Jinsi ya kuishi kwa furaha na mkeo/mumeo Siku zote za maisha yenu.

Jinsi ya kuishi kwa furaha na mkeo/mumeo Siku zote za maisha yenu.

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
JINSI YA KUISHI KWA FURAHA NA MKEO/MMEO SIKU ZOTE ZA MAISHA YENU.

Anaandika, Robert Heriel Mtibeli.
Baba/Mume.

1. Nitaendelea kutoa elimu. Sipo hapa kumbadilisha mtu anayeishi maisha anayoyahitaji.

2. Nipo hapa kwa ajili ya wenye uhitaji wa kuishi maisha ya furaha, kuishi kwa amani wao na familia zao. Hii ndio sababu ya mtibeli niko hapa.
So wale wanaofikiri nipo kuwabadilisha hiyo kazi watibeli hatufanyagi. Huo muda hatuna. Tunaheshimu mipaka yetu, tunaheshimu mipaka ya wengine.

3. Kwa Watibeli kumbadilisha mtu anayeona anaishi maisha anayoyahitaji ni mwiko. Ni dhulma. Ni kuingilia mipaka ya Watu wengine. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

4. Ili maisha yakamilike yanahitaji Familia. Binadamu bila familia(watu wake) anaishi maisha ya mateso, upweke, huzuni, kutanga tanga.
Maisha yanahitaji watu. Na watu wako wakwanza ni familia.

5. Familia ni Baba(mume), Mama(Mke), na Watoto. Kisha wazazi wa mume na wazazi wa Mke, hawa wote wanaunganishwa na kuwa jamaa wenyw undugu.

6. Kwa maana hiyo undugu na ujamaa haununuliwi. Undugu unajengwa na Upendo. Ndio maana Watibeli hawaoi wala kuolewa kwa Mahari. Kwa maana ya kupangiwa kiasi au kumpangia kiasi kijana anapotaka kumposa binti.

7. Kijana atakuwa na hiyari ya kutoa zawadi kama anayo. Kama anavyoenda kuwapelekea wazazi wake zawadi.
Kwa Sisi Watibeli, Wakwe ni wazazi.
Na Mzazi hawezi kumdai mtoto wake wala mtoto hawezi kumdai Mzazi wake.
Isipokuwa wanapeana kwa mapenzi, upendo.

8. Hii ni kusema Watibeli msingi mkuu wa Familia ni UPENDO na upendo haunaga bei. Huwezi kuununua. Upendo utahusu moyo. Naam moyo wenye mapenzi ya kweli na utu wa kiwango cha juu.

9. Binti na kijana wangu, Kama nilivyokwisha kukuusia na kukuandika nyaraka za mwanzoni!

10. Unapochagua mke/mume lazima utumie akili kuliko hisia. Hilo ni Jambo la Kwanza.
Upendo ni uchaguzi (love is a choice) na kamwe upendo sio Hisia kwetu Sisi Watibeli.

11. Tunaamua tumpende nani na sio kuendeshwa na moyo.
Tumeutiisha moyo na moyo unafuata kile tunachokihitaji.

12. Hii ni kumaanisha ndio maana tunaweka vigezo na masharti Kwa wale tunaohitaji kuwaoa/kuolewa nao. Kwa kuzingatia zile kanuni za mahusiano.
Ikiwemo MFANANO.

13. Hivyo kabla hujaingia kwenye ndoa lazima uhakikishe unayemuoa/anayekuoa anasifa za msingi ikiwemo Mfanano.
Je mnafanana, kimtazamo, kihisia, kimalengo, kiuchumi, kimaumbile, n.k.

14. Kisha mkishaingia kwenye ndoa mambo yanakuwa bafanabafana.

15. Zifuatazo ni njia za kuishi kwa Amani na furaha wewe na mkeo/mumeo;

a) Maslahi ya familia yawekwe Mbele.
Kila mtu awaze hatma na malengo ya familia yenu zaidi.
Awaze watoto, awaze kuandaa furaha yenu ya wakati huu na wakati ujao.
Awaze kupambana na kutokomeza/kutiisha maadui ya familia yenu ikiwemo adui Ujinga, umaskini, maradhi, fitna za walionje, tamaa za mwili, kiburi n.k.

Mnapokwaruzana mkikaa mjadili zaidi jinsi ugomvi wenu unavyowaletea athari kufikia malengo.
Hii ni kumaanisha Familia lazima iwe na Malengo na Dira na sio dira isiyojadiliwa. Lazima mkae mzungumze na mpange Dira na Malengo ya familia yenu.
Kwamba kwa nini mpo Pamoja?

b) Mtengeneze Mwenza wako.
Hii itahitaji uwazi wa kweli usio na shutma.
Kama unataka mkeo awe mrembo, tako Fulani hivi, au kiuno Fulani au avae vitu Fulani hivi. Mtengeneze.
Sisi watibeli tunatengeneza Wenza wetu, tunamodify ila hatubadilishi.

Mumeo kama unataka avae Kiana flani, au awe na six pack au awe na kakitambi Noma kama kangu unamtengeneza.

c) Mawasiliano na Uhuru.
Ni sharti Mfikie level ya kitibeli, kwamba mkeo/mumeo akiwa na Jambo lolote, narudia lolote awe na uwezo wa kukuambia bila kukuficha.
Kama unapiga show mbovu akuambie na mtafute ufumbuzi. Usione aibu ukiwa na mkeo/mumeo. Yaani mtu mvuane nguo, mpaka mmezaa alafu unaona shida kuzungumza ukweli?

Kama mwanamke unawasiwasi Fulani kuhusu uzuri wako au mabadiliko yako hasa baada ya kujifungua. Usikae kuwaza ujingaujinga. Mfano, wanawake wengi hufikiri wakitoka kujifungua Maungo yao ya siri(uke) unatanuka na kuwa mkubwa au kulegea. Hali inayowanyima kujiamini na kuhisi mwanaume aliyenaye hafurahii. Na hii inaleta migogoro mingi ndani ya ndoa.

Ukweli ni huu, Utamu na uzuri wa mwanamke Hasa mke ni matokeo ya mahusiano mazuri na mtazamo wa mwanaume.
Sisi watibeli hatuoni shida kuzungumzia mambo hayo kwani ni mambo madogo na rahisi Sana.
Mkeo akiwa na hofu mtoe hofu ili naye afurahie. Asitumie nguvu kubwa kukuridhisha wewe huku yeye akibaki kama mtumwa. Furahishaneni.
Mtoe hofu.

Inaweza kuwa ni kweli Uke umetanuka kidogo au kulegea lakini mwambie ni mtamu, mzuri, unajoto, na zaidi mwambie utarudi kama zamani tukifanya mazoezi. Na mfanye mazoezi kweli.
Utashangaa mambo yanabadilika na mwanamke wako anakufurahia.

Mwanamke anafika mshindo kwa kuwa huru mbele yako, Uhuru unaleta Uhuru wa kihisia. Hatumii nguvu nyingi. Dakika tano anauwezo wa kupiga goli mbili.

d). Uwazi na uaminifu.
Sisi Watibeli tunapewa pesa na Wake Zetu.
Akaunti zetu zinamilikiwa na Wake Zetu.
Password ya bank, simu zetu wanazo wake zetu.
Wanawake hawatuombi hela kwa sababu wao ndio tumewapa umiliki wa pesa.
Hii inatutatulia matatizo mengi ndani ya familia zetu.
Iko hivi, mwanamke usipompa akaunti ya pesa yeye anajua muda wote unahela na unatoa pesa nje. Hata kama hautoi. Lawama, masononeko, gubu, na kuhisi hapendwi kunakuwa kwingi.

Sisi kama Watibeli tunampa Mwanamke benki akae naye. Kumkabidhi fisi bucha. Nyumba inatulia tuli. Anaparangana mwenyewe.

Ukiwa na shida ya pesa anakupa. Nataka niende Jioni Bar na washikaji, anaingia ndani anakupa elfu hamsini😄.

Kingine wanawake wanauchungu na pesa zikishakuwa zao. Zikiwa kwako hawana uchungu nazo.
So sisi Watibeli tunapowapa wanawake pesa ziwe zao automatic matumizi ya mwanamke yataenda down. Ile pesa ataiona ni ndogo.
Milioni moja ni nyingi ikiwa mikononi mwa mume. Hivyo kukuomba elfu 50 au laki ya kusuka mkeo au mwanamke haoni shida.

Ila ukimwambia milioni hiyo chukua wewe ndiye mmiliki na ndiye mambo ya bajeti humu ndani utayaendesha wewe. Nakuhakikishia Hana uwezo wa kutoa 50k akasuka. Atatumia chini ya 30k na atakaa na msuko huo hata miezi miwili.

Unapompa mwanamke Jiko, benki ajiamilie usisahau kuwa na exist door ya akiba na emergency ambazo hazitatumika. Hii mkeo asijue.

Na mkeo hatakuwa na shida na akaunti hiyo kwani anajua wewe ni mwanaume

e) Siku zote kuwa Upande wa mkeo/mumeo mkiwa nje
Awe amepatia au amekosea. Haijalishi lazima ulinde maslahi ya Familia yenu kivyovyote kwa yeyote.

Lazima umtetee mwenza wako. Usimkosoe mbele za watu. Ikiwezekana beba lawama kwaajili yake. Naye anaowajibu WA kubeba lawama kwaajili uako.
Sisi Watibeli ni Watu wa Haki lakini kwenye Familia zetu mke/mume wa kitibeli anahaki zaidi.

Huwezi kuwa na haki sawa mbele ya mke wangu. Na watoto wangu hilo futa kwenye akili yako na usilitegemee.
Watibeli tulifanya tafiti na chunguzi zetu tukabaini binadamu hawanaga Wema.

Na kamwe usimuweke mkeo/mumeo katik mzani mmoja na mtu back. Mkeo/mumeo ni mimeo/mkeo haijalishi nini. Lazima apewe upendeleo.

Kuna atasema ooh! TaikonMaster Una double standards, ooh! Unakigeugeu. My friend nakufundisha elimu ya kweli.
Elimu ya darasa la Kwanza sio elimu ya kidato cha tano.
Darasa la kwanza ulifundishwa 1 - 2 haiwezekani lakini uliponda level ya elimu ulijua inawezekana. Sio kwamba hesabu ni kigeugeu. Bali ni level ya ufahamu

Ulipokuwa Mdogo uliambiwa maji hayapandi mlima. Lakini ufahamu, akilo na teknolojia ikikua unagundua maji yanapanda mlima. So ni level ya maarifa.

Haya ni mambo ya kifamilia.
Kwenye level ya kitaifa. Mtanzania mwenzako ni Bora kuliko mtu WA taifa jingine. Lazima umtangulize yeye.

Huwaga nashangaa Sana watu wanapoponda Wake/waume zao tena mbele za watu wasiohusika. Ni dalili ya mtu asiyejiheshimu, asiyejitambua, aliyeamua kujivua nguo.

Watibeli hatugombani na asili. Sisi tunaangalia uhalisia.

f) Mwenye Akili ndio awe Kichwa cha Nyumba.
Mwanamke ni kichwa cha nyumba kwenye mambo ya kike, ukike.
Mwanaume ni kichwa cha nyumba kwenye mambo ua kiume/uume.
Wote ni viongozi. Wote ni mhimili.

Ingawaje Mwanaume ndiye kichwa cha nyumba mbele za umma.
Kwamba kwenye Familia ya kitibeli, mathalani familia ya TaikonMaster, Robert Mbele za umma ndiye Rais, kichwa cha familia Yake, yeye ndiye atatoa oda, maelezo, habari, yeye ndiye mzungumzaji mbele za umma. Mke yaani Binti Kimoso hatotakiwa kuonekana akizungumza zungumza mambo ya kifamilia, taasisi za familia, sijui makampuni ya familia au matukio ya kifamilia. Yeye atakuwa kimya tuu Siku zote isipokuwa mumewe akiwa hajiwezi au hayupo.

Mwanamke ndani ya nyumba atakuwa kama Waziri Mkuu, mtendani mkuu wa shughuli za nyumba. Mipaka yake ni ndani ya nyumba, kuhakikisha oda zote za mumewe zinatekelezwa na kuwaweka watoto sawa.
Mwanamke anayohaki ya kuamua mgeni gani awepo ndani na nani asiwepo. Na Sisi Watibeli tukamsikiliza lakini lazima atoe Hoja zenye mashiko.
Hawezi kujiamulia tuu bila hoja.

Mwanaume wa kitibeli nazungumzia mimi nikiwepo ndiye ninaweza kutoa oda Nani awepo na Nani asiwepo bila kuzuiwa wala kuulizwa. Ingawaje Mke anayohaki y kujua sababu ya mimi kufanya hivyo. Ninaweza kumpa sababu au nisimpe.
Lakini yote kwa yote mke anaowajibu wa kutii kwani itafanyika kwa maslahi ya familia.

Mwanamke kuwa kichwa au kiongozi ndani ya nyumba haimaanishi atakuwa Sawa na Baba/mumewe. Bali watibeli tunamaanisha. Kwamba yapo maeneo wanawake wanawazidi wanaume kiuwezo na kimaamuzi . Maeneo hayo, vipaji hivyo mwanamke atakiwa kichwa.

Mfano, Sio Kila mwanaume anauwezo wa kuwa na roho ngumu kumnyima mtu msaada. Wanaume wengi Kila akiombwa pesa na mtu yeyote hata kama sio shida kubwa mwanaume anatoa. Familia yake inashida, hawali vizuri, bado watoto wanamahitaji ya shule lakini mwanaume hawezi kusema hapana, wakati huo mkewe anauwezo wa kukataa.
Basi ni vyema mwanamke awe kiongozi WA mambo ya mapato na matumizi.
Kwa watibeli sio tatizo.

Wanawake wengi ni wazuri wakuangalia na kujali maslahi ya watoto wao kuliko wanaume.
Kwa vile wanawake ni watu wakijihami na kuogopa Siku mume ukiwa haupo itakuwaje, ni vizuri mwanamke akapewa uongozi WA mambo yajayo. Kukushinikiza, kukufuata fuata, kukuhamasisha, na kusimamia.
Kazi yako mwanaume itakuwa kuangalia usalama, ubora, na uthabiti wa wazo au mradi.

Kwa Leo nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndoa ni utapeli

Kutafuta furaha ndani ya Dunia ni sawa na kutafuta mwanamke bikra kwenye wodi ya wazazi sijui kama utampata.
 
Back
Top Bottom