Jinsi ya Kuepuka Kuibiwa Mafuta Unapojaza.....

Jinsi ya Kuepuka Kuibiwa Mafuta Unapojaza.....

Hii ya kidumu kuna "sheli" flani hivi maeneo ya Tegeta waligoma kuniwekea kwenye kidumu. Nilipowauliza kwanini wakanambia ni kwa sababu za kiusalama... nami kwa sababu za kiusalama nikaondoka salama na fedha yangu ikiwa salama...

Sitakagi ujinga kwenye usalama wa pesa yangu... malabuku zao na nusu!!
Aahaahaaaaaa
 
DAA KWA KWELI WIZI WA MAFUTA UMEVUKA MIPAKA...MM NAONGEA NA KAKA YANGU MJESHI ANANIPA YALE MAKONTENA YAO NAWEKA LITA ISHIRINI NKIFIKA HOME NAJAZA KWENYE TANGI
Wewe ndo unashirikiana na kaka yako kuiiba mafuta ya serikali eeh. We ngoja
 
Pump imechezewa au haijafanyiwa calibration muda mrefu. Kuna wakala wa vipimo WMA kazi yake ni hio kukagua mita na vipimo vingine kama 1kg means 1kg au 1L means 1L etc
Sasa nimeelewa kwa nini baadhi ya vituo vya mafuta hujaa sana magari mpaka kupanga foleni (huwa nashangaa sana) wakati vingine vinakuwa na gari moja au hakuna kabisa.

Huwa najiuliza hawa watu hawana shughuli za kufanya mpaka kupanga foleni ya kujaza mafuta?

Na mimi nisivyopenda msongamano huwa naenda vile visivyokuwa na magari[emoji23]
 
juzi nilimwambia aniwekee mafuta ya 80000 akajikuta anaweka ya 180000, yaani hapo niliwaibia wao. sasa kazi kwake mhudumu, halafu alikuwa ni mwanamke, na hivyo wanawake SIWAPENDI ,nikaondoka zangu huyoooooooooi
huyo atakuwa alishawachapa sana wateja wengine sasa hiyo inaitwa kulipa. ila pia inaweza kuwa bahati mbaya tu kujisahau.
 
Mungu anakuona. Kuna mtu alinisimulia stori kama hii au nilisoma JF alitoa 40,000 sasa muhudumu na haraka zake akaweka auto mode akabonyeza 400,000 akaenda kujaza gari ingine upande wa pili! Anakuja kushtuka gari imejaa full tank mafuta yanamwagika pump yake inasoma 150,000!
gari gani hiyo mkuu pronto, manake hilo tank tumbo la mamba
 
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusu watu kuibiwa mafuta kwenye vituo. Sio mbaya kuelimishana nini cha kufanya ili kuepuka wizi huu.

Kabla ya kujua nini cha kufanya ni vizuri tujue njia kuu zinazoweza kutumika kukuibia mafuta.
1.Kukuwekea mafuta bila ku-reset mashine. Yaani anakuja bodaboda au gari anaweka 5000/10,000 ukija wewe mhudumu anaendelea kukuwekea kuanzia 5000/10,000 ile ile.
2.Pump iliochezewa, yaani kwenye lita moja yenyewe inaweka ml 700 etc.

Njia za kuepuka wizi huu ni hizi
1.Hakikisha mashine ime-reset 0000 kabla ya kuwekewa mafuta. Ukifika kituoni acha uboss, ikibidi shuka kwenye gari hakikisha mhudumu kaanzisha 0000
2.Nenda na kidumu cha lita 5 mwambie akujazie mafuta lita tano, angalia kidumu kilivyojaa na geji(kwenye pump) inavyosoma.

Ukifanya hayo mawili hapo huibiwi mafuta hata siku moja. Kingine nashauri uchague kituo kimoja uwe unaweka mafuta hapo hapo. Wakikuzoea hawawezi kukufanyia uhuni,pia lolote likitokea unajua ni wao tu.

Lakini ukiweka mafuta randomly hapa 3000 pale 10000 unaweza ukawa unamlaumu mtu bure kumbe uliibiwa jana ulipoweka 10,000 umekuja kushtukia leo ulipoweka 20,000.

Mimi huwa naweka mafuta weekly,thamani ile ile ya hela kazi yangu ni kuangalia idadi ya lita na mshale umefika wapi, siku zote mshale unakuwa eneo lile lile,hawezi mtu kuniibia.
Ni kweli boss lakn duuu ni shidaaaah
 
Kwa kweli hapo labda umix JiLusekelo na Valeur afu ushushie na safari lager

Ha ha ha, hapo kweli unaweza kufika hiyo level, na pembeni kuwe na dogo dogo sasa ili akuongezee confidence.
 
Self-service gas pumps....kiboko ya wajanja wajanja.

Unajiwekea mafuta kwenye gari yako bila wasiwasi.

IMG-20160723-WA0020.jpg
 
Hii ya kidumu kuna "sheli" flani hivi maeneo ya Tegeta waligoma kuniwekea kwenye kidumu. Nilipowauliza kwanini wakanambia ni kwa sababu za kiusalama... nami kwa sababu za kiusalama nikaondoka salama na fedha yangu ikiwa salama...

Sitakagi ujinga kwenye usalama wa pesa yangu... malabuku zao na nusu!!
[emoji23][emoji23]
 
Ha ha ha, hapo kweli unaweza kufika hiyo level, na pembeni kuwe na dogo dogo sasa ili akuongezee confidence.

Yeah... huyo ndo anaongeza vocabularies na swaga za kina Chris Tucker... LOL
 
Mimi huwa natumia njia ya pili ya kuweka kwenye kidumu,sasa huwa nawaacha wahudumu hoi sana,maana nilivyo na ninavyofanya sifananii kabisa.(maana nipo kibosi bosi )
umenichekesha sana, hapo watu wanakuona kama hauko sawa kumbe mwenyewe una yako hapo hutaki kuibiwa akili yako unaijua mwenyewe mjini hapa. Nimeipenda sana hii
 
Nilishashuhudia jamaa full tank capacity 60 ltrs anadaiwa alipe 78ltrs!
Duh yaani tank yake full capacity 60lts ila pump inasoma 78lts?!! Ndio haya niliosema display inaonesha lita 1 pump inajaza 700ml.
 
Kwa hiyo ukicornfirm kwa kidumu ukakuta imesoma sahihi, hakuna namna nyingine ya kuibiwa ukiacha hiyo ya kureset?
Namna ingine ya kuibiwa ni ile ya Bajaji/bodaboda aliekutangulia kuweka ya Buku 3 halafu ukija wewe unaetaka ya Buku 20 mhudumu harudishi mita mwanzo, bali anaanzia hapohapo ilipoishia bajaji na kuendelea, unajikuta umewekewa ya buku 17 only,

Ogopa sana Sinza Kijiweni na Ubungo Mataa
 
Back
Top Bottom