Jinsi ya kufanya miujiza (Education is power)

Jinsi ya kufanya miujiza (Education is power)

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,887
Nawasalimia wana JF wote.

Leo nipo hapa kuongelea swala hili la kufanya miujiza na uponyaji.
Kwanza awali ya yote ningepeda kutoa utangulizi kama ifuatavyo.

UTANGULIZI
Sisi binadamu tuko na nguvu kubwa sana ndani yetu. Ni kitendo cha kujua jinsi ya kuitumia. Nguvu tuliyonayo ni nguvu ya kiroho ambayo huwezi ukaiona kwa macho ya damu na nyama lakini unaweza ukaitumia na ikaleta matokeo katika ulimwengu wetu huu.

Nguvu tuliyonayo sisi haijui kuwa hiki chema au kibaya ni mtu tu atakavyo amua kuitumia. Wengine wanaitumia kufanya uchawi lakini wengine wanaitumia kufanya miujiza ya uponyaji. Ni wewe tu utakavyoamua kuitumia hiyo nguvu. Yenyewe ipo.

NAMNA GANI WAWEZA KUIPATA HIYO NGUVU.
Watu wengi sana duniani wamekuwa hawajui hawa watu wanaofanya miujiza au wanaofanya uchawi wanapata wapi nguvu? Je hao watu ni special one? Mimi nina sema hapa ni kwamba tumesahau au tumekataa maarifa na tukakubali kuwa tunasimuliwa na kuwa sio watendaji.
Kwa wale mnaosoma biblia (Hosea 4:6 inasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa....."). Inamaana watu wamekosa maarifa ndio maana waenda tu bila kujua nini cha kufanya.

Nguvu yetu ya kufanya makubwa ipo ndani ya nafsi zetu (Consciousness). Au ninaweza kusema sisi watu tunaishi katika ulimwengu wa aina mbili(Ulimwengu wa damu na nyama pia Ulimwengu wa kiroho). Sasa ulimwengu wa kiroho ndio unaguvu na ndio chanzo za nguvu zote. Na ndio uhalisia wetu sisi na ndio reality yetu sisi.

Sasa basi kiwango cha kutumia nguvu au kuwasiliana na nafsi zetu unapungua kadri umri wetu unaposogea. Mtoto anapozaliwa asilimia kubwa sana anakuwa yupo pamoja na nafsi ya ili tatizo lake anakuwa ni mgeni duniani hajui kuongea hajui chochote kilichopo duniani. Kwamaana hiyo hawezi akafikisha ujumbe wowote. Lakini kwakuwa tumekosa maarifa mtoto anapoanza kukua tunaanza kumfundisha vitu vya dunia tu na kusahau asili ya ni nini. Jambo hilo ninamfanya huyo mtoto awe mbali na nafsi yake. Kadri anavyo zidi kukua anazidi kuwa mbali.

Njia yakuweza kuwasiliana na nafsi zetu ni kuhakikisha tunafunga milango ya fahamu ya miili yetu (macho, masikio, mawazo, ngozi nk). Tunapofunga milango hiyo ya fahamu ndio tunakuwa na uwezo wa kuanza kuwasiliana na nafsi zetu.
Kwa wale wasomaji wa biblia: (mathayo 6:6 "
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.")

Jambo kubwa ninalojaribu kuongea hapa ni kuwaweka sawa waumini wa dini ya kikristo waelewe ni mambo gani yameandikwa kwenye kitabu chao na kwanini hawayafuati.

Njia ili uweze kuwasilina na nafsi yako kwa ufupi ni kufanya meditation (Sina neno zuri la kiswahili). Hii ndio njia bora ya kuweza kuwasilian na nafsi. Kadir unavyozidi kufanya meditation unzidi kupata uwezo mkubwa wa kufanya mambo hapa duniani.
Asilimia zote za watu waliofanikiwa au wanaofanikiwa hapa duniani wanafanya meditation.
Joshua 1:8
This Book of the Law shall not depart from your mouth, but you shall meditate on it day and night, so that you may be careful to do according to all that is written in it. For then you will make your way prosperous, and then you will have good success.
Genesis 24:63 And Isaac went out to meditate in the field toward evening. And he lifted up his eyes and saw, and behold, there were camels coming.
Psalms 119:97 Oh how I love your law! It is my meditation all the day.

Kwa hiyo meditation ndio njia nzuri ya kuweza kuwasilina na nafsi zetu.
Unajua sisi tunauwezo wa uungu ndani yetu? Unajua tunauwezo wakufanya mambo makubwa na dunia yetu ikawa sehemu nzuri ya kuishi? Sisi ni gods na tuna nguvu ya kuitwa gods na ni kweli sisi ni gods Zaburi 82:6 "
Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia."

Utafanya nini ukikaa katika nchi ya watu walio na uwezo na unaona kabisa wanauwezo lakini wanalia shida? Je utawaacha tu hivyo au utawafundisha namna gani walivyo na uwezo? Ni mawili hapo. Ukiwafundisha watajitambua na utakosa watumwa kwa sababu unafurahia wao kuwa watumwa wako. Utawajaza vitu vingi vya ajabu na kuwafanya wakutegemeewewe. Jambo la pili utawafundisha ili waweze kujitambua na kuleta amani katika jamii hiyo kwa kuwa hakutakuwa na tofauti maana watu wanajitambua na wanaelewa wao ni nani.

Je hili jambo la pili linafanyika sasa. La hasha hawataki kabisa wanatufundisha makanisani kuhusu utoaji wa sadaka na kuwa waadilifu ilituweze kwenda mbiguni. Jambo ambalo ni tofauti lkabisa na inavyotakiwa.

Ninayo mengi sana ya kuweza kuongea nanyi rafiki zangu. Lakini hebu niweke kalamu yangu chini na niwaache nanyie muweze kuusoma waraka huu na kuniuliza maswali. Na mimi nitakuwa tayari kujibu inaweza kuwa siyo yote nitajimbu maswali yaliyo ya msingi.

By Annael
EDUCATION IS POWER

Nimesoma vyema post from ⬆ to ⬇ but ningependa kukuuliza swali as follows " je nitamtambuaje kuwa huyu ni mtumishi wa MUNGU na huyu sio...? Koz kama sikosea YESU alisema watumishi wake ni kama miti mema na matunda yao ni mema Lakini wale watumishi waovu watumiao nguvu za Mwovu nao matunda yao pia yatakuwa mabaya.?
 
Samahani sana ndugu yangu hapa mimi ninaongelea Jinsi gani sisi tulivyo na nguvu na tunauwezo mkubwa sana. Nimetumia biblia tu kwa ajili ya reference. Lakini kusema kweli mimi sio mkristo na hayo mambo ya kuhusu mtumishi wa kweli au la nihisi ni kulingana na dini yako inasemaje. Mimi siyo mtu wa dini mimi ni mtu wa kuleta mwanga kwa watu. EDUCATION then KNOWLEDGE then WISDOM then POWER
 
Obrigado
 
Mkuu somo zuri sana but kitu kinanichanya kidogo!

Sired yako iliyopita kule Jamii intelligent, Short and clear ulisema hizi dini (Islam and christian) ni OLD WORLD ODER = OWO. ulizizodoa na kusema zinapotosha, hazimueki mtu huru kiasi cha kuweza kufikiria kwa kina. LEO VIPI????
Hapa ndugu yangu sijabadili msimamo wangu upo pale pale. Nimetumia hiyo biblia kama reference ya kufikisha ujumbe kwa wenzetu watu wa dini. Ukiisoma vizuri nimeweka wazi kabisa. Na unajua chanzo cha maasi yote haya asilimia kubwa inasababishwa na hii dini ya kikristo.
 
Hahahahahaaaaaaa! :tape:

So unataka kusema wakiristo ni tatizo ila biblia iko sahihi?

Na ikiwa biblia ndio chanzo cha hayo matatizo kwanini unaitumia kama reference kusapoti madai yako????

Ivi unaichukuliaje biblia?
 
Biblia ni kama vitabu vingine vya hadith za kale. Unajua ukitaka kuishi na kupata watu kutoka kwenye jamii fulani fanana nao kwa kitambo. Hatimaye waeleze ukweli kuwa hakuna kitu kinachoitwa mungu duniani, mungu kaumbwa na watu na sio kuwa mungu kawaumba watu. Kwa sababu watu hao wamefungwa na vifungo vya imani. Ni vyema kuwapa elimu kidogo kidogo mwisho wa siku somo litaeleweka na kuiweka dunia kuwa mahali salama kwa watu wote. Hii ndio ninayo isema NWO lazima elimu ipite kwanza na ndipo tutakapofikia kipindi cha kuweka silaha chini na kuwa kitu kimoja. Laki ni sharti mambo ya dini yafe kabisaaaaa.
 
Ok. i like the way you explain.

Short and clear unajua roho ni nini, unajua connection ya mwili na roho and you know how to use it. Isnt it????

If yes, nimgeomba tu mtazamo wako juu ya hatma ya roho baada ya mwili kufa. as it believed roho hazifi.
 
Roho consciousness kama ulivyosema hazifi na sio as it believed ni kweli kabisa.

Tumekuja hapa duniani kutokea kwenye evolution nyingine kwaajili yakuja kupata different experience. Tukaingia na kuchukua mwili. Na baada ya hapo tutaenda kwenye evolution tofauti. Either in other planet or different milky way.
 
Hahahahaaaa! Aisee nnamengi ya kuuliza hapo, ila post yako hii_
Ngoja nitaanzisha thread inayohusu kabla ya kuzaliwa tulikuwa wapi na baada ya kufa tunaenda wapi.

Imenikata makali!

Ok. usiache kunitag kwa hiyo thread.
 
Hapa ndugu yangu sijabadili msimamo wangu upo pale pale. Nimetumia hiyo biblia kama reference ya kufikisha ujumbe kwa wenzetu watu wa dini. Ukiisoma vizuri nimeweka wazi kabisa. Na unajua chanzo cha maasi yote haya asilimia kubwa inasababishwa na hii dini ya kikristo.

Nilianza kukubaliana nawe ila kwa hoja kuwa ukristo ndio chanzo cha maasi hapo tushapoteana mkuu.
 
Back
Top Bottom