Jinsi ya kumtambua mtu anayeendesha gari ya shemeji yake

Jinsi ya kumtambua mtu anayeendesha gari ya shemeji yake

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Zifutazo ni tabia za vijana wanaoendesha gari za shemeji zao:-

I. Lazima washushe vioo mpaka chini kabisa kisha wanaweka kishoka.

II. Lazima waweke sauti kubwa sana ya radio yaani makelele barabara zote anazopita

III. Ana kimbiza gari ovyo ovyo hata kwenye makorongo hajali anajua shemeji atayengeneza tu

IV. Akiwa njiani kama kaona rafiki hawajamuona lazima awaite kujidai anawasalimia.

V. Ukimpigia simu anakukatia anakutumia sms " I'm driving, i will call you later"

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
vi)Saa zote wana haraka mihoni kibao hasa kwenye taa za kuongoza magari zinapowaka kijani tuu
 
MCHUNGUZI HURU

hii ni kwa hapa Bongo au unamzungumzia all over the world
 
Last edited by a moderator:
Sio waendeshao magari ya shemeji tu bali hata wanaoazima magari ya marafiki na ndugu zao nao huwa na tabia kama hizi
 
Wengine huwa wanawasha taa kubwa za mbele mchana ili watu wawe wanawaambia'umesahau kuzima taa zako'!
 
MCHUNGUZI HURU

Aisee wanakeraa! Kumbe ndo hawaaaa!
Juzi mtu kanishambulia mitusi hamu sina, kisa nimechelewa kidogo kuiona ya kijani!
 
Last edited by a moderator:
hukatiza mitaa ya mademu waliowatosa mara kwa mara. na wengi wao hupiga picha na magari hayo na kupost fb.
 
Umenikumbusha mbali sana kipindi nipo darasa la tano sista la saba kuna kijamaa form one nilikihisi kinamlamba sista akija home na backel me naichukua naenda kuvitembelea videm vyangu nikifika Shemeji zangu nao wanachukua baskel sijui nao wanaenda wap.

Nimejikuta nacheka tu.. kwahiyo hata huyo shemeji yako huenda nae aliazima tu hiyo baiskeli hahaaaa
 
Dah! Umenikumbusha kuna chalii flani alichukua gari la ndugu yake flani hivi sasa anatoka nalo kitaa akiona sehemu masela wamechil anajidai kushuka na kwenda kwenye tyre ya mbele na kutoa kichupa au kimsumari then anajipigapiga mikononi na kuongea mwenyewe hapo huku anaelekea kwenye gari.

Nilikuwa natamani kila siku nikutane na hicho kituko chake sababu kilikuwa ni extraordinary.
 
Mm hata kwa shemeji siwezi fika hata kama ninashida yakunitoa roho yangu cjui kwa sababu u arusha umenizidi lakini ndo wanachuga walivyo hakuna mtoto wa mama
 
akishuka kwenye gari ana karibu na bonet huku kaning'iniza funguo mkononi
 
Back
Top Bottom