Jinsi ya kufuta na kuondoa Michirizi (Stretch Mark) kwenye ngozi

Jinsi ya kufuta na kuondoa Michirizi (Stretch Mark) kwenye ngozi

wapenzi wadau,naombeni mnijulishe ni dawa gani nzr inayotoa 'strech mark' alama za tumboni zinazobaki baada ya kujifungua! Jamani zinakera mno! Kuna watu wanasema et huwa zinatoka zenyewe naturally! Sasa kama ni kweli,zinachukua muda gani bada ya uzazi! Coz for me,its almost a month and some days since nimejifungua,and the marks,are still there! Help...
 
sasa hivi umeshakuwa mtu mzima huwezi kuwa na feature za usichna jiandae na mabadiliko zaidi ya utu uzima mama mikunjo ya usoni na mvi etc
 
sasa hivi umeshakuwa mtu mzima huwezi kuwa na feature za usichna jiandae na mabadiliko zaidi ya utu uzima mama mikunjo ya usoni na mvi etc

hii imenifanya nicheke,,,lolz! Hata hivyo nadhani kuna dawa za kuondoa ngoja tusubiri wataalam:nono:
 
ni ngumu kutoka,ila nasikia unaweza kuimprove isionekane saana kwa kupaka cocoa butter au bio oil:A S 2152:
 
my wife wangu ana watoto sita sasa , hana..imejiishia yenyewe, vuta subira binti, mwezi mmoja tu hautoshi.
 
Pakaa Hollywood cocoa butter creme, au Palmers cocoa butter, au Bio Oil. Ila huwa haziondoki, zinafifia tu.
 
wala haina haja ya hayo mabio oil ila kama unaweza kumudu sawa maana hayatoki kesho wala kewshokutwa utapaka mpaka uchoke,vasselin ni nzuri zaidi utapaka na yananafifia taratibu kama ambavyo yanafiifia ukipaka Bio Oil na mazagazaga mengine...
 
Watu wa pwani baada uzazi hujichuwa kwa mafuta ya nazi, hujisiriba liwa na manjano mara kwa mara. Nadhani hayo husaidia.

Aunt yenu alikuwa akifanya hivyo wakati huuuo tungali vijana na mpaka leo anaendelza liwa na manjano na MashaAllah ukimuona hujuwi kama amejukuu.
 
Wana JF, Mke wangu nasumbuliwa na Kupasuka ngozi (stretch marks), amepasuka mapaja yote na sehemu kubwa ya mikono, tumbo na kiuno. Baadhi ya dawa alizoltumia bila mafanikio ni pamoja na PURE TISSUE OIL (Johnson’s healthy skin) na Stretch Nil, zote zimedunda. Tunaomba msaada wenu tafadhali. Asanteni
 
Pole sn mkuu!! Hivi hilo tatizo halisababishwi na unene? Waone specialist (wa idara za dermatology) hao ulio taja labda sio specialist wa ngozi
 
duu kwani unawasha au unataka kuonesha tumbo na kiuno chako maana kama hauwashwi ni bora uzipotezee tu hizo michirizi..
 
.....kuna cream inaitwa mederma stretch marks therapy mie imenisaidia sana, nilipata stretch marks kipindi cha ujauzito ila sasa hivi kwa kutumia hii cream zote zimeondoka. Ila sasa inabidi upake muda mrefu, mie imechukua miezi 6 stretch zote kutoka.
 
Yaani nyie mnahangaika na cream za kuondoa hiyo mipasuko badala ya kumpeleka mke gym akapunguze unene? You are kidding guys. Hakuna cream inaweza kuwa effective katika hilo, zaidi kutafuta shamba kila jumamosi akashike jembe au kwenda Gym.
 
.....kuna cream inaitwa mederma stretch marks therapy mie imenisaidia sana, nilipata stretch marks kipindi cha ujauzito ila sasa hivi kwa kutumia hii cream zote zimeondoka. Ila sasa inabidi upake muda mrefu, mie imechukua miezi 6 stretch zote kutoka.

Asante, Hatuna ujauzito na hatujajifungua ila stretch marks zimetoka sana. Tulisha tumia lotion moja ambayo ni "Herbal lotion for prevention of Prignancy stretch marks'' nayo haikutusaidia.
 
mkuu, kwanza nikupongeze kwa kumjal mkeo na kuona tatizo hili ni lenu wote.kuna mafuta yanaitwa bio-oil, yanakuwa na box nyeupe ina maandishi ya orange. ni nzuri pia kwa kulainisha ngozi na kuondoa stretch marks. lakini kama anavyosema pretty, usitegemee matokeo ya haraka sana. pia google cellulites uone kama utapata info za kuwasaidia. kila la kheri
 
Back
Top Bottom