn sijawahi kutapeliwa,

ni mmoja tu ndo alinibadilishia jora na nilimrudishia akakubali
Nilikuwa nasubiri akatae au anigeuke niende kwenye page yake nikacoment utumbo anabahati hakubisha.
 
Mkuu ni hatar, mm niliagiza shati kali 4, yan zinakuja shati sijawah hata ziona, na mzgo umeshafika, ni hatar, ogopa.
 
Kuna page 1 maarufu sana fb na insta, ila nisiwataje nitawaharibia biashara.
 
Endelea
 
Sijui huwaga ni nini kwakweli kuna mmoja mpaka akampaga mke wake simu eti aniseme mzigo mbona haufiki, aiseee nilijiskia vibaya wakati tulishamalizana mpaka kaongea na wenye gari kwamba imeharibika na mizigo haiwezi faulishwa kama abiria maana inapoteaga, nilikua tayari mzigo wangu urudishwe naye nimpe pesa yake, sema konda akaniambia tulia kesho unafika kweli ulifika, akaja kurudi tena tufanye biashara nikamuambia tu asante napenda hela ila yako ni ngumu, nikamdirect kwa mtu mwingine hakuridhika akarudi tena roho ikamgomea kabisaa.
 
Uwe unalipia baada ya kupokea na kuukagua mzigo. Wafanya biashara wa online walio serious hufanya hivyo.
 
Kuna wateja hawajui kuwa sometimes kuna emergency, wao wanachojali ni matakwa yao, wateja wa hivyo hata ukimrejeshea malipo yake hawaishi kulalamika.
 
Kuna binamu yangu katuma 150k kwa rafiki yake ajiunge jeshi toka mwaka jana mwezi wa sita anasubiri,nmeamini kuna watu wanaamini misemo ya wahenga[emoji23][emoji23]
 
Kiongozi inabidi uokoke kabisaaa maana yawezekana ulifanya biashara na malaika bila kujua! Vijana wa bongo dasalama sio wakumuazima hata pumzi yupo tyr akue kabisa
 
Polisi ipo
Tumia sheria kudai haki
 
Fact
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…