Jinsi ya kufika Msumbiji (Maputo) kwa bus

Jinsi ya kufika Msumbiji (Maputo) kwa bus

A
Aliyekudanganya nani mkuu? Hivi mimi ninayepita kila siku kwenda na kuludi na wewe nani mkweli?
Ukisikia Alshababi walikuwepo Cabodelgado na pemba, siyo Mozambique nzima, Askari wa Tanzania walikuja mwaka jana kulinda mipaka kwa ajili ya usalama tu, na hakujawahi kutokea tukio lolote la utekaji kwa hiyo njia linalohusiana na Alshababi,
Ahsante mkuu kwa clarifications
 
Mkuu achana na hiyo njia ya songea
Kuna mapori makubwaaa sanaa
Waasi huteka magari huko
Kaambiwa 58,000 anajua atafika Maputo hiyo route imepoteza sana vijana aisee nashangaa mpaka leo watu wanaendelea kutangaziana hiyo route wengi walipita wakiitafuta SA wanaenda kutokea Manguzi huko SA na wangine wamepoteza maisha...
 
Mkuu hii ni mihemuko au?Hebu pitia pitia basi kabla hujaropoka. I know what I am doing with evidence.
Tueleze unachojuwa, ni lini US viza inatolewa nje ya nchi yako without special case au kuwa na residence permit kwa nchi unayoombea?
 
Aliyekudanganya nani mkuu? Hivi mimi ninayepita kila siku kwenda na kuludi na wewe nani mkweli?
Ukisikia Alshababi walikuwepo Cabodelgado na pemba, siyo Mozambique nzima, Askari wa Tanzania walikuja mwaka jana kulinda mipaka kwa ajili ya usalama tu, na hakujawahi kutokea tukio lolote la utekaji kwa hiyo njia linalohusiana na Alshababi,
Cabo delgado sio pemba?
 
Tueleze unachojuwa, ni lini US viza inatolewa nje ya nchi yako without special case au kuwa na residence permit kwa nchi unayoombea?
Mkuu hebu kasome kwenye website kwanza upate maarifa. Mimi nina kundi la watu ambao wanachukua visa nje ya nchi mara kwa mara. US consulates ni universal. Nenda kasome kwenye website wamelielezea vizuri hilo upate maarifa
 
panda basi mpaka Songea,za super feo au Newforce nauli ni 58,000 zinaingia usiku, utalala kesho yake panda gari zinazoenda border au Congress kwa jina jingine border nauli 10,000 Zinaondoka saa 4 asubuhi,pale utakutana na border ya Tanzania na Mozambique, utaingia saa 8 mchana
Kutoka border mpaka Mji mmoja unaitwa Lichinga nauli 1500 mts sawa na Tshilings 58,000 utaingia kuanzia saa 3 usiku, kesho yake alfajili utapanda gari la kwenda Maputo ni siku 2 na nusu au siku 3 nauli, 4,800 sawa na Tshilings 152,000

Faida ya hii njia ni kalibu, gharama nafuu halafu unavuka inchi moja kwenda nyingine na hutasumbuka lugha kivile maana utatumia kiswahili tu mpaka unaingia maputo

This is the best route.
Nimeitumia sana njia hiyo kwa safari za Pikipiki kutoka Songea mwendo saa 8 tushaingia mgodini.
 
Hakuna usalama huko unadhani kwa nini watu wanapenda kuzunguka mkuu...Usalama kwanza ndio mambo muhinu kwenye safari huko kipande kikubwa ni pori na bara bara ya Vumbi..ukiachilia mbali hao Islamic wapo wanaoteka magari huko...

Siyo kweli, hiyo njia ni salama na watu wanaitumia kila siku, iwe magari ama bodaboda. Suala la mapori nchi hii hakuna mahali utakwenda bila kukuta mapori njiani wakati ukiunganisha mkoa na mkoa
 
Hio njia ni fupi sana. Ila sijawahi kupita. Watu wengi hawaijui hii njia ndio maana wanatumia Ile ya lilongwe hadi tete kisha Maputo,huo ni mwendo wa siku kama 4.
Ila hii ya songea lichinga ni fupi ingawa toka songea hadi boda ya msumbiji ( kilometa 120) barabara bado hawajamaliza kupiga lami.Lakini kuna mtu aliniambia upande wa msumbiji ni lami
Na huku upande wa lichinga hauna Wale Islamic state,hivo ni salama kwa kiwango kizuri

Kutoka Songea mpaka border ni kilomita 120 kutoka border mpaka lichinga ni kilomita 270 na kilomita 100 ndiyo lami kipande kinachobaki ni vumbi,ingawa kipindi cha kiangazi barabara zinakuwa nzuri tofauti na masika
 
Sio kweli mwezi wa 12 nilikwenda msumbuji tena nilikwenda jimbo lile la vita cabo Delgado, mimi ni muislam na nimeenda vizuri nimepita boda ya mtambaswala hadi nampula. Unaenda vzr tu ili mradi uwe na nyaraka za halali. Huko utazunguka sana nenda hadi mtambaswala nenda hadi Mueda pale utapata gari za pemba, pemba unapata gari za Maputo safari haitizidi siku 3 hadi unafika maputo
Sijaelewa unapinga nini na umeandika nini??
 
Siyo kweli, hiyo njia ni salama na watu wanaitumia kila siku, iwe magari ama bodaboda. Suala la mapori nchi hii hakuna mahali utakwenda bila kukuta mapori njiani wakati ukiunganisha mkoa na mkoa
Msumbiji sio salama mkuu kwenye mapori yao hilo halina ubishi...sijazungumzia Tanzania nazungumzia huko kwa hao Wabangu bangu...
 
Msumbiji sio salama mkuu kwenye mapori yao hilo halina ubishi...sijazungumzia Tanzania nazungumzia huko kwa hao Wabangu bangu...
Hata kama ni Salama, ukiona route haina border to border buses ujuwe kuna walakini, hakuna sehemu yenye fursa wafanyabiashara wa transportation wasifanye research.
 
Hata kama ni Salama, ukiona route haina border to border buses ujuwe kuna walakini, hakuna sehemu yenye fursa wafanyabiashara wa transportation wasifanye research.

Mabasi yapo, shida ni lami. Ndomana wengi wa wafanyabiashara na wachimba madini wanatumia pikipiki kwenda huko. Nauli kwa pikipiki kwa miaka kadhaa nyuma ilikuwa 100,000 tsh kwa kichwa. Dereva anakula mshkaki toka Songea mjini, ni mwendo wa saa 8, mwendo wa safari siyo kukata vitunguu
 
Hujaelewa nilichoandika.
 
Back
Top Bottom