SoC04 Jinsi Wizara ya Afya inavyo weza kushirikiana na Hospitali Binafsi na Wadau wa Afya kuleta ufanisi katika suala la Bima ya Afya

SoC04 Jinsi Wizara ya Afya inavyo weza kushirikiana na Hospitali Binafsi na Wadau wa Afya kuleta ufanisi katika suala la Bima ya Afya

Tanzania Tuitakayo competition threads

tz mickey

New Member
Joined
Apr 23, 2024
Posts
3
Reaction score
4
Ni mara kadhaa sasa kipindi cha hivi karibuni kumeshuhudiwa sinto fahamu katika mfumo wa bima ya afya swala lililopelekea huduma kusuasua na kuleta sinto fahamu.Ifuatayo chini ni moja ya mfano dhahiri wa kuonesha kwamba kuna changamoto katika kuandaa mikakati ya kuboresha mfumo wa bima ya afya.Katika moja ya miaka ya hivi karibuni


Cc
1716519630550.jpg

Chanzo;wizara ya afya

-cha msingi hapa ni kila kitu kifanyike kwa mikakati (strategies) sio kufanya kitu kama kujaribu
Tanzania tuitakayo hasa upande wa bima ya afya tuna tarajia iwe hivi;
1.mabadiliko ya mfumo wa bima ya afya yaende kwa awamu mfano uwepo muda wa utekelezaji na muda wa kufanya maboresho,
-Mfano 2024-2026 (utekelezaji wa sera mpya),2026-2027 (kufanya maboresho)
-tofauti na tulivo shuhudia hivi karibuni ambapo kipindi ambacho wananchi hawakutaraji kukutana na mabadiliko flani mfano kupunguzwa kwa huduma flani ilihali yupo kwenye shida inakua ngumu kuendana na mfumo kutokana na uwepo wa shida katika suala la uchumi binafsi kumudu gharama husika kwa kipindi kifupi.
-hii itasaidia wanufaika kuwa na ufahamu juu ya kinacho enda kutokea na kujiandaa na mabadiliko yeyote hasi.
Screenshot_20240524-061216 (1).png

Chanzo;Eastafrica Redio


2,kuwepo kwa kwa ushirikishwaji wa wadau wa afya na wamiliki binafsi wa hospitali na vituo vya afya Kabla ya kufika muda wa kuelekea kipindi
cha kufanya maboresho,
-serikali isitangaze utekelezaji wa mabadiliko kabla ya kuafikiana na wadau juu ya utekelezwaji wa vipaumbele shauriwa ili mambo yaende sawa.
Mfano kama kipindi cha kufanya maboresho ni 2026-2027 wizara ikutane na wadau kabla ya kipindi maalumu tajwa ili kujadili vipaumbele vya mabadiliko.Ambavyo ndivo vitakua sambamba na ajenda kuu.
Mfano kama muda wa kukaa na kujadili juu ya yaliyo shauriwa na yale yaliyo pangwa kuboreshwa ni mwezi may 2026-august 2026 basi wadau watoe maoni kuanzia mwezi february 2026.
1716519925446.jpg

Chanzo;eastafrica Redio

3.ushirikishwaji wa wananchi kama walengwa wakuu wa huduma katika kutoa maoni juu ya vipaumbele vya mabadiliko mfano changamoto katika mfumo uliopo na namna ya kufanya maboresho.
(hili lifanyike muda mchache kuelekea muda wa kufanya maboresho mfano 2026-2027)
-inakuja kuwa ni vigumu kuendana na mabadiliko kwa sababu yaliyo lengwa kuboreshwa Katika mfumo mpya haya fikii uhitaji tarajiwa wa wananchi.
4.vipaumbele viende kuboresha mfumo kidigitali zaidi kulingana na mabadiliko mengi kwa dunia ya sasa kutawaliwa na digitali.
-Mfano.Napendekeza alama ya finger print iwe sehemu ya utambulisho wa mwanachama wa bima kwamba hata asipo kuwa na kadi au ikitokea hayupo kwenye fahamu za kawaida pia iwe rahisi kutambulika mfano ame zirai ama imetokea shida yeyote inayo mfanya asiweze kuweka utambulisho wake wazi yeye kama yeye aweze kutambulika na apewe huduma.
-pawepo mfumo wa kielektroniki ambao hata ukiweka dole gumba uweze kutoa utambulisho wa uanachama Kwamba upo ama la?
5.Kuja na mpango wa bima maalumu zisizo athirika kwa watu wenye magonjwa ya kudumu(mda mrefu) Au magonjwa ya kurithi, na yanayo wafanya kuwa na kinga dhaifu na kuwa na hatari ya kuugua magonjwa mengine kirahisi na muda wowote ambayo pindi zikitokea changamoto za mfumo wa bima na kukosekana huduma wanakua hatarini zaidi.
Mfano,Wagonjwa wa HIV,wagonjwa wa Magonjwa ya moyo,pumu na mengineyo ambayo yana waweka hatarini kuugua magonjwa yanayo tokana na mfumo wa kinga kuwa dhaifu,magojwa kama malaria,kifua kikuu, Na mengineyo.
-wakiwa na bima maalumu tofauti na wengine ina wajengea mazingira ya kupata huduma mara kwa mara zaidi tofauti na wengine bila shida mfano,kupima (kufanya body check up) na kuwa na uhakka wa kufika kwenye vituo vya afya muda wowote bila kuwa na hofu.
6.Kutokea changamoto kwenye mfumo wa bima za afya ilihali bado wanachama ni wachache ni picha mbaya kwa mpango tarajiwa wa bima ya afya kwa wote.
-Mfano kama wizara na serikali kiujumla isipo weka mfumo wa uhakika wa kiuendeshaji na wananchi kujiridhisha juu ya upatikanaji wa huduma kwa uhakka bila changamoto kama zilizo tokea hivi karibuni zilizo pelekea kukosekana kwa huduma na utata katika utoaji wa huduma,Kwa kutokuwepo baadhi ya huduma kwa wenye bima bado kuna kazi ya ziada ya kufanya zaidi upande wa serikali.
-cha msingi ni kutumia mfumo huu ambao bado una wanachama wachache kujipima juu ya kumudu mfumo wa wanachama wengi au bima kwa wote.

7.Kuwepo namna ya kuheshimu makubaliano katika pande zote mbili Upande wa serikali na wadau wa afya
-mara kadhaa imeshuhudiwa kutokea mvutano baina ya wadau binafsi wa afya na menejimenti ya Serikali upande wa afya ikiongozwa na wizara ya afya,palikua na sinto fahamu zilizo pelekea kukosekana kwa huduma ama kusuasua kwa utoaji wa huduma Mfano mzuri ni hospitali ya agakhan iliyokua miongoni mwa hospitali zilizo sitisha utoaji wa huduma za bima ya afya (NHIF).
-hiyo na ashiria kutokuwepo kauli ya pamoja ya maridhiano baina ya pande zote mbili(serikali na wadau wake).Cha msingi kwa serikali ni kuweka mikakati ya kuheshimu makubaliano ya maridhiano ya pande zote huku maslahi na matakwa ya pande zote kuzingatiwa zaidi.

HITIMISHO;
"kwa pamoja tunaweza kuamua kila kinacho tuhusu wote kama kutakuwa na mikakati sahihi ya kibunifu kwa kuzingatia dhima kuu ya huduma kwa wananchi",,"afya ndio mtaji nambari moja kabla ya chochote kile"
-ukitaka kujua umuhimu wa sekta ya afya,rudia takwimu za madhara ya covid-19 kwa rasilimali watu na shughuli zake (kiuchumi na kisiasa)
 
Upvote 1
Back
Top Bottom