Jinsi ya kulala usingizi mtamu kila siku

Jinsi ya kulala usingizi mtamu kila siku

Usingizi mrefu na usio katikakatika ni muhimu sana kwa afya ya mwili, akili na roho. Mtu mzima anapaswa kulala si chini ya saa 8 kwa siku. Zingatia yafuatayo ulale usingizi mrefu na mtamu.

1. Oga kabla ya kulala

2. Kula chakula chepesi na kidogo walau saa moja kabla ya kulala.

3. Usinywe maji chini ya saa moja kabla ya kulala.

4. Tumikisha mwili au akili vizuri mchana ili ulale vizuri usiku.

5. Hakikisha chumba, matandiko na nguo za kulala ni safi, hakuna chawa, kunguni, etc.

6. Nguo za kulala ziwe nyepesi na laini.

7. Kitanda kiwe kikubwa na godoro liwe nene.

8. Egemeza shingo vizuri kwenye mto laini usio mkubwa wala mdogo sana.

9. Hakikisha chumba kina mzunguko mzuri wa hewa.

10. Hakikisha chumba kina giza totoro. Zima taa zote chumbani.

11. Zima simu au alarm zote kwenye simu.

12. Hakikisha hakuna kelele zozote ndani na nje ya chumba, zima redio, tv, etc

13. Lala kati ya saa 2 na saa 4 usiku.

14. Usilale kifudifudi.

15. Tumia chandarua kama kuna mbu

16. Usitumie caffeine kabla ya kulala hii ipo kwenye kahawa, chai, cocoa na vinywaji vyenye cola eg Coca Cola, pepsi cola, etc

17. Acha kujamiiana katikati ya usiku

18. Usilale na mtu anayekoroma. Malkia Elizabeth alilala chumba tofauti na mumewe Prince Andrew ili apate usingizi mzuri.

19. Usiendekeze mawazo hasi unapokwenda kulala

20. Sali kabla ya kulala. Omba Mungu ulinzi na usingizi mwema wakati wa usiku

NB: Jijengee mazoea ya kulala mapema utafurahia maisha zaidi na utakuwa na nguvu nyingi kimwili, kiakili na kiroho.
Hiyo namba 17 na sisi tulio owa inatuhusu...?
 
22.Hakikisha Huna Deni
23.Hakikisha Umetuma Pesa Kwa bi Mkubwa Kijijini Kwani Kama Anahaingaika roho Haitalala kwa amani Utaona Ndoto za Jinamizi
 
Kuna mitaa kulala Hadi bodaboda wamalize pilika zao ...kutwa mnasikia pikipiki zao
 
Umemwita Prince Andrew mume wake Malkia Elisabeth. Ushukuru M I 6 hawapo karibu.
 
11. Zima simu au alarm zote kwenye simu
🔨🔨🔨

Hapana, hii ya kuzima simu no way, bora useme weka sauti ndogo...kuna siku nilikuwa navamiwa huko nje jirani yangu akaniokoa kwa kunipigia simu kwamba kuna wezi wanataka kuruka ukuta waingie ndani...kuna siku nikapigiwa simu kijana wangu aliyekuwa safarini kapata ajali usiku....kuzima simu?? Nooooooo!!!!
 
17,tutakaa.Nimestuka 9 usiku usingizi umekata,pembeni ipo tandam ya kwenda,lazima niombe gemu lasivyo wote tuwe macho Hadi monie.Kifupi ni kwamba usingizi Mimi huja baada ya kupiga bao refu.
 
Back
Top Bottom