MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Maelezo meengi yaani nimesoma mpaka baadaye nimeanza kuona kama sauti ya Nanauka ikiimba....26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.
Hoja yako kuhusu kutumia pesa za wengine (leverage) huku zako binafsi zikiendelea kuzaa faida kwenye compound interest ni mbinu ya kifedha inayotambulika, na kwa mtu mwenye maarifa ya juu ya fedha, inaweza kuwa na manufaa.
Hata hivyo, changamoto ni hii: mbinu hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uelewa wa hatari za kifedha, na uwezo wa kurejesha mkopo kwa wakati hata kama mambo hayaendi vizuri. Ni wachache sana wanaoweza kuitumia mbinu hiyo kwa mafanikio.
Wengi wanaokopa, katika nchi zinazoendelea, hawakopi kwa ajili ya uwekezaji, bali kwa matumizi ya kila siku kama chakula, kodi, mavazi, au sherehe. Kwa hiyo, hawazalishi chochote kutoka kwenye mkopo.
Katika mazingira kama hayo, hata kama mtu ana pesa zake benki zinazopata compound interest, bado hatakuwa na faida ya kweli kwa sababu anaingiza faida ndogo sana benki (labda 10% kwa mwaka), lakini anatumia mkopo wa riba kubwa (labda 15% au zaidi), halafu fedha hiyo inakwenda kwenye matumizi yasiyo na marejesho.
Matokeo yake ni kwamba faida ndogo inayopatikana kwenye compound interest inafutwa kabisa na mzigo wa mkopo wa matumizi. Mwisho wa siku, mtu huyo atazama kwenye madeni ingawa anaonekana ana akili ya kifedha.
Kwa hiyo, siwashauri watu wa kawaida waanze na mkakati wa “leverage” kabla hawajajenga msingi wa nidhamu ya matumizi, akiba, na uelewa wa mikopo yenye tija. Ni bora kuwa huru kifedha kuliko kuishi kwa kutegemea mikopo kila siku.
Hekima ya Mithali 22:7 bado inabaki kuwa ya kweli: "Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye."
Na bado sote tunahitaji Mungu atutimizie ahadi yake kwamba tukifuata kanuni zake, atatufikisha kwenye level ambayo: “Tutawakopesha mataifa, wala hatutakopa.” (Kumb. 28:12)
cc: DeepPond Soulja boy Mvinyo mpya
26 Life kwanza nikusahihishe, ningekuwa na hali ngumu ya maisha nisingeshinda hapa naandika mada za kuwasaidia wengine.

Nilikaa mwaka mzima bila kununua nguo zilizopo zimechakaa sana. Je niigata pesa sinunue kwa kuwa nguo ni anasa?Panga bajeti ya mapato na matumizi.
– Bajeti inakusaidia kujua unachopata na kutumia bila kupitiliza.
Tumia pesa kwa vipaumbele, si kwa mazoea au tamaa.
– Tofautisha kati ya mahitaji ya lazima na anasa au starehe.
Epuka maisha ya kushindana na watu wengine.
– Kuiga maisha ya wengine hupelekea matumizi ya kupita uwezo wako. Ukiona jirani yako amenunua Rolls-Royce Spectre, usikope pesa ili ununue Bugatti Tourbillon.
Jifunze kusema “hapana” kwa matumizi yasiyo ya lazima.
– Nidhamu ya kusema hapana ni silaha muhimu dhidi ya madeni.
Tenga akiba kila mwezi, hata kama ni kidogo.
– Akiba ni kinga dhidi ya dharura zinazoweza kukulazimisha kukopa.
Ridhika na kile Mungu alichokupa kwa sasa.
– Kuridhika huzalisha amani ya moyo na huzuia tamaa ya kupita kiasi.
Fanya kazi kwa bidii na ubunifu. Usiridhike na chanzo kimoja cha pesa. Panua wigo.
– Mapato yako yataongezeka ukiongeza bidii ya kazi na vyanzo vingine vya mapato halali.
Usitumie mikopo kuendeshea maisha ya kila siku.
– Mikopo inafaa zaidi kwa ajili ya uwekezaji. Usikope kwa ajili ya kununua chakula au mavazi.
Epuka mikopo ya haraka, yenye riba kubwa.
– Mikopo hiyo inaumiza zaidi kuliko kusaidia; inawaingiza watu wengi kwenye mateso.
Mshirikishe Mungu katika mipango yako ya kifedha.
– Mungu huwapa hekima wale wanaomtumaini, hata katika masuala ya pesa.
Asante kwa kongole. Nakuombea, Mungu akufunulie, utambue kuwa hata zile mada zangu unazozitwanga spana zina elimu nzuri ya kukusaidia kupata faida ya milele kuliko hizo compound interestsUmetoa elimu nzuri Sana dada, japo Huwa nakupiga Spana, Ila hapa nakuona kongole😊👍
Mabilionea na mataifa makubwa hukopa kwa madhumuni ya kuwekeza au kukuza biashara zao. Na wanapokopa wanahakikisha kwamba mikopo hiyo inaleta faida na si mzigo.Taifa linakopa, bilionea wanakopa, mimi ni nani hata nisikope?
Biashara inakata moto muda wowoteLeo nipo pamoja naww mama mchungaji wabongo wengi ni vilaza wanakopa kununua gari na kujenga nyumba sio biashara hvo Bora wasikope kabsa
Matumizi ya kawaida ni yapi?Mabilionea na mataifa makubwa hukopa kwa madhumuni ya kuwekeza au kukuza biashara zao. Na wanapokopa wanahakikisha kwamba mikopo hiyo inaleta faida na si mzigo.
Wengi wetu tunakopa kwa matumizi ya kawaida au anasa bila mpango wa marejesho, na hapo ndipo tunapoingia kwenye hatari ya kuishi kama watumwa wa mikopo sawasawa na andiko hilo "akopaye ni mtumwa wa akopeshaye" (Methali 22:7).
Mimi hapa nahamasisha kuishi bila kutegemea mikopo. Sijasema kwamba usikope kabisa. Ni bora kujifunza namna ya kutumia fedha kwa busara, na kuendelea kujenga uhuru wa kifedha kwa kuzingatia hekima ya Biblia.
Kwàakili hizi mtakua maskini vizaz na vizazBiashara inakata moto muda wowote
Heri wanaokopa ili kujenga na maisha mengine yaendelee
whatever the case huwezi kuishi bila kukopa hasa kwa nchi zetu masikini hizo , anakopa hadi trump hizo namna ulizosema ni ma theory tu hamna kitu.Soma tena vizuri mada. Sijasema kukopa ni dhambi