Jinsi ya ku root simu yako ya Android

Jinsi ya ku root simu yako ya Android

Wadau nimejaribu kuroot htc min na tecno c8 pamoja na huawei y330 zote zimegoma je kuna changamoto wapi
 
Jinsi ya ku ‘root’ simu yako ya Android.

Utangulizi:
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika Mawasiliano, Kuhifadhi kumbukumbu za muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program ambazo huwekwa kwenye mfumo wa simu (Operating System). Programu hizo hubeba maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji kufanyia mambo mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti), Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji wa Simu au Computer ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi yake. Katika miongo michache iliopita zimetengenezwa program nyingi mpya na zenye maboresho makubwa na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika program mbalimbali unaleta ukuaji katika Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia zimeleta urahisi na ufanisi. Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na Kuran), Kamusi, Camera, nk.. vyote vimetengenezewa PROGRAM na kuwa rahisi kuvitumia katika simu muda wowote, mahali popote.

SASA TUJE KWENYE MADA;

Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake. Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho;
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)

Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda Settings – About phone – Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara! kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!! Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni. Sasa watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT’ kua ni kuifanya simu ikubali Program zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers). Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.

JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.

Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root, SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root, Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa kutumia Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya simu za Android. Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha I isearch na kui download. Kwa msaada uliza……

Maandalizi:

(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%

(ii) Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer”

(iii) Sasa nenda Settings>Developer options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)

(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).

Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa download KingRoot 4.0 (or above) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is unavailable’. Chini gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!

--

Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this Device” HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!

FAIDA ZA KU ROOT SIMU:

1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila kuwa rooted!

2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.

3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano (performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root

ZINGATIA:
Rooting inaweza kuharibu kabisa simu yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote). Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki zangu zisizopungua 20 bila madhara yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..

Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’

HITIMISHO:

Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno H6, baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzima!!

Makala na:
Athanas Chriss

0757413078 (Whtsp tu)

Mkuu athanas za mida. nimejaribu kuroot htc min na tecno c8 pamoja na huawei y330 zote zimegoma je kuna changamoto wapi
 
"manfive, post: 14975067, member: 281456"]Maisha murua kabisa baada ya kufanikiwa kuroot Huawei yangu asante kwa mleta uzi[/QUOTE]
Ata yangu nimeiroot setting hiyo naipata wap
 
Mkuu mm natumia samsung galaxy s5 ina version ya marshmallow. Je ni root kwa rooter ipi ambayo haitumii komputer?
 
naomba maelekezo namna ya kutoka android version ya 4.3(jellybean) had 4.4.4(kitkat) au 5.1.1(lollipop) bila kutumia computer wala wi fi. simu yangu ni galaxy s3. naomba kwa lugha nyepes tafadhar kama ya Athanas( mi ni slow learner). simu nilishairoot kwa kingsroot ingawa sijaona faida ya ziada.
 
Tumia Cynanogen Mod
 
ndo nini hiyo na ifanyikaje? licha ya utetezi wangu bado hivyo.
 
Wengi tumekuwa tukijiuliza maswali kuhusu ku ROOT simu
Hapa kuna maelezo machache yanayoweza kukufungua,
Ili kufahamu fungua link hapa chini

=========

Nini maana ya ‘Kuroot’ simu yako? #Android #Rooting

Kuroot ni nini? Kuroot simu ya Android ni jambo linalofungua geti kuu la programu endeshaji hiyo na hivyo kukuruhusu kufanya mambo mengi zaidi katika programu endeshaji hiyo kuliko ilivyo kawaida.
Tushaulizwa mara kadhaa juu ya jambo hili na ata baadhi kuuliza jinsi ya kuroot simu zao. Haya ni yote ya kufahamu kuhusu ‘rooting’.

root-android.png

Kwa kiurahisi
Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta ya Windows basi utakuwa unafahamu ya kwamba pale kompyuta ikiwashwa inakupa chaguo la kuingia kama mtumiaji mkuu yaani Administrator – ambapo ukiingia kama Administrator unaweza fanya mengi zaidi katika upakiaji wa programu na ata katika masuala ya mafaili.

Pia kuna uwezo wa kuingia kama Mtumiaji Mgeni – yaani Guest. Ambapo hapa hautaweza fanya mabadiliko mengi katika kompyuta hiyo, utabanwa katika mambo mengi yanayohusu uwekaji programu na ata kufanya mabadiliko ya mipangilio (settings) ya kompyuta hiyo.

Toleo la Android katika simu yako – iwe Samsung, Huawei, Tecno n.k linavyokuja linakuwa linakupa uwezo wa kufanya mabadiliko ya kama mtumiaji mgeni (Guest) katika simu hiyo.

Tendo la kuroot ndilo litakalokupa uwezo wa mtumiaji mkuu, yaani Administrator katika simu hiyo na hivyo utaweza fanya mengi ata yale yanayoweza haribu kabisa programu endeshaji hiyo.

Je utaweza fanya yapi kutokana na kuroot simu yako?
android-root-1.png

Ukiroot programu endeshaji ya Android ya simu yako utaweza kufanya mambo kama vile

  • Kuweka apps ambazo kwa hali ya kawaida isingewezekana kabisa kuwekwa kwenye simu
  • Kufuta (delete) apps na programu zilizokuja na simu husika ambazo kwa kawaida huwa huwezi zifuta. Apps hizi zinaitwaga Bloatware
  • Kusasisha au kubadilisha kabisa toleo lako la Android. Ata kama mtengenezaji simu husika, iwe Samsung n.k bado hajakupa sasisho rasmi kwa ajili ya simu yako kuweza kupata toleo la kisasa zaidi la Android, kwa kuroot unaweza fanikiwa kupakia toleo la kisasa au ata kubadili kabisa
  • Kufanya mabadiliko mengine mbalimbali kulingana na utakacho katika muonekano na utendaji kazi wa simu yako
Njia za Kuroot
Kuna njia nyingi sana kwa sababu suala la kuroot simu linategemea mambo mengi sana, mara nyingi njia ya kuroot simu flani haifanani na ya kuroot simu nyingine. Tofauti zinakuwa kwa kampuni kwa kampuni ya simu na ata saa nyingine tofauti zinakuwa kwa aina ya simu ata kama zinatoka kampuni moja.

Katika kuroot kwenyewe bila kujalisha app au programu au hatua utakazotumia, njia kuu ni mbili;

  • Ya kutumia makosa ya programu endeshaji – Kupitia kufahamu makosa, yaani ‘exploits’ basi watengenezaji apps au programu wanaweza fanya programu/app iingie ndani kabisa ya Android ya simu yako na kukupa uwezo wa Admin, yaani simu ikawa ‘rooted’
  • Kwa kuweka ‘Custom Recovery’ – Hii ni njia isiyo salama zaidi kwa kifaa chako ila pia ndiyo moja ya njia inayokuwa mara nyingi tofauti tofauti kwa kila kifaa.
Muhimu kufahamu
  • Makampuni yenyewe ya simu sio yanayotoa njia za kuroot na kwa kiasi kikubwa huwa hawashauri ufanye jambo hili. Kama simu ina warranty basi kitendo cha kuroot kitaondoa sifa ya warranty hiyo.
  • Ukikosea njia au ata kama umefanya kila kitu sahihi kama mambo yasipoenda vizuri basi Android inaweza nasa katika hali inayoifanya simu yako isiweze tumika. Hali hii inaitwa ‘Brick’ – yaani jiwe. Mara nyingi hii inamaanisha itakubidi uanze upya.
Tutakuletea njia mbalimbali maarufu za kuroot simu lakini kama unajiamini na unataka fanya mwenyewe basi mtandao wa XDA ni moja ya sehemu muhimu ya kuanzia. Kitu muhimu sana ni kuhakikisha unafuata maelekezo na kutumia mafaili husika kama maelezo ya jinsi ya kuroot simu hiyo husika. Njia hazifanani.

Je ushawahi kuroot simu yeyote? Waambie wengine ilikuwa ni simu gani na ulitumia njia gani?
 
sidhani kama ni sahihi kusema root ni sawa na administrator na simu isio na root ni sawa na guest. kama tunatoa mfano wa computer

root = local disk c
bila root = libraries

simu isio na root ni kama computer inayokuja bila local disk c huwezi ona mafile ya windows (system android) huwezi badili mafile ya application, etc

angalia hii picha
LzBkPX5.png

hilo ndio folder mama la android kwa lugha nyengine ndio Root mahala mafolder yote yanapoanzia,

ukiangalia vizuri hio picha utaona kuna folder linaitwa sdcard, folder hilo pekee ndio unaruhusiwa kulifungua kwenye simu isio na root na ndani ya folder hilo ndio kuna picha ulizopiga za camera, miziki, video zako, media za whatsapp na mambo yote uliodownload na kutumiwa. hivyo kiurahisi

Root = mafolder yote
bila root = folder la sdcard
 
Mm yangu ni nokia xl dual sim rm-1030 je naweza kuiroot na kuinstall google play maana nikifata procedure ya xda kuroot kwa frama root yaan bila computa inagoma kuroot pia nikitumia computa nikiconnect simu yangu inashindwa kusoma kwenye manager ya kwenye pc inakuwa inaload tuu mda wote naomba msaada nn tatizo ?
 
Kiongozi hiyo si window phone? Sina ujuzi sana kama unaweza weka play store, maana play store ni kwa android.
 
Back
Top Bottom