Jinsi ya ku root simu yako ya Android

Mbona mimi hizo rooter zote zimekataa? Hizo apps zote za kuroot zimefail. Sim yang ni Huawei Y520
 
 
Ku root simu za android ni kitendo cha ku unlock operating system ya simu yako ambacho kitakuwezesha kuinstall aia yoyote ile ya application kwenye simu yako mfano operating system,application na games. sitokuwa na maelezo mengi zaidi isipokuwa nitaenda moja kwa moja kukuonyesha ni jinsi gani unaweza ku root simu yako ya android kwa kutmia computer.

Kuna softiware nyingi sana ambazo zinaweza kutumika kufanya rooting ya simu yako lakini kati ya hizo zote ambayo ni nzuri kutumia ili kuroot ni hii iitwayo kingo android root app hii inafanya kazi kwenye device zenye android za version 4.4 kuja chini japo bado inafanyiwa marekebisho ili kuweza kufanya kazi kwenye version ya aina yoyote ile

HATUA
Download na Install KINGO ROOT kwenye computer yako, chukua simu yako ya android kisha chomeka kwenye computer yako kwa kutumia usb, hakikisha usb debugging iko enabled

Run/fungua kingo root kwenye computer yako kicha bonyeza kitufe kilicho andikwa root. rooting itaanza hivyo subiri hadi imalize. katika hatua hii simu yako ita reboot mara kadhaa hivyo iache usifanye chochote


ikimaliza kuroot bonyeza kitufe cha finish ili kureboot simu yako


Angalizo
ili kufanya hii kitu hakikisha simu yako ina betri angalau 50% uwe umeunga computer yako na internet usb cable unayo tumia iwe ni original. Kumbuka rooting wakati mwingine huweza kusababisha madhara kwenye kifaa chako mfano simu kuwa inazimika bila sababu endapo rooting ikiwa haijafanyika kikamilifu.

Simu kufa kabisa endapo kuna makosa yalitokea wakati wa kufanya rooting. na mengine mengi. hivyo fanya hii kitu huku ukiwa unajua kuwa inaweza ikakuharibia simu yako. Kama unasimu yenye android version kuanzio 5.0 na kuendelea usijaribu hii kitu kwani haitokubari na inaweza kukuharibia simu yako
 
Simu yangu ina android version 4. 4. Je inafaa kufanyia rooting ?
 
Njia ipi ni sahihi kwa simu yenye version ya kuanzia 5.0.
 
Mimi Leo najuta ku root simu yangu. Jamaa wako kimya hata ukiwapigia simu kwa namba walizoweka humu na wala hawaji tena kusaidia ama kujibu maswali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…