Salaam, Shalom!!
Salamu hapo juu itoshe kukujulisha kuwa walengwa wa HOJA hapo juu ni Wana wa Mungu, ni wale ambao wanahangaika,wanafanya KAZI Kwa bidii, wanajitenga na UOVU, walipao ZAKA nk nk, lakini Bado malengo Yao hayafanikiwi Kwa hatua za kuridhisha.
Neno la Mungu lasema katika
( Yakobo 4:3)
"Mwaomba Wala hampati, Kwakuwa Mwaomba vibaya, Ili mvitumie Kwa tamaa zenu wenyewe"!!
Ujumbe huo hapo juu haukuandikwa Kwa ajili ya wapagani, Bali Wana wa Mungu,
Hivi kijana, unasugua goti ukiomba Mungu akujaalie upate deal zuri katika KAZI zako Ili upate gari Kwa ajili ya kumfurahisha mchumba wako, Unadhani utajibiwa kirahisi?
Unapiga goti ukimwomba Mungu akutajirishe Ili maadui wako wakuheshimu, Unadhani utajibiwa kirahisi?
Mwingine uko kitandani unaumwa cancer au gonjwa hatari, ukimwi Kwa Mfano, unamwomba Mungu akuponye lakini huweki AGANO nae kuwa ukiponywa utafanya nini Kwa ajili ya Mungu, sahau kujibiwa.
Mimi Rabbon, nilipooa, nilikuwa napata shida sana Kila Jumapili sababu palikuwa na shida sana ya USAFIRI, nilimwomba Mungu anijalie nipate gari Ili gari Hilo linisaidie kuwahi Kanisani jumapili na litumike kusaidia huduma Kanisani, na nilimwomba Mungu anijalie ninunue gari Hilo baada ya mwaka mmoja sababu sikuwa na pesa za kutosha, Cha kushanga nilipata gari ndani ya miezi SITA tu.
JINSI YA KUJIBIWA MAOMBI YAKO KIRAIHISI!!
1. SIASANI
Ikiwa umepanga kugombea, na ungependa Mungu akusaidie kushinda Udiwani, ubunge, Urais nk nk, weka AGANO na Mungu, Mwambie hivi, Mungu wangu ukinifanikisha kuwa mbunge, nk nk, nitahakikisha Ufalme wako Mungu unaingia bungeni, nitahakikisha HAKI inatawala ndani ya bunge na Kwa wananchi, utafanikiwa kirahisi.
2. KIUCHUMI
Wengi mmefungua biashara na mnamwomba Mungu awatajirishe, lakini hamsemi mkipata utajiri mtafanya nini Kwa ajili ya INJILI. Hamuweki AGANO na Mungu kuwa mtatumia vipi utajiri wenu kuhakikisha watoto mitaani wanaishi vizuri na kupata mahitaji Yao, wajane nk nk!!
3. KIJAMII
Wengi mnatamani mfanikiwe katika huduma mzifanyazo, mnatamani kufahamika, lakini hamweki AGANO na Mungu kuhusu jinsi mtakavyitumia kufahamika kwenu kuwaleta wengi Kwa kristo, kamwe hamtatoboa msipofanya hivyo, sababu mnaomba vibaya Ili mpate hayo Kwa tamaa zenu.
4. MAHUSIANO NA NDOA.
Ulipokuwa single, bachelor ulimtumikia Mungu vizuri, ukaomba Mungu akupe NDOA, Kweli Mungu kakupa mume/ mke mzuri, Cha ajabu tangu umeoa, Kanisani huendi tena, maombi hufanyi tena, huduma huendi tena,
Sasa Kwa kuwa Mungu anapenda umtumikie kama zamani, ataruhusu huyo mume akutese vilivyo, huyo mke akutoe JASHO Kwa kukupiga matukio, Ili urudi tena Kanisani, urudi magotini ujue yupo Mungu na urudi kumtumikia, makinika!!
5. UJENZI.
Unaomba Kila kukicha, unamwomba Mungu akusaidie Ili upate nyumba Yako Ili kuondokana na adhaa akupazo mwenye nyumba wako wa sasa. Utachelewa sana, maana unakosea kuomba.
Omba hivi, EE Mwenyezi Mungu, ukinijalia kujenga nyumba nzuri, kubwa, nitahakikisha natenga chumba special Kwa ajili ya maombi, nitatenga chumba/ nyumba special Kwa ajili ya Wageni ambao ni watumishi wa Mungu, nyumba hiyo itakuwa na standard zote za nyumba Bora Ili wahubiri wajapo katika Kanisa letu, wasilale nyumba za wageni zinazotumika na watu wengi wasio waaminifu, nitahakikisha, nyumba yangu / chumba changu Kwa ajili ya kupokelea watumishi wa Mungu ni kisafi na kitakatifu, ambatisha AGANO lako na sadaka.
Amini nakuambia, Mungu hawezi kataa offer hiyo, atakufanikisha haraka sana.
Yatosha Kwa sasa, mbarikiwe🙏
Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala hii;
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
Karibuni 🙏.