Wanaume wa siku hizi haswa vijana wa mjini, akiona mwanamke mzuri tu amsemeshi pale pale, atamuangalia jinsi alivyo na kumfuatilia baada ya siku kadhaa. Kabla ya hapo, atasuka nywele kwanza, atoboe masikio, akanunue suruali inayobana mapumbu na isiyoifika matakoni, yaani haistili matako yake ili avae mlegezo, atatoboa pua, kisha atapaka lipstick. Akijiangalia kwenye kioo akiona anafanana na mwanamke ndipo ataenda kumtokea huyo demu na mapozi ya kibongo fleva, atajifanya anabana pua kuongea broken English ya wamarekani weusi na lafudhi ndeeeefu isiyoeleweka, huku akibinya mapumbu. Kicheko kinakuja pale anapotolewa nje na huyo demu, ghafla anarudi katika hali yake ya kawaida na sauti yake ya kawaida inarudi na kuanza kumkashifu bi dada, malaya gani wewe kwanza sijuwi ukoje, katika mademu we ni demu? Hivi tujiulize, mwanamke gani mwenye akili timamu anayetaka kutoka na mwanamme anayefanana kama demu au mwanamme asiyejitambua?