Jinsi wenye magari wanavyopigwa na mafundi

Jinsi wenye magari wanavyopigwa na mafundi

Kuna tatizo mkuu?, yes kwenye gari sijui vitu vingi sana.

Na kuna watu wengi sana nawakataa sababu matatizo yao siwezi kusolve.

Ili uwe fundi ni lazima ujue kila kitu kwenye gari?.

Labda wewe uniambie kwenye gari ni kazi gani ambazo unafanya?

Na pia ili na mimi niwe fundi kama wewe ni vitu gani niongeze?
hapana hujanielewa.nimemjibu huyo jamaa hapo uu kuwa watu watapigwa tuu coz hakuna fundi anae weza Mambo yote..mwingine anadili na gia box tuu mwingine ingene tuu

mwingine mfumo wa umeme tuu. huwezi kuwa fundi wakila kitu kwenye gari labna unaweza ukawa na uelewa tuu wakutambua matatizo mbalimbali
 
Kuna tatizo mkuu?, yes kwenye gari sijui vitu vingi sana.

Na kuna watu wengi sana nawakataa sababu matatizo yao siwezi kusolve.

Ili uwe fundi ni lazima ujue kila kitu kwenye gari?.

Labda wewe uniambie kwenye gari ni kazi gani ambazo unafanya?

Na pia ili na mimi niwe fundi kama wewe ni vitu gani niongeze?
huwezi kuwa fundi wakilakutu ndio Mana nikasema watu watapigwa tuu coz lazima wakutane namafundi aina mbalimbali.sababu hata mziba pancha nifundi anaweza kukupiga tuu🤣🤣
 
Kuna watu anapeleka gari kupiga rangi bampa halafu linarudi linamisi halafu anarelax tu....
kuna muda inaweza tokea
mfano mm juz kati nilipeleka gar kupigwa rangi nilikuepo muda wote wa tukio saa naondoka nikasikia sauti kwenye engine mlio wa belt inapiga kelele nisingekuepo ningewaza nimepigwa
in short hakikisha siku unapeleka gar kwa fundi umepata muda wa kutosha sio unapeleka una ishu zako unawah uwaachie unless apo unapoiacha gar ni kampuni kubwa haina makanjanja zipo sehemu watu wanaacha magar na kuna usalama hamna shida ila ni chache sanaaa
na kuna sehemu unakuta umeenda na tatizo la gar yako unaona wanataka wachukue kitu kwenye gar nyingine ulioikuta apo wakuwekee apo paogope paogope kbsaa na ww ukiwa haupo watachukua kifaa chako waweke kwa mungine
 
mfano sensor ina wire 4, anaamua kuzibadili, wire uliokuwa huku anaweka huku, wa huku anaweka huku,

Hiyo inasumbua sana kuja kuzirudisha hizo wire.....
Huo mchezo upo sana kama una tabia ya kubadilisha mafundi.
 
Anakata wire ili baadae ukija kunotice tatizo si utarudi kwake?

Hapo ndio atakupiga hela,

Na asikudanganye mtu, hakuna matatizo magumu kufix kama matatizo ambayo mtu alikaa akalitengeneza, yanasumbua mno....
Tatizo la kutengenezwa ni gumu sababu mtu anakuwa anajua way out so ataangalia njia ambazo hamtaweza kutatua hadi yeye mwenyewe aamue kutatua.
 
Kuna watu anapeleka gari kupiga rangi bampa halafu linarudi linamisi halafu anarelax tu....
Hayo yamenikuta gereji ya magomeni hapo popobawa. Gari imeenda nzima kunyooshwa imerudi kitasa kimoja kibovu, kioo kinashuka nusu, haipigi jino moja sahizi ni cycle kama 4 hadi 6 ndio inawaka. They fucked my car kwa kuilaza hapo only 3 days.

Ati fundi anakwambia braza gari naona haiwaki sijui itakuwa mafuta. Niliwaambia kauli moja tu kuwa ilikuja inatembea hapo na itarudi inatembea. 🤣🤣🤣🤣 🤣
 
Labda kwa kuanza nieleze kisa kilichomkuta jamaa yangu.

Jamaa ana Subaru Forester 2006 2.0L

Usiku wa kuamkia 9 january 2023 zilinyesha sana mvua na kuna maeneo mjini yalijaa maji, sasa bahati mbaya wakati anaenda mishemishe kuna mahali alifika maji yakawa mengi.

Katika kupita maji yakawa yameingia mpaka ndani ya gari.

Sasa baadae kuna jamaa akawa amewapelekea ili watoe seat na makapeti ndani ili wayakaushe.

Jioni alipoenda kuchukua gari alipoendesha kidogo ikaanza kuwaka Check engine.

Akarudi wa wale jamaa wanamkaushia vitu vya ndani, wakacheck weeee mwisho wa siku wakasema Control box (ECU) imelowana hivyo inabidi ikakaushwe na bei ya kukaushwa ni Tsh. 150,000/=. 😂😂😂😂.

Basi jamaa akanipigia, kuniuliza kuhusu hayo aliyoambiwa na hao jamaa. Nikamuambia ninachokifahamu kuhusu check engine kwamba kuna chances kuna connectors maji yameingia na hivyo kupelekea kuwaka kwa hiyo check engine.

Lakini pia nikamshauri alete gari tuangalie kama kweli control box imeingia maji, me nitaikausha na hot air gun.

basi akaja jioni hiyohiyo, Kufanya diagnosis shida ikatokea P0037 HO2S heater circuit low(B1S2). Hii ni O2 sensor ya nyuma au baada ya masega(CAT converter).
View attachment 2525315


Nikasema labda maji yameingia kwenye connector ya Oxygen Sensor nikacheck connector iko poa, pia nikacheck connector zingine mpaka kwenye ecu wala hakuna maji.

Basi nikamuambia atembelee kama haitazima basi sensor inaweza kuwa imeshaleta shida.

Katembelea almost a week bila check engine kuzima basi akarudi tukatafuta Oxygen sensor tukaona bei mlima (180k sensor used, ndugu zangu wa Subaru poleni sana).

Basi tukafikia hitimisho kwamba tuagize tu nje. Lakini kabla ya kuagiza nikasema nijiridhishe tena na wiring ya ile gari. Hiyo ilikuwa ni jana.

Oxygen sensor ina waya 4, nikaanza na waya mmoja baada ya mwingine. Diagram yake hii hapa chini.

View attachment 2525288


View attachment 2525290

Hapo wire mbili za heater circuit, mmoja signal line na mmoja ni ground.

Signal line na ground niliziconfirm haraka sana kwa kutumia signal generator. Yaani naingiza signal kutoka kwenye wiring ya o2 sensor halafu naangalia kwenye live data inasomaje. Nikaona inavyosoma kwenye signal generator ndio inavyosoma kwenye live data.

Wire za Heater circuit, kuna mmoja unatoka kwenye Main relay na unakuwa na Voltage ya battery. Huu nao ulikuwa poa.

Huu mmoja uliobaki wa heater circuit unaenda straight kwenye ecu, nikaanza kuufatilia kama unafika kwenye ECU, nikajaribu pin zote kwenye connectors za ECU hamna kitu. Basi jana nikaishia hapo sababu muda ulikuwa umeenda.

Kazi ya leo ikawa kufatilia huo waya mmoja umekatika wapi maana signal haifiki kwenye ecu.

Nikaspend muda mwingi sana kuangalia hizo diagrams baada nilivyoenda kule mbele mahali ambapo connector ya oxygen sensor inaingia nikanote vitu viwili.

1. Kulikuwa na tape mpya imefungwa, (mind you, hiyo gari haina hata miezi 6 toka iagizwe nje).

View attachment 2525300
Hapo baada ya kuitoa hiyo tape.

2. Waya niliokuwa naususpect kwamba una shida ulikuwa umetokeza kwa nje.

View attachment 2525301

Basi nikatoa hilo gamba jeusi na hiki ndio nilichokikuta ndani.

View attachment 2525302

Huo waya umekaatika kama hivyo, na siyo kwamba umekatika wenyewe, bali umekatwa.

Nikauunga huo wire na creamper pin.

View attachment 2525303

Nikarudishia gamba lake, nikapiga tape, nikarudisha kila kitu, nikawasha gari kwenda kutest, kila kitu kiko poa.

Jamaa alikuwa smart kwa waya alioukata sababu katika waya zote nne ndio waya mgumu kuufatilia.

Kiukweli kama ambavyo imekuwa ikishauriwa siku zote humu ndani kuhusu suala ya kuachia mtu gari halafu wewe unaenda kwenye mambo yako, Usimuamini mtu.

Trust get you killed.

Fine, umeamua kumpiga mtu basi angalau usimuharibie gari yake.
Umetumia akili sana kujitangaza kuwa wewe ni fundi wa Euro cars.
Hongera sana mkuu. Nimekukubali
 
Back
Top Bottom