Deinstein 01
JF-Expert Member
- May 12, 2024
- 2,090
- 3,928
Habari Wakuu!
Moja ya kitu kinachomfanya mtu aishi maisha yenye furaha ni kujua kusudi lake na kuliishi kusudi lake.
Bila shaka najua ya kuwa watu wengi hawajui kusudi lako lao la kuwepo hapa duniani. Kwakuwa mienendo ya watu wengi inakuchochewa na watu waliowazunguka. Mfano unakuta mtu tangu yupo mdogo wazazi wake wanamchochea awe daktari hata kama moyo wake haupo kwenye udaktari. Au unakuta mtu anashawishiwa na watu waliomzunguka asomee kitu fulani kwakuwa kina ajira ila unamkuta huyu mtu hajijui mwenyewe yaani hana SELF REALIZATION maisha yake yanaendeshwa na mitazamo ya watu wengine na si kwa mitazamo yake.
Sasa kwenye kujua kusudi lako la kuwepo duniani halihusiani na imani yako juu ya uwepo wa Mungu. Kwakuwa kuna walokole kibao hawajui kusudi lao ukiwauliza juu ya kusudi lao wao wanakwambia tu kusudi lao ni kumsifu na kumuabudu Mungu. Ila kuna Atheists kibao wana SELF REALIZATION na wanaishi kusudi lao kwa misimamo yao.
Ukitaka kujua kusudi lako fanya vitu vifuatavyo;
TENGA MUDA WA KUTAFAKARI JUU YA MAISHA YAKO. Kila siku tenga walau dakika 15 kila siku kutafakari juu ya mienendo yako tafuta mahali penye utulivu na usiwaze kitu chochote isipokuwa wewe mwenyewe. Hii itakusaidia kutambua DESIRES zako yaani vitu unavyotamani kuaccomplish na itakusaidia kupata SELF REALIZATION na SELF AWARENESS.
USIRUHUSU MITAZAMO NA MIENENDO YA WATU WENGINE IKUENDESHE.
Watu wengi hatupo huru kwakuwa tunatawaliwa na mitazamo na mienendo ya watu wengine. Kwakuwa umeambiwa hiki na wewe unakifuata au umeona mwenzako kafanya hivi na wewe unaiga bila ya kufikiri. Hii inasababisha uishi kusudi la watu wengine na si lako.
SIKILIZA MOYO WAKO.
Hata kwenye biblia Mathayo 6:21 inasema
Mathayo 6:21
[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Ujaribu kuuelewa mayo wako unataka nini yaani undesire nini hasa ukiachana na vitu vidogovidogo kama vile sex. Kwakuwa hapo ndo hazina yako ilipo.
Kwakumalizia, haimaanishi kuishi kusudi lako ni kuwa na majumba, magari au kuwa na pesa unaweza kuwa na hivyo vitu ila hauna furaha. Mtu kama Papa Francis hakuacha mali nyingi ila aliishi kusudi lake ,Mahtma Gandhi hakuacha hata nguo zinazoeleweka ila ndio mwanzilishi wa taifa la India. Anwar Sadeet aliyekuwa rais wa Misri aliyeipatanisha Misri na Israel aliuliwa na alikuwa mfungwa ila Misri haitakuja kumsahau.
Yangu ni hayo tu.