Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

kwa mfano juz tumetoka dom njian jamaa mmoja ni afisa wa serikali alitoka dom amekunywa mchemsho wa kuku na chapati tatu ,soda na maji ya uhai lita 1 ,gairo kala chips na mishikaki 5 + soda+maji , msamvu kala juice ya 1 lta ya azam na biscut ya choclate, mizani ya mikese kanunua korosho za buku 3 ,chalinze kanununua mahind ya kuchoma na pepsi baridi wakati tunafika maili moja huyu mheshimiwa kanununua mayai 2 na maji hiv wana jf kweli vitambi vitapungua??

Usiombe huyo mtu akakutolea "kijambo" manake huo mchanganyiko wake ni balaa :whoo:
 
Mie nimeomba nielekezwe wapi naweza pata hizo majani ya chai.hayo ya jogging,maji ya moto sio ninachokitaka.


ok mi sifaham wapi utapata ila njia mbadala unayoweza kutumia ni MAZIWA YALIOCHACHA (MTINDI) unasaidia sana kupunguza tumbo.. kunywa walau mara mbili kwa siku... trust me u will see the difference.
 
Naomba mnisaidie nifanye mazoezi ya namna gani ili niweze kukata kitambi na kujenga misuli ya mwili bila ya kwenda Gym,mda wangu wa kwenda Gym hautoshi..Shukrani.
 
Punguza biere,wanga,vyakula vya mafuta.Piga nyagi wangu,yaani konyagi kwa sana.Kama hutumii pombe basi,piga pushapu za kulala chali na funga miguu kwa kamba.Unapopiga hizo pushapu usiinue miguu,bali make sure only kuanzia kiunoni hadi kichwa ndo vinainuka tu.Waweza fanya vyote hapo juu.Kwa siku ukipiga mia ndani ya wiki utafurahi.Piga asubuhi na jioni
 
No pain No gain, kubali mazoezi yawe sehemu ya maisha yako. Unaweza kuwa na vifaa vya mazoezi nyumbani kwako na ukapiga kaz za kueleweka.
 
Mazoezi kwa sana mzee, hususan kuruka kamba na kukimbia
 
kukimbia ni the best, ila kama huna muda wa kukimbia ruka kamba na fanya mazoezi ya sit ups kwa wingi.
 
Punguza kula starch na vyakula vya mafuta....punguza kunywa bia na ikitokea wataka kunywa then kunywa spirits kiasi...asubuhi ukiamka kabla hujapiga mswaki kunywa maji ya moto kwa kiwango uwezacho...jitahidi kufanya mazoezi na utafanikiwa.
Kumbuka unene unatokana na kula chakula kingi zaidi ya mahitaji ya mwili wako...zoezi na kula kiasi kutakusaidia...usisahau kunywa maji mengi sana....juice za kutengeneza nyumbani ni nzuri...abstain eating fast foods and soda.
best of luck.....
 
Naomba mnisaidie nifanye mazoezi ya namna gani ili niweze kukata kitambi na kujenga misuli ya mwili bila ya kwenda Gym,mda wangu wa kwenda Gym hautoshi..Shukrani.

Mara nyingi watu hasa sisi wenye vitambi huwa tunatamani au fikiria kuwe na mbadala wa mazoezi ili kupunguza vitambi..mfano chai za kichina, konyagi, mashine mbali mbali....hakuna kitu kama hicho. Siri ni mazoezi tu. Hongera mkuu kwa kutambua hilo na kutaka kufanya mazoezi kupunguza/kukata kitambi.

Inategemea kitambi chako ni cha ukubwa gani....lakini kitambi husababishwa na mlundikano wa mafuta kwenye abdominal wall (hata ndani ya abdomen yenyewe) unaotokana na kuingiza calories nyingi mwilini (kwa njia ya chakula) kuliko ambavyo unaweza kuzitumia.

Kwa hiyo cha kwanza ni kukata hiyo ziada ya calories unazoingiza mwilini kwa kufanya diet. Na pili kuchoma hiyo ziada iliyolundikana kama mafuta kwenye mwili wako. Unapochoma hiyo ziada ya mafuta mwili, kwa kuwa inajilundika kwenye abdominal wall (kitambi), basi kitaanza kupungua. Na hapo sasa ndio unaanza mazoezi ta kukaza misuli ili upate 'six packs'!

Kwa hiyo mazoezi ya kufanya ni: kukimbia (jogging) umbali mrefu, kutembea umbali mrefu, kisha ndio uanze kufikiria 'sit ups' za aina mbali mbali kukamilisha lengo!

Bahati mbaya wengi wetu huwa tunafikiria sit ups tu zitasaidia kukata kitambi, kwa hiyo nakaa tu nyumbani na kufanya sit ups 100 asubuhi na 100 jioni naona nimemaliza....hapana, unajichosha na kujiumiza bure. Kata mafuta kwa kuyachoma kwanza (jogging, walking) kisha sit ups zinafuata kukaza misuli!
 
Ukiamka fanya seatups kama mia hv then Kunywa maji ya moto asbh lita nzima ndani tia kijiko 1 kikubwa cha asali na mdalasini pia kijiko asubuhi kunywa chai isiyo na sukari na mkate kipande toasted na nusu yai la kuchemsha na embe nusu,mchana kunywa maji lita mbili na matunda kwa wingi isipokuwa parachichi,ukisikia njaa tafuna raisings(dhabibu kavu) jioni wali size ya ujazo wa kiganja chako na mboga za majani na samaki aliyechemshwa fanya hv kwa wiki 2 tumbo kwisa!!
 
Ukiamka fanya seatups kama mia hv then Kunywa maji ya moto asbh lita nzima ndani tia kijiko 1 kikubwa cha asali na mdalasini pia kijiko asubuhi kunywa chai isiyo na sukari na mkate kipande toasted na nusu yai la kuchemsha na embe nusu,mchana kunywa maji lita mbili na matunda kwa wingi isipokuwa parachichi,ukisikia njaa tafuna raisings(dhabibu kavu) jioni wali size ya ujazo wa kiganja chako na mboga za majani na samaki aliyechemshwa fanya hv kwa wiki 2 tumbo kwisa!!

Suruali bado itakaa vizuri kwenye kiuno? Maana wengine tunataka kupungua lakini hatuna bajeti ya kununua suruali mpya
 
Kuruka kamba na mazoezi ya aerobics, pamoja na kupunguza mila yenye vyakula vinavyoongeza wanga na mafuta itasaidia.lakini kupungua inawezekana lisiwe ni zoezi la wiki moja tu. Linataka muda kidogo ili mwili uweze kupokea mazoezi
 
Ukiamka fanya seatups kama mia hv then Kunywa maji ya moto asbh lita nzima ndani tia kijiko 1 kikubwa cha asali na mdalasini pia kijiko asubuhi kunywa chai isiyo na sukari na mkate kipande toasted na nusu yai la kuchemsha na embe nusu,mchana kunywa maji lita mbili na matunda kwa wingi isipokuwa parachichi,ukisikia njaa tafuna raisings(dhabibu kavu) jioni wali size ya ujazo wa kiganja chako na mboga za majani na samaki aliyechemshwa fanya hv kwa wiki 2 tumbo kwisa!!
...na mazoezi ya kutosha hasa ya kukimbia.
 
Hii sio ya kitaalamu bali ni mimi ninavyofanya na ndio inayonisaidia kupunguza tumbo.
Kwasababu vitu vya formula mimi huwa siwezi kuvifuata na huwa naviona vigumu sana kwahiyo huwa najaribu kuishi vile ninavyoweza.

Na kizuri zaidi ni kwamba hii sio diet ya kujinyima.
Ila unaweza usifanikiwe pia kutokana na mwili wako kwakua tumeumbwa tofauti lakini unaweza kujaribu kama itafanya kazi



Tukianza na asubuhi nikiamka mimi kama Mzizimkavu, naanza kunywa maji glass 3 ya Uvugu vugu kabla ya kupiga mswaki.
Na nikiisha amka nakunywa maji ya uvugu vugu yaliokamuliwa ndimu au limao glass zingine tatu kabla ya kunywa Chai.
Ukizoea maji ni matamu kuliko hata Bia
Kuwa Teja wa Maji kuna raha yake pia




Mimi napenda vitu vichachu kwahiyo maji saa zingine naya hisi kama yamepooza ila nikikamulia ndimu/limao kwenye maji ya uvuguvugu hata nisipoweka sukari yanaleta ladha fulani hivi

Ukiweza kunywa maji ya uvugu vugu kila wakati unapohisi kiu ya maji itakuwa vizuri au hata mara tatu kwa siku angalau



Si mpenzi sana wa Chai kwakuwa sipendi kabisa vitu vya sukari, lakini siku ninapo amua kunywa chai huwa nakunywa yenye tangazwizi nyingi sana na badala ya kutumia sukari huwa naweka asali...... Ila unaweza kutumia viungo vingine mbali mbali vya ki pwani (masala)



Asali




Kwa kifungua kinywa Sausage za kuchemsha au kama utakaanga iwe kwa mafuta yasiozidi kijiko kimoja kikubwa cha kulia (nashauri ya alizeti au olive)




Mayai ya kuchemsha si mabaya pia kwa kufungua kinywa

Kumbuka mimi huwa sifanyi diet hivi ndivyo ninavyokula na inasaidia


Badala ya kutafuna Sambusa, Popcorn na cookies au chocolate kila wakati bora muda wako uelekeze kwenye matunda, kama huwezi kupitisha lisaa bila kuweka kitu mdomoni





Mchana unaweza kupiga bakuli la mchemsho wa ndizi, ziwe Bukoba au za kule kwetu Moshi zote sawa kwakuwa mchemsho hauna mafuta kabisa unajilia kadri utakavyotosheka




Kuku Choma ni chakula kingine ambacho kinanifaa nyakati za mchana, lakini haswa hupendelea Kuku wa kienyeji ambao hawakukuzwa kwa madawa

Mara nyingi usiku naipotezea tu, pengine nalalia glass 2 za wine au beer kadhaa zisizozidi 3
Au Kuku wa kienyeji wa kuchemsha aliewekwa chumvi na ndimu na ka ndizi kamoja ka kuchemsha au kukaanga kwa mafuta kidogo sana




Ugali naupenda sana na huwa najiachia nao siku za kujiharibu

Lakini kumbuka wanga sio kitu cha kukiendekeza sana hasa unapotaka kutoa kitambi
Nikiona kinachomoza, napunguza maswala ya ugali.
Japo kwangu ni ngumu siku ipite bila Ugali, ila kumbuka miili inatofautiana... naweza nikala ugali mwaka mzima mwingine akala wiki akafumuka
So usinifatishe ila jaribu kupunguza au uepuke kama utaweza


Tumbo liko hapa sasa!!!!!

Hili ndio tatizo lililonikuta mpaka mkaona ile ishu imechomoka siku ya Birthday yangu


Kwakweli chips ni tamu hasa kwa sisi tunaofanya kazi za usiku ukirudi umejichokea unavamia tu



Unakuta unafululiza hata mwezi unazila kisha unaenda kulala
Japo tunapenda chips vumbi ila tuwe na kipimo isizidi, isiwe kila siku
Ukijumlisha na bia, daaah!! dah!!!!!! dah!!!!! shughuli imeisha



No. 1 enemy kwa vitambi vya wanawake ni hii kitu
Kula angalau mara moja kwa wiki tafadhali kama huwezi kuacha kabisa




Wenye kuweza kufanya sit ups pia fanyeni japo najua mazoezi ni magumu sana na yanatia uvivu hasa unapokuwa na kazi nyingi



Maji ni kitu cha lazima na cha kila siku
Ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu Asubuhi, Mchana na Usiku utafanikiwa japo kidogo



Narudia hii sio Diet ya kitaalam ni jinsi ninavyo ishi mimi, jaribu kama utaweza kufanikiwa kwa wale walioniomba ushauri.
Ila kama mwili wako ni mkubwa sana pia jaribu kupunguza kipimo cha chakula unachokula kila siku, ila usijinyime sana.

Mboga mboga kibao kila siku ukiamua mchana na jioni. Ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom