SoC01 Jinsi ya kuacha Tabia usiyoipenda na kujenga tabia unayoitaka

SoC01 Jinsi ya kuacha Tabia usiyoipenda na kujenga tabia unayoitaka

Stories of Change - 2021 Competition

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Je umewahi kutamani kuacha au kupenda kuwa na tabia zifuatazo?
  • Unachukia sana kunywa pombe lakini hujui jinsi ya kuacha kunywa pombe​
  • Unachukia sana tabia ya kuvuta sigara lakini hujui utaachaje​
  • Unataka uwe msomaji wa vitabu lakini unashindwa unaona uvivu kila unapojaribu​
  • Hupendi somo flani chuoni lakini lazima ulisome na ulifaulu, unataka ulipende lakini imeshindikana​
Basi nakuletea njia rahisi ambazo zitakusaidia kuacha tabia yeyote usiyoipenda na kujijengea tabia nyingine unayoitaka

Pombe, sigara, bangi huzalisha furaha bandia kwa muda, ikiisha nguvu kichwani furaha nayo huyeyuka kama theluji, watu wengi wanatumia pombe,sogara,bangi n.k wakiamini kuwa zinawaletea furaha ya kweli. Hii ni hatari kwa afya ya akili

Jinsi ya kuacha tabia usiyoipenda mfano unywaji wa pombe au sigara.
  1. Chagua tabia yeyote nzuri unayotaka kuwa nayo mfano usomaji vitabu, kuandika makala, kutype kazi za ofisini ulizobakiza n.k​
  2. Ukienda kunywa pombe beba kitabu chako, au au kalamu na karatasi yako tafuta sehemu nzuri kaa hapo agiza bia yako anza kunywa taratibu huku ukisoma kitabu chako fanya hivyo ukichoka funga kurasa nenda nyumbani.​
  3. Zoezi hilo lifanye kila unapojisikia kwenda kunywa pombe au kuvuta sigara.​
  4. Baada ya siku 40, nenda hapo hapo au mahali unapoenda kupata pombe kila mara mfano Bar agiza maji badala ya pombe kisha endelea na zoezi la kusoma kitabu chako. Hii itakuhamisha kutoka kwenye kupenda pombe itakupereka kwenye kupenda kusoma vitabu na kunywa maji na hatimaye utakuwa umeweza kuachana na pombe kabisa​
Jinsi ya kupenda somo gumu unalolichukia (kwa wanachuo, wafanyakazi n.k)
  1. Tafuta kitu chochote cha kutafuna au kinywaji baridi unachokipenda mfano popcorn, pipi, big g, carot, au juisi​
  2. Anza kulisoma somo usilolipenda huku ukitafuna popcorn taratibu, au huku ukinywa juisi mdogo mdogo, au huku ukisikiliza mziki uupendao taratibu​
  3. Fanya hivyo mara kwa mara kwa mara zisizopungua 40 utajikuta unapenda hilo somo bila kutumia juisi, popcorn wala Big G​
Njia hii ni ya kisayansi na ni ya gharama nafuu, unaweza kuiona ni ya kitoto lakini inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa

Unaweza kuwa mbunifu pia mfano kama hupendi kufanya mazoezi na ila unatamani kuwa na tabia ya ufanyaji mazoezi basi weka earphone zako masikioni weka mziki uupendao kisha anza jogging. Ukifanya hivyo mara 40 utajikuta unapenda mazoezi bila kusikiliza mziki.

Nawasilisha
 
Upvote 5
Back
Top Bottom