Jinsi ya kukokotoa Ongezeko la Asilimia Mshahara!

Jinsi ya kukokotoa Ongezeko la Asilimia Mshahara!

Ukiondoa kima cha chini hiyo 23.3% wengine watalamba 2%, 4, 12, 7 , 8 etc ila hawatafika ongezeko la watu wa kima cha chini. Uko sahihi kabisa mkuu.
Usinilishe maneno! Sikumaanisha hivyo, mara zote kote duniani nyongeza ya mishahara huwa kinatajwa kiwango cha wale wanaopokea kima cha chini. Nashangaa kwanini sasa hivi watu wanatokwa povu as if ni kitu kipya.
 
Nimeona wengi wanauliza nikaona nianzishe uzi labda kusaidia, ni hivi chukua asilimia ya kilichoongezwa mf. 28% gawanya kwa 100 yaani 28:100 halafu zidisha na Mshahara wako, yaani 0.28*(mshahar wako kabla ya kodi)= halafu jibu lake jumlisha tena na Mshahara wako, jibu lake ndiyo kiwango ulichoongezwa.

Huo mshahara kabla ya Kodi ndio ukokotoe!
Hapa unazungumzia kima kipi? Cha chini, kati au juu?
 
Mbona kwenye tanagazo hawajasema kwa kima cha chini, ila wameandika ikiwemo kima cha chini.
Hapo sasa, Rais kasema ongezeko kwa wote ikiwemo kima cha chini. Ila watu wanakazania ooh kima cha chini tu... Yani sijui ni wivu [emoji1][emoji1] mtu anaona haimuhusu hii so anaona akatishe wenzie tamaa.
 
Tukubali,, Tanzania kuongeza Mishahara kwa asilimia 23%,, kwa Wafanyakazi wote ni ndoto za Abunuasi. Hapo kilichowekwa wazi ni Benchmark ya kima cha chini tu tu kwamba ni 23%,, hii statement '' ikiwemo kima cha chini kwa asilimia 23" muielewe vizuri. Yani hapo kila scale ina percent yake sema hawajataka kuweka wazi. Subiri mtakachokutana nacho julai ndio mtajua siasa ni mbaya kwa afya za wananchi😰😰😰😰😰
 
Ni hivi, rais ameongeza mshahara 23% ya mshahara wa kima cha chini kwa wafanyakaz wote .

Hakuna mahali wamesema rais ameongezea wenye kima cha chini tu. Hii ina maana gani,

Hii ina maana kuwa mshahara utaongezeka kwa 23% ya kima cha chini kwa wote, mfano kima cha chini let say ni laki 3, hivyo 23% yake ni elf 69,

Hivyo hata kama mshahara wako ni mil 1, unatoa kima cha chini ambacho ni laki 3, unatafuta 23% yake ambayo ni elf 69, Alaf unajumlisha na hiyo mil 1, kwaiyo mshahara wako utakuwa mil 1 na elf 69.

Hivo ndo maana yake, haya sasa anzieni hapo kujua mishahara yenu itakuwaje
Zaidi ya ramli chonganishi !!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndio hivyo sasa usichokubali ni nini?? Walimu bhana, mmezoea dhiki, shida, mateso, manyanyaso na chuki, hivyo kama mshazoea umasikini hivi.

MSHAHARA UNAONGEZWA KWA KILA MTU NA KWA KILA KADA KWA 23.3%. UTOFAUTI UTAONEKANA KWENYE KODI KWANI KODI HUTOZWA KAMA IFUATAVYO HAPA CHINI.

1. 332,000 Kushuka chini HAKUNA KODI.

2. 332,000 - 760,000
TAX = 20,000 + 20% Ziada ya 332,000.

3. 760,000 - 1,000,000
Tax = 68,000 + 25% ziada ya 760,000

4. 1,000,000 na Kuendelea
Tax = 128,000 + 30% ziada ya 1,000,000.

Wewe angalia utakuwa wapi katika nyongeza hiyo kisha unajua sasa kodi kiwango gani utalipa.
Nyongeza ya aina hiyo !!! Hadithi za Sindbad baharia !!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mnazidi wachanganya tu watumishi hivi serikalini msemaji wa serikali si aje atoe ufafanuzi au wale wandishi wetu wa you tube vipi hii siyo habari mbona issue za kija Jeff na kanze mnapanda mpaka magari vipi mnashimdwa mpigia sm waziri mwenye dhamana akafafanua hili suala maanaa watumishi kama hawaelewi vile
Wenye mishahara Yao wataiona kwenye salary slip zao. Wengine wataipanga huku jf. .

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Screenshot_20220516-120432.jpg
 
Nimeona wengi wanauliza nikaona nianzishe uzi labda kusaidia, ni hivi chukua asilimia ya kilichoongezwa mf. 28% gawanya kwa 100 yaani 28:100 halafu zidisha na Mshahara wako, yaani 0.28*(mshahar wako kabla ya kodi)= halafu jibu lake jumlisha tena na Mshahara wako, jibu lake ndiyo kiwango ulichoongezwa.

Huo mshahara kabla ya Kodi ndio ukokotoe!
Kweli Watumishi mlikuwa na NJAA sana ya mshahara

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Chukua mshahara wako GROSS SALARY X 1.233 = MSHAHARA MPYA

HAKUNA HAJA YA MBWEMBWE NYINGI... ILA HII KWA KIMA CHA CHINI
Hesabu inakusumbua,,hebu angalia hyo hesabu yako.

Gross salary ×0.233[emoji736]
Gross salary ×1.233[emoji777]
 
Hesabu inakusumbua,,hebu angalia hyo hesabu yako.

Gross salary ×0.233[emoji736]
Gross salary ×1.233[emoji777]
😁 hapa wewe ndo umepuyanga. Yako ni nyongeza siyo gross salary.
 
Nimeona wengi wanauliza nikaona nianzishe uzi labda kusaidia, ni hivi chukua asilimia ya kilichoongezwa mf. 28% gawanya kwa 100 yaani 28:100 halafu zidisha na Mshahara wako, yaani 0.28*(mshahar wako kabla ya kodi)= halafu jibu lake jumlisha tena na Mshahara wako, jibu lake ndiyo kiwango ulichoongezwa.

Huo mshahara kabla ya Kodi ndio ukokotoe!
%23.3 imeongezwa kwa kima cha chini, kadri mshahara unapoongezeka kutoka kima cha chini basi hiyo % inaenda ikipungua, yaani kulingana na ukubwa wa mshahara kuna ambaye ongezeko litakuwa <%5 nenda na ile principal ya " increasing with decreasing rate "
 
Back
Top Bottom