Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Amua kuwa unaacha tarehe 18.03.2014, tarehe husika ikifika unaiona sigara kama kituo cha jeshi then you done!

Elewa kuwa hakuna dawa ya kuacha sigara ila ni UAMUZI MGUMU tu.

Ni vigumu sana mwanzoni unapoacha kwani utajisikia hali mbaya ila vumilia.
 
nitumie njia gani au dawa gani ya kuacha kabisa kuvuta sigara


MADHARA YA KUVUTA SIGARA(TUMBAKU) KIAFYA



1.shinikizo la damu ambalo husababisha ugonjwa wa moyo, stroke
2.pumu
3.matatizo ya kifua
4.kansa ya modo
5.kansa ya mapafu
6.kansa ya figo
7.kansa ya matiti
8.kansa ya tumbo
9.kansa ya koo
10.watoto kuzaliwa na uzito mdogo na kuwa na matatizo ya kiafya ambayo h humwezesha mtoto kufa haraka akiwa bado mchanga
11.matatizo ya meno
12.uvimbe katika ubongo
13.ngozi kunyauka/kuwa na makunyanzi mapema


KWA MAMA MJAMZITO na anaye vuta sigara matokeo ya ujauzito mara nyingi hua;


1.kusababisha mental retardation (utaira wa akili) kwa mtoto mchanga
2.mtoto kuzaliwa katika uzito mdogo sana na kuwa mwepesi kupata magonjwa haraka kutokana na udhaifu wa afya
3.kufariki kwa mtoto ghafla (SIDS)
4.udhoofu wa viungo vya mwili wakati mtoto bado yuko tumboni kwa mama na anapotoka (ulemavu)


Sio hivyo tuu, kukaa karibu na mvuta/wavuta sigara pia kuna madhara yake makubwa pia (second hand smoke). Tafiti zinaonyesha kwamba, watu wengi wana umwa na magonjwa yaliyo chronic pia mara nyingi hukutwa kwamba at some point in their lives walikuwa exposed sana kwenye moshi wa sigara (second hand smoke).


Tumbaku inamchanganyiko wa kemikali za madawa mengi ambayo yanaashiria katika kusababisha magonjwa makubwa na kuzorota kwa afya. Moja wapo ikiwa ni dawa ya kulevya iinayoitwa NICOTINI. Mtu anapovuta sigara, anapotafuna tumbaku, hilo dawa la kulevya la Nikotini hufyonzwa moja kwa moja kwenye mfumo wa damu (bloodstream).


Hii Nikotini inapofyonzwa kwenye damu hufanya tezi za adrenaline kusisimka na kutoa hormoni inayoitwa epinephrine ambayo nayo hii hormone huenda na kusisimua mfumo mkuu wa nerves situation ambayo husababisha moyo kupiga kwa kasi kupita kipimo na kufanya BLOOD PRESSURE kupanda.


Vitu vingi hutokea ndani ya mwili wakati wa kuvuta sigara ambavyo vinasababisha watu wengi ambao wanavuta ama kutafuna tumbaku kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu.


Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara


Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.


Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.


Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.


Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.


Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.


1* Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?


2*Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.


3* Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.


4*Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.


5*Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.


6*Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.


7*Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.


8*Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.


Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
 

Attachments

  • Madhara ya kuvuta Sigara.jpg
    Madhara ya kuvuta Sigara.jpg
    31.7 KB · Views: 187
  • Stop smoking.....jpg
    Stop smoking.....jpg
    22.9 KB · Views: 173
Natumaini mu wazima,nimekua nikijaribu kila njia niachane na uvutaji wa sigara ila nashindwa,saa zingine naweza kukaa hata wiki nzima bila kuivuta ila kukitokea kitu kidogo cha kunichanganya akili baasi lazima nitavuta tena kwa kuziunganisha hata tano kwa mpigo.

Jamani kama kuna mtu anaweza akanielekeza dawa,nipo tayari kuitafuta kwa gharama yeyote maana imeshakua kero kwangu,nachukia tabia hii ila nahisi kama nimenasa kwenye mtego"fegi".Thanks
 
Meditation na kunywa maji kwa wingi
Njia nyingine kidogo ina ukakasi lakini ni tiba hasa ,ukisikia hamu ya sigara na hata bangi washa sigara au msokoto wako halafu mchukue kunguni mchome pale kwenye sigara halafu vuta moshi ukifanikiwa kuimaliza hiyo sigara au huo msokoto ndio mwisho wa wewe kuvuta
 
Ok...mi nimefanikiwa kuacha sigara baada ya miaka kama mitano ivi, naamini dawa ni wewe mwenyewe,kaa chini ainisha hasara za sigara,alafu angalia faida zake,hasara ni nyingi kubwa ni ya kiafya lakin pia kuna watu hutaweza kukaa nao au kuwa nao karibu sababu ya harufu na aibu,basi nikajiwekea malengo,kwanza nikaanza,leo sivuti,siku ilipoisha nikasema pia kesho sivuti,kama unavoona ni malengo madogo na yanatekelezeka,sio rahisi inahitaji uvumilivu piaikaisha wik,nkasema kama wik nimeweza basi wik ijayo sivuti,mpaka ikawa tabia,unapokuwa kwenye hiyo program jiepushe na washkaj wavutaj au mazingira yatayofanya upate hamu ya kuvuta,ilie nicotin iliyo mwilini itkuw inapoteza nguvu na mwishowe inaisha hata hamu husikii tena,ukiskia harufu unajiskia vibaya!
 
Ok...mi nimefanikiwa kuacha sigara baada ya miaka kama mitano ivi, naamini dawa ni wewe mwenyewe,kaa chini ainisha hasara za sigara,alafu angalia faida zake,hasara ni nyingi kubwa ni ya kiafya lakin pia kuna watu hutaweza kukaa nao au kuwa nao karibu sababu ya harufu na aibu,basi nikajiwekea malengo,kwanza nikaanza,leo sivuti,siku ilipoisha nikasema pia kesho sivuti,kama unavoona ni malengo madogo na yanatekelezeka,sio rahisi inahitaji uvumilivu piaikaisha wik,nkasema kama wik nimeweza basi wik ijayo sivuti,mpaka ikawa tabia,unapokuwa kwenye hiyo program jiepushe na washkaj wavutaj au mazingira yatayofanya upate hamu ya kuvuta,ilie nicotin iliyo mwilini itkuw inapoteza nguvu na mwishowe inaisha hata hamu husikii tena,ukiskia harufu unajiskia vibaya!
Hii ndio dawa ya kweli ya kuacha kuvuta ambayo hata mimi niliitumia nikaacha kabisa kuvuta: strong personal will to stop smoking. Hakuna sijui vidonge au unga wa kunywa kusaidia kutibu tatizo la uvutaji.
 
Kwani ulianzaje kuvuta?nini kilikushawishi kuvuta sigara? mimi naona tatizo lako ni la kimazingira, jaribu kufikiria aina ya watu wanaokuzunguka, harafu uone ukweli.
 
Hivi huyu bwana Mzizimkavu hawezi kua hii dawa?

MziziMkavu hakosi dawa yeyote utakayoitaka na hata ukitaka maombi ya kanisani au msikitini pia anayo, ila dawa ya kuacha sigara kama ulivyoambiwa hapo juu ni wewe mwenyewe kuamua tu hutaki basi, kila kitu mpaka utumie dawa!
 
Mimi nilikuwa mvutaji lakini nimeacha kwa ile mbinu wazungu wanaita Cold turkey. Ukiamua unaweza ila lazima kwanza kile kitendo cha kuvuta sigara ukichukie.
 
MziziMkavu hakosi dawa yeyote utakayoitaka na hata ukitaka maombi ya kanisani au msikitini pia anayo, ila dawa ya kuacha sigara kama ulivyoambiwa hapo juu ni wewe mwenyewe kuamua tu hutaki basi, kila kitu mpaka utumie dawa!

Kwahiyo jamaa ni maltipapasi..
 
Wasiliana na tb joshua ukipata yale maji yake ya baraka hutakaa uvute sigara tena, mimi nilitumia nikafanikiwa kuacha baada ya kuwa mvutaji kwa miaka 29,
 
wakuu ni zaidi ya miaka 5 najaribu kuacha sigara lkn nashindwa.naombeni msaada wenu.shukrani
inafu iz inafu
 
Weka nia tu..jipangie badala ya kuvuta tafuta kitu kingine cha kufanya kwamfano badala ya kununua sigari nunua pia taratibu utaacha.kitu cha kwanza kua na nia ya kuacha.
 
mkuu jaslaws nimeshanunua pipi kali mpk mifuko inajaa lkn wapi.mbaya zaidi kwenye vikao vya jioni navuta sana
 
(1) Weka nia, (2) punguza kama unavuta 8 vuta 4 baada ya kuzowea punguza na kubaki 2 kisha 1 kisha nusu,ukifikia hatua hii ujue umekaribia mwisho, anza kuvuta marambili kwa siku kisha maramoja kwa siku, ukoizowea hari hii anza kutumia pipi kifua kila upatapo hamu ya sigara. kumbuka hautakiwi kuacha ghafu ra
 
wakuu ni zaidi ya miaka 5 najaribu kuacha sigara lkn nashindwa.naombeni msaada wenu.shukrani
inafu iz inafu

Mimi binafsi niliwahi kuwa mvutaji mkubwa wa sigara, mpaka pakti mbili kwa siku.

Niliamua tu siku moja kuacha kuvuta, miaka 15 nyuma, mpaka leo AlhamduliLlah sijavuta tena.

Ni kuamua tu.
 
Back
Top Bottom