Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hakuna forumula
amlete ukiwa haupo tu nyumbani
mkeo umkute kanuna na mtoto anatazama tv
kinachofuata ni maelezo tu
wakati jipu lishapasuliwa
Je ina maana utalazimisha kwa mkeo pokea mtoto? au utaacha mpaka siku anaoa au kuolewa
mtume mtoto akampelekee ela ya matumizi alafu amwambie baba kanipa nikulete hapo habari kwishaKuna majambo yanayowasibu wanaume wengi katika pitapita zao na kung'angania nyumba ndogo wanajikuta wanapata watoto nje ya ndoa ni njia ipi ya kistaarabu ya kumtambulisha mtoto wako wa nje kwa mkeo unayempenda????????
ni tamaduni tu
kuna nyumba nilienda, nikakuta unga, mchele na mafuta ya kupikia yanafichwa chumbani kwa wazazi, kidogo macho yanidondoke.
Hii ya mtoto wa nje na ndani kuna sehemu wala hawatofautishi, mimba tu inaletwa home.
Na mtoto kuletwa home si kwamba kimenuka, lakini lazima waotot wafahamiane wakiwa wadogo waweze kuishi pamoja.
Kwa hiyo, hakuna fomula, kama kwenu huwa wanaficha hadi siku unakufa/anakufa fuata hayo hayo.
Wapi dear ambako kuzaa nje ni sehemu ya maisha.
Kwa faida ya mabinti walio single embu tumegee hiyo siri.
My dad alimkataa kijana fulani alotaka kumuoa mdogo wangu kwa kigezo kuwa hao kazi yao kuzaa nje...wote tulibaki midomo wazi ...kumbe ni sehemu ya culture ya watu fulani.
wala si kuzaa nje tu.
Mwanamme anatoka jioni home
anakuaga 'ngoja nikatongoze'
anarudi labda saa nne hana shati
ana kanga kajitupia, anakuambia, nimeacha nguo wakusaidie kufua.
Kama hujaona utadhani story, sembuse mtoto ndio aache kwenda kwa babaye??
Kuna sehemu wake wengi ruksa, na usitegemee mtu anaoa tu bila kuwa hajafanya lolote. Sometimes wanazaa, wanaamua kuhalalisha.
Yote inategemea umekulia wapi
Kama umediriki kumwita mkeo unayempenda, huyo mtoto wa kando katokea wapi?
Afu mara nyingi ukiona mwanaume anaanza kufikiria kuleta mtoto wa nje ndani in most cases huko nyumba ndogo kimeshanuka...maana kama unaendelea ku mantain nyumba ndogo kwa nini unataka kuinyang'anya mtoto. Yeye hana right ya kulea mwanae? Au unamuona kicheche hana sifa za kulea?