Jinsi ya kujua kusudi lako la kuishi duniani

Deinstein 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
2,090
Reaction score
3,928
Habari Wakuu!

Moja ya kitu kinachomfanya mtu aishi maisha yenye furaha ni kujua kusudi lake na  kuliishi kusudi lake.

Bila shaka najua ya kuwa watu wengi hawajui kusudi lako lao la kuwepo hapa duniani. Kwakuwa mienendo ya watu wengi inakuchochewa na watu waliowazunguka. Mfano unakuta mtu tangu yupo mdogo wazazi wake wanamchochea awe daktari hata kama moyo wake haupo kwenye udaktari. Au unakuta mtu anashawishiwa na watu waliomzunguka asomee kitu fulani kwakuwa kina ajira ila unamkuta huyu mtu hajijui mwenyewe yaani hana SELF REALIZATION maisha yake yanaendeshwa na mitazamo ya watu wengine na si kwa mitazamo yake.

Sasa kwenye kujua kusudi lako la kuwepo duniani halihusiani na imani yako juu ya uwepo wa Mungu. Kwakuwa kuna walokole kibao hawajui kusudi lao ukiwauliza juu ya kusudi lao wao wanakwambia tu kusudi lao ni kumsifu na kumuabudu Mungu. Ila kuna Atheists kibao wana SELF REALIZATION na wanaishi kusudi lao kwa misimamo yao.

Ukitaka kujua kusudi lako fanya vitu vifuatavyo;
TENGA MUDA WA KUTAFAKARI JUU YA MAISHA YAKO. Kila siku tenga walau dakika 15 kila siku kutafakari juu ya mienendo yako tafuta mahali penye utulivu na usiwaze kitu chochote isipokuwa wewe mwenyewe. Hii itakusaidia kutambua DESIRES zako yaani vitu unavyotamani kuaccomplish na itakusaidia kupata SELF REALIZATION na SELF AWARENESS.

USIRUHUSU MITAZAMO NA MIENENDO YA WATU WENGINE IKUENDESHE.

Watu wengi hatupo huru kwakuwa tunatawaliwa na mitazamo na mienendo ya watu wengine. Kwakuwa umeambiwa hiki na wewe unakifuata au umeona mwenzako kafanya hivi na wewe unaiga bila ya kufikiri. Hii inasababisha uishi kusudi la watu wengine na si lako.

SIKILIZA MOYO WAKO.

Hata kwenye biblia Mathayo 6:21 inasema
Mathayo 6:21
[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Ujaribu kuuelewa mayo wako unataka nini yaani undesire nini hasa ukiachana na vitu vidogovidogo kama vile sex. Kwakuwa hapo ndo hazina yako ilipo.

Kwakumalizia, haimaanishi kuishi kusudi lako ni kuwa na majumba, magari au kuwa na pesa unaweza kuwa na hivyo vitu ila hauna furaha. Mtu kama Papa Francis hakuacha mali nyingi ila aliishi kusudi lake ,Mahtma Gandhi hakuacha hata nguo zinazoeleweka ila ndio mwanzilishi wa taifa la India. Anwar Sadeet aliyekuwa rais wa Misri aliyeipatanisha Misri na Israel aliuliwa na alikuwa mfungwa ila Misri haitakuja kumsahau.

Yangu ni hayo tu.
 
Tumeumbwa ili tumjue Mungu, tumpende, tumtumikie na kisha tufike kwake mbinguni full stop! Mengine ni kujilisha upepo tu!😁😁😂😂
 
Nilipo maliza chuo mwaka 2018 pale UDOM CiVe nilibahatika kufika mtaani nikiwa na malengo makubwa sana ila baada ya kuteseka maabara nikaja gundua kuwa unaweza pata Pesa kwa kulidhisha watu ambao wapo na upweke unaotokana na kazi kuwa nyingi.

Njia hizo nilitumia kanuni za physics ambazo nilijaribu kutafuta uhusiano kati ya energy na speed nikaona kuwa ili uweze kumu win mshangzi lazima ufate hii kanuni
E =MC².
Maana yake nini Energy E ni direct proportionally kwa Mshangazi (M)
Ili upate mshangazi lazima uwe na Energy hvyo kula sana ..

Lakini hapo hapo energy haitoshi kumuweka shangazi costant yaan
M = E/C². Ili kumuweka Mshangazi costant ni lazima ucheze na speed .

Speed ni muhimu ujue ku balance speed maana hawa ni watu ambao hawataki kashi kashi saana .

Hivyo ili uweze ku dumu basi fanya hvyo zingatia energy na speed...

Mpaka sasa nimeandika vitabu viwili vipo kwa softcopy - Astrosexual Aerospace
-Biochemical Desire

Siuzi narudia tena siuzi hivi vitab
 
Endelea kuridhisha mishangazi. Ila ARV zitakuwa adimu.
 
Kabla ya kujua kusudi lako la kuwa duniani, na kama lipo, unatakiwa kujua maana ya kusudi.

Kusudi, kwa muktadha wa uzi huu, maana yake nini?
 
Kabla ya kujua kusudi lako la kuwa duniani, na kama lipo, unatakiwa kujua maana ya kusudi.

Kusudi, kwa muktadha wa uzi huu, maana yake nini?
Sawa mkuu.
Kusudi lako la kuwepo duniani ni sababu ya wewe kuwepo hapa duniani. Yaani ni jinsi utakavyoimpact jamii positively.
 
Sawa mkuu.
Kusudi lako la kuwepo duniani ni sababu ya wewe kuwepo hapa duniani. Yaani ni jinsi utakavyoimpact jamii positively.
Nimekuuliza kusudi maana yake nini, si kududi lako kuwepo duniani ni nini.

Narudia. Kusudi maana yake nini?

Ku impact jamii positively maana yake nini? Kwa mujibu wa nani? Kwa nini kusudi la mtu kuwepo duniani liwe ku impact jamii positively?

Mtu ambaye hana uwezo wa ku impact jamii positively inakuwaje sasa, yeye hana kusudi la kuwepo duniani?
 
Nimekuuliza kusudi maana yake nini, si kududi lako kuwepo duniani ni nini.
Kusudi ni nia au lengo alilonalo mtu.

Ku impact jamii positively maana yake nini? Kwa mujibu wa nani? Kwa nini kusudi la mtu kuwepo duniani liwe ku impact jamii positively?
Kuimpact jamii positively ni kutumia vipawa vyako na maarifa kuisaidia jamii. Sidhani kama kuna mtu anazaliwa ili aje kufanya mabaya kwenye jamii. Of course wapo wanaofanya mabaya ila mwisho wao huwa mbaya.

Mtu ambaye hana uwezo wa ku impact jamii positively inakuwaje sasa, yeye hana kusudi la kuwepo duniani?
Kila mtu anauwezo wa kuimpact jamii positively hata kama ni kilema.
 

Law nyingine hii itumie
Newton alisema "the greater the mass of an "object" the greater force of attraction" 😁😊😁
 
Hilo neno kusudi linachanganya na linaweza kuweka tafsiri kwamba kuna sababu ya watu kuwapo duniani tofauti na wanayojiwekea wenyewe wakishakuwepo duniani.
 
Ebo! Eti sex vitu vidogo unaumwa nini wewe??!!!
Wee pep kaishiwa mawazo kisa kukosa mbususu lakini amepewa mbususu tayari man city wanapiga watu mabao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…