Rakims
JF-Expert Member
- Jun 4, 2014
- 5,002
- 4,571
Ikiwa ni mapenzi yako katika kujaribu kwenda kung'arisha au kutakasa nyota yako kwa mnajimu yoyote yule basi kuna mambo ni muhimu na unatakiwa kuyazingatia unapokwenda huko ili uweze kupata hitaji lako.
IPO HIVI:
Yeyote kati yenu atakapoenda kutaka kusafishwa nyota kwa mtu yoyote yule basi aende akiwa na backup ya mambo yafuatayo;
Basi fahamu kabisa kuwa hawezi kukusafisha nyota yako zaidi ya kukupa jini au uchawi ambao utakusukuma kwa muda fulani uone mafanikio kisha utaharibikiwa ili urejee tena kumpelekea pesa na atakugeuza kitega uchumi.
Mtaniwia radhi sihitaji quotes za watu hapa inayosema udini au damu kuwa maji na maji kuwa damu. Nyota ni maarifa kama ilivyo maarifa mengine ya kibinadamu.
Rakims
IPO HIVI:
Yeyote kati yenu atakapoenda kutaka kusafishwa nyota kwa mtu yoyote yule basi aende akiwa na backup ya mambo yafuatayo;
- Ahakikishe kwanza anaemfata anajua vema kuhusu nyota za watu kulingana na imani zao.
- Ajulikane ana nyota gani na ina tabia gani?
- Siku nzuri kwake ni zipi na mbaya ni zipi?
- Asili ya nyota yake ni ipi?
- Tabia ya nyota yake ni Ipi?
- Maada ya nyota yake ni Ipi? (Hili ni la kuzingatia zaidi MAJI,UPEPO,MOTO,UDONGO)
- Nyota yake inang'arishwa kwa mlango upo? (ambao yeye akiona mafanikio ndio atajua nyota imeng'aa
- Ascendant yake ni Ipi?
- Descendant yake ni ipi?
- Sharif yake ni ipi?
- Nuksi yake ni ipi?
- Direction yake kinyota ni ipi?
- Milango yake imekaa vipi?
- Malaika wa nyota yake ni yupi?
- Jini wa nyota yake ni yupi?
- Shetani wa nyota yake ni yupi?
- Nyota yake kwa muda huo ipo usawa gani?
- Cusps na decanates zake zipo vipi?
- Indication ya nyota yake ni ipi?
- Daraja la mwezi kwa nyota yake ni lipi?
- Daraja la sayari kwa nyota yake ni lipi?
- Amjuze alipotoka, alipo na anapokwenda? (Na ziwe acumulate na yeye)
- Ajue afinity zake?
- Angles zake ni vipi?
- Amtajie na thamani ya nyota yake na uwezekano wa kung'aa?
- Nini kinaweza kuboost nyota yake? (Madini,Vito,Mawe n.k)