Jinsi ya kununua kiwanja bila kutapeliwa

Jinsi ya kununua kiwanja bila kutapeliwa

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Kuna watu wengi sana wanatapeliwa katika kununua viwanja.

Binafsi nina mpango wa kwenda kununua kiwanja sehemu fulani.

Kwa wenye uzoefu, ningependa kufahamu ni taratibu zipi za kuzingatia kabla hujanunua kiwanja?
Je? kwenda kwa mwenyekiti wa mtaa pekee inatosha, utajuaje kama kiwanja husika ni kweli cha huyo anayeuza? kwamba sio cha familia n.k

Unaweza ongeza lolote lile ambalo unadhani ni la muhimu ukiwa unataka kununua kiwanja au shamba.

Karibuni kwa mjadala.
 
Kwa taarifa yako Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 haimtambui Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa kama Shahidi la muhimu nenda Wizara ya Ardhi uangalie mmiliki Halali wa hiyo ARDHI, kisha nenda kwa mwanasheria akutengenezee mkataba muende kwenye kiwanja, ujiridhishe mipaka, na akukabidhi NYARAKA ZOTE original (Zenye majina yake matatu mfano PURITY AKILI KAMUI wa S.L.P 21 OLASITI, ARUMERU, ARUSHA, TANZANIA), shahid wako awe mwanasheria, Majina yake 3, atie saini,cheo na muhuri wake. Pia hakikisha uhalali wa DOCUMENTS (TITLE DEED)
 
1.usilipe pesa bila kupewa nyaraka.

2.hakikisha umekiona.

3.usinunue kutoka kwa mke au mume pekee.

4.hakikisha kuna mkataba halali.
5.kama kimepimwa nenda ofisi ya ardhi kuhakiki taarifa.
 
Asante blessings kwa kutufungua macho, kumbe sheria ya ardhi haimtambui Mwenyekiti Serikali ya Mtaa. Naona watu wengi hatujui hilo
 
nijuavyo mimi ardhi ina expire umri wa ardhi umegawanyika hivi 33 66 and 99 years miaka 33 ni nyumba ya kawaida ya kuishi 66 na 99 ni nyumba za ibada na viwanda so kwanza tafuta lowyer akupe taratibu kabla hujafanya manunuzi
 
  1. Serikali za mitaa ni hatua ya awali kabla hujaenda kokote. Wanajua maeneo yanayowahusu na migogoro iliyopo. Kwa maeneo yaliyopimwa wanayo ramani ya kila kiwanja au ramani inayooonyesha mmiliki wa kiwanja na information za kila kiwanja.
  2. Serikali ya mtaa wakikuhakikishia kuwa kiwanja kinamilikiwa kihalali na mhusika anayekuuzia, hakikisha mauziano yanawahusisha mashahidi wakiwamo mwakilishi kutoka serikali ya mtaa.
  3. Mauziano kwa wanaotaka kukwepa gharama kubwa na kwa usalama zaidi bora kwenda mahakamani ambako mnunuzi, mwuzaji, mjumbe toka serikali ya mtaa na shahidi unayeona anafaa wakati wa kuandikishiana hati ya ununuzi wa kiwanja mahakamani.

Huu ndio utaratibu ambao huwa nautumia mimi na haujaleta matatizo, maana kwenda idara au wizara ya ardhi ni kwa viwanja vilivyopimwa jambo ambalo serikali ya mitaa wanazo documents na vielelezo vya kila eneo lao kiutawala. Idara ya ardhi ni pana na pengine itakurudisha huko huko kwa serikali ya mtaa. Jaribu kufuata utaratibu nilioainisha hapo juu utapata kiwanjwa kwa njia halali.
 
Asanteni wadau wote. Kuna wale waliokuwa wakimiliki mashamba yao miaka mingi sana iliyopita hivyo hawana doc zozote zile za kuthibitisha umiliki wa maeneo yao. Mfano, wamiliki wengi wa mashamba huko bagamoyo. Kwa situation kama hiyo unafanyaje?
 
Asanteni wadau wote. Kuna wale waliokuwa wakimiliki mashamba yao miaka mingi sana iliyopita hivyo hawana doc zozote zile za kuthibitisha umiliki wa maeneo yao. Mfano, wamiliki wengi wa mashamba huko bagamoyo. Kwa situation kama hiyo unafanyaje?

Ni vizuri ukishaoneshwa shamba utafute muda bila kumshirikisha muuzaji uwatafute majirani zaidi ya mmoja na wakati totauti uulizie kuhusu mmiliki halisi wa hayo maeneo. Other wise unaweza kuuziwa shamba ukaja kuambiwa wenyewe wapo Dar na hawauzi. Vile vile ni kama ni mzee mwenye shamba ni vizuri awashirikishe watoto wake ili baadae wasije kulalamika kwamba umemlaghai mzee wao.
 
Ni vizuri ukishaoneshwa shamba utafute muda bila kumshirikisha muuzaji uwatafute majirani zaidi ya mmoja na wakati totauti uulizie kuhusu mmiliki halisi wa hayo maeneo. Other wise unaweza kuuziwa shamba ukaja kuambiwa wenyewe wapo Dar na hawauzi. Vile vile ni kama ni mzee mwenye shamba ni vizuri awashirikishe watoto wake ili baadae wasije kulalamika kwamba umemlaghai mzee wao.

mkuu hapa umenena vyema. kwa upande wangu nna tatizo moja mzee aliuza kiwanja kwa siri (maana sio mama wala watoto kufahamu ). Yeye hafahamu kilipo na alieuziwa hafahamu pia maana mama ndo alikihangaikia kukipata ila akaandika jina la mzee katika hati baada ya mzee umwambia ataitumia kuombea mkopo. sasa tunataka anza fatilia hiki kiwanja maana mauziano yao naona kama yana utata je? tunaweza fanikiwa kwa hili mkuu.
 
Back
Top Bottom