Jinsi ya kulipia kwa VISA

Naomba kuuliza baada ya kufungua hiyo akaunt inakuwa ni online tu au voda watakutumia physical MasterCard ahsante
 
Mkuu samahani naomba maelekezo ya alipay namna ya kujiunga,maana sehemu ya nchi Tanzania siioni. Naomba unifafanulie maana ninashindwa kujiunga nayo. Naomba usaidizi wako. Natanguliza shukrani zangu kwako.
 
Hivi ukitumia CRDB Bank Mastercard si ndio njia rahisi zaidi na unapata statements kirahisi?

Mimi huwa natumia CRDB MasterCard kwa online transactions. Naona iko poa sana pia
Mimi pia nimetumia sana CRDB Mastercard (zamani kabla ya kadi kuexpire)...shida ya hawa jamaa ni kwenye kuiruhusu kadi yako ifanye hizi online transactions.
Unapopewa kadi huwa haiwezi kufanya hizi transactions, wanataka mteja aridhie mwenyewe kwa kwenda bank na kujaza forms za kukubali kadi iruhusiwe. Ukijaza form watakutumia "code" kwenye simu ili uendelee na registration kupitia website yao ya crdb (Verify card through VBV). Shida inaanzia hapa, sijui wana tatizo gani maana ukishafika kuverify identity (kuingiza hiyo code) hakuna kinachoproceed mbele, na ukirudia mara tatu wanablock akaunti. Nimepata tabu matawi matatu ya mikoa tofauti (kwa kuwa nilikuwa nasafiri). Na kila ukienda wanakujazisha form upya ili utumiwe code nyingine. Nilishaenda ofisni kwao nikamwambia muhusika, najaza form, hiyo code itumwe nikiwa hapahapa, then fanya registration kwenye computer yako hapohapo, niondoke nikiwa nimelimaliza hili, akanijibu hawezi (nikachoka kabisa).
Kadi ya kwanza iliyoexpire nayo ilikuwa hivihivi. Kilichosaidia nilipost hii kadhia facebook, kuna jamaa (tulisoma naye, alikuwa crdb) akanifuata inbox. Nikarisk kumpa details zangu zote za kadi, akalitatua. Kiufupi CRDB Mikoani wako na shida sana na hii product. Washanifukuza, kuna bank nimeenda nimefungua akaunti, wamenipa kadi inayofanya hizi transactions hata dk15 haijaisha.
 
Tusaidie jina la hiyo bank inayofanya transaction ndani ya dakika 15 kama hutojali mkuu
 
Tusaidie jina la hiyo bank inayofanya transaction ndani ya dakika 15 kama hutojali mkuu
SIyo transaction Mkuu, ndani ya dk 15 ni kufungua account na kupewa card ambayo iko verified kufanya online transaction. Nilienda Absa Bank Kiongozi
 
Mkuu naomba maelezo kuhusu namna ya kujiunga na Alipay, ulifanyaje mpaka ukafanikiwa? Natanguliza shukrani zangu kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…