Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

Ukiwa na kipaji hufi na njaaa usitolee mfano watu wenye kipaji kama soka, kuimba nk..

Tutoleee mfano mtu aliyeanza na kapu la karanga la efu kumi, au chapati au pipi afu akaja kuwa bilionea step by step bila kufichaficha[emoji28]
Konde boy alianzia chini, sa ivi anagawa hela jukwaani.

Pia Makonda kuna picha za zamani alikua choka mbaya sa ivi yuko hapo alipo.
The Masanja na wenzake walikua choka mbaya, sa ivi wana magari ya kubadilisha kuanzia jumapili mpaka jumaosi.

Tatizo hapo katikati huwa hatuambiwi ukweli walifanyaje, labda mfano kujipendekeza kwa wakubwa, kuuza unga, walisoma elimu ya juu zaidi, walienda kanisani na kuombewa etc. huwa hawatamki kabisa, ili na sisi tuwe matajiri.
 
kuna mtu alishawahi kuniambia, katika nchi zetu hizi za kiafrica ukitaka kuwa tajiri haswa, tajiri kwelikweli lazima ashiriki moja ya mambo haya ili kumuwezesha kufika huko.
1. Rushwa,Ufisadi/wizi wa mali za umma/kampuni
2. Kukwepa kodi, Biashara za magendol/Haramu
3. Ushirikina
4. Kurithi mali
Hizi zingine ni porojo tu za mdomoni
Upo sahihi kabisa!
 
Watu wengi sio wakweli. Utakuta mtu ana bodaboda mbili anakupigia mahesabu kwa mwezi kila boda moja inamuingizia 300,000 which means kwa siku ni 10,000. Sasa kanunue wewe uone,unakuta faida sio ile ulioaminishwa. Dereva pasua kichwa. Mwisho wa siku utaishia kuiuza tu. Don't believe everything you hear. People don't share their struggles.
 
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kugundua talanta yako na itumie ikuletee mafanikio. Wengi mnafeli sababu mnataka kufuata vitu ambavyo by nature hauko talented. Kama ambavyo Dangote hawezi kuwa footballer mkubwa ndivyo sawa na wewe hutoweza kuwa Dangote katika biashara.
Moja ya kauri ya kijinga ni hii ya taranta, hakuna anayezaliwa na taranta ya Biashara ila tunapata kila Day wanaibuka wafanya Biashara wenye njaa na ubunifu kwasababu ya njaa ya pesa.

Njaa ya pesa/mafanikio inakupa taranta ya kila biashara hapa duniani Ukulima, Engeener, Ufundi, Upishi, Udereva nk

Asikwambie mtu fuata taranta sijui passion ni ujinga angalia pesa ipo wapi chora mikakati ya kuiendea ifuate ukionja utamu wa pesa utakuwa na passion na hicho kitu.

huwezi kuwa timamu eti uwe na taranta sijui passion ya kuogerea je umeona mtu yeyote Tz aliyefanikiwa kwenye hiyo nyanja hakuna je wapo walofanikiwa kwenye kilimo ndio wapo kibao weka mtaji kachukue Captivator, Harvester nk kalime mikese huko utafanikiwa na utakuwa na passion na kilimo ukionja pesa tu watu kibao wote watakula mazao yako sasa kwenye kuogerea utaishia kufa masikini tu.
 
Hahaha!! Hao ni motivational speakers wa kibongo ndio wanawadanganya hivyo. Nyambaf zao!!!
Kuna watu utawasikia eti mbona Bill Gates aliacha shule unaanza kumwambia ukweli usiseme shule sema Havard. Chuo cha watu wenye hela na wenye akili na siyo kwamba aliacha shule aliishindwa ila aliacha kwakua aliona anachokitaka yeye kifundishwe hakikuepo, kwahiyo ni shule ilimshindwa yeye siyo yeye aliishindwa shule.

Sasa kijana unapata division zero shule ya kata ukiambiwa rudi darasani utetezi wako ni Bill Gates naye hakusoma, pumbavu.
 
utajiri ni KARAMA, asikudanganye mtu, HATA ukopi maarifa aliyofanya tajiri fulani kwa asilimia 100% haikuhakikishii kufankikiwa hata kwa 1 %, , hata ukopi maneneo ya '' motivational speaker '' kwa 100% na kuyafanyika kazi, hayakuhakikishii kufanikiwa hata kwa 1 %,
 
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kugundua talanta yako na itumie ikuletee mafanikio. Wengi mnafeli sababu mnataka kufuata vitu ambavyo by nature hauko talented. Kama ambavyo Dangote hawezi kuwa footballer mkubwa ndivyo sawa na wewe hutoweza kuwa Dangote katika biashara.
Rudia kusoma nilichoandika
 
utajiri ni KARAMA, asikudanganye mtu, HATA ukopi maarifa aliyofanya tajiri fulani kwa asilimia 100% haikuhakikishii kufankikiwa hata kwa 1 %, , hata ukopi maneneo ya '' motivational speaker '' kwa 100% na kuyafanyika kazi, hayakuhakikishii kufanikiwa hata kwa 1 %,
Izo karama zinakuja kwaaliye fanya izo njia kwa ufanisi ndio anapewa nafasi ya kuwa tajiri au asiwe tajiri, ila kama umekaa bila kufatisha chaguo lako linakuwa moja kukosa tu.
 
Back
Top Bottom