Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

nashukuru sana kwa michango yenu.ngoja nifunge mkanda na kuanza hili zoezi
cc.
mapolomoka,faizafoxy
 
Njoo inbox dawa ninayo, yaani hiyo ukianza kuitumia ukivuta sigara utatapika vibaya na unaweza ukazirai
 
Mimi binafsi niliwahi kuwa mvutaji mkubwa wa sigara, mpaka pakti mbili kwa siku.

Niliamua tu siku moja kuacha kuvuta, miaka 15 nyuma, mpaka leo AlhamduliLlah sijavuta tena.

Ni kuamua tu.

bila shaka sasa hivi unajiburudisha na 'kitu cha Arusha' huku ukichanganya na miraa!
 
Mimi binafsi niliwahi kuwa mvutaji mkubwa wa sigara, mpaka pakti mbili kwa siku.

Niliamua tu siku moja kuacha kuvuta, miaka 15 nyuma, mpaka leo AlhamduliLlah sijavuta tena.

Ni kuamua tu.

Kumbe bibi ulikua smoka eeh
 
Tumia pipi Kifua kila Wakati unaposikia hamu ya kuvuta .also fua nguo zinazonukia sigara na Epuka mawazo yanayoweza kupelekea kuvuta.
 
Wana JF uvutaji Sigara una madhara makubwa kwa Afya, naomba kwa wenye kujua ni njia zipi au hatua zipi za kuchukua kama mtu anataka kuacha tabia ya uvutaji Sigara?
Karibuni sana.
 
nimekuwa mvutaji mzuri wa sigara kwa muda wa miaka 8,nilikuwa navuta 5 mpaka 6 kwa siku. nilianza kama utani baada ya kuathiriwa na moshi wa wavutaji nami nikasema ngoja nijaribu, baadaye nikafanya kweli na kuwa mvutaji mzuri kuliko hata walionifundisha. sasa nina wilki 3 sijavuta na wala sitaki kunusa hata moshi wake.
nimekwenda hospitali kuangalia afya nimekuta nina afya nzuri pia nimeshauliwa niwe nakunywa maji ya uvugu vugu zaidi ya lita nne kwa siku.
na wewe kama ni mvutaji nakushauri kuanzia sasa acha.

vinavyokatazwa ndivyo vinavyopendwa.

uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako kama unavuta alafu huli chakula kinachoeleweka.
 
Back
Top Bottom