Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Unakunywa pombe?

Mimi nikiacha kunywa nakata uzito vizuri sana.
 
Tafuta kitabu kinaitwa SAYANSI YA MAPISHI kimeandikwa na Dr.Boazi Mkumbo ,pia fuatilia mafundisho yake Facebook na ana application yake Hea app
 
Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural

Ukipunguza kula na kufanya mazoezi NI LAZIMA upungue, KUNA kitu hakiko sawa kwenye issue yako ya Kula, mfano hata uwe na diet ipi, lakini ukila 30ms kabla ujaenda kulala tena chakula heavy hata kama ni mlo mmoja kwa siku utaendelea kunenepa, kagua hiyo diet yako
 
Naimani utaleta mrejesho hapa in few days,Hiyo ni mipangilio ya vyakula vyako ndo vinasababisha hayo,pia kwa mujibu wa kitabu chake kasema watu wenye matumizi makubwa ya wanga wanashambuliwa na ugumba,kisukari,ngozi isiovutia,uchovu kila wakati,

Haamini kama mazoezi na kujinyima ndio njia ya kutatua matatizo hayo,
Kiufupi amepindua sana mtizamo wa watu wengi Kwene suala la magonjwa haya yasiyoambukiza. Mm nilikinunua kwa 30,000 tu,ila sijutii
 
Dah me mwenyew nishawekaga dau kwa mtu anayetaka nimuwazime changu maana[emoji53] [emoji53]
 
Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural
Nitafute mkuu kama kweli una nia. Nitakusaidia bila gharama zaidi ya bundle utakayotumia kujibu viswali viwili vitatu.
 
Naimani utaleta mrejesho hapa in few days,Hiyo ni mipangilio ya vyakula vyako ndo vinasababisha hayo,pia kwa mujibu wa kitabu chake kasema watu wenye matumizi makubwa ya wanga wanashambuliwa na ugumba,kisukari,ngozi isiovutia,uchovu kila wakati,

Haamini kama mazoezi na kujinyima ndio njia ya kutatua matatizo hayo,
Kiufupi amepindua sana mtizamo wa watu wengi Kwene suala la magonjwa haya yasiyoambukiza. Mm nilikinunua kwa 30,000 tu,ila sijutii
Samahani mkuu kinauzwa wapi
 
Mkuu..wali pia inaleta kitambi,,, ebu kula dona kwa mboga mboga na acha kula wali kwa muda wa mwezi mmoja...alafu ulete feedback hapa.
 
Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural
Kitambi ni uzembe wa kwenda haja kubwa,hebu punguza huo uzembe ndani ya miezi 3 uone.
 
Mkuu ebu kuwa vegetarian kwa muda wa wiki mbili tu utaona mabadiriko,niliwahi kuwa na 97kgs,nikapiga tizi huku nikila supu ya samaki na mboga za majani kwa wiki2 nikapata 76kgs
 
Mkuu ulifanyaje nisaidie hili ni janga
Nianze kwa kusema mimi sio daktari ila tatizo la uzito lilinifanya nisome articles nyingi kuhusu kupungua nikagundua yafuatayo ;

1: Ini ni kiungo muhimu sana katika uchomaji wa mafuta , kwa hiyo ukiona mtu ana kitambi tafsiri ya haraka ni ini alichomi mafuta vizuri. Ndio kusema huwezi ondoa kitambi au kuchoma mafuta kwa mazoezi bila kutakua tatizo la ini.
- Kutatua tatizo la ini vitabu vinashauri 'detox diet' ila mimi nimetumia maji ya limau na vitunguu swaumu kila siku asubuhi kama detox agent. Unachukua vitunguu swaumu punje sita ,unakata kata vipande vidogo vidogo unameza kama dawa kwa kutumia maji glasi moja iliyokamuliwa limau,

2: Figo pia ni muhimu kwenye kupunguza uzito, figo hutumika kuchuja chakula na uchujaji unahitaji maji mengi kufanyika. Kwa hiyo kama sio mnywaji wa maji mengi kila siku mwili unatabia ya kuweka akiba ya maji mwilini ili figo likiyahitaji yatumike. Na maji mengi yanabaki maeneo ya tumbo 'waistline ' karibu na figo hivyo kutengeneza kitambi au unene.
- Kutatua hili utatakiwa unywe lita 3 za maji kila siku, sio kwa mara moja kidogo kidogo unaweza kunywa kila baada ya masaa kadhaa mwisho wa siku zifikie hizo lita. Kwa kufanya hivyo mwili utakuwa na uhakika na maji na utaanza kuyaachia maji ya ziada baada ya siku tano hivyo utapungua kiasi. Kwa maji pekee unaweza kukata kilo 5.

3.Usiache kula breakfast na lunch na usile wali usiku au kitu cha wanga. Mimi nilitumia tikiti kama dinner nusu au robo kipande.
Mimi niliachana na sukari kwenye chai na hakikisha hauli chakula cha usiku baada ya saa 1 usiku.

4:Achana na soda au pombe ,punguza wanga , vitu vya mafuta kula.

5: Kabla ya kulala kata kata vitunguu swaumu punje 3 meza na maji ya uvuguvugu glass moja kama dawa.

6: Ukiweza tembea kwa lisaa mara 3 au zaidi kwa wiki.

Nilikuwa na kilo 101 sasa nina 79 kitambi hakipo kabisa, ila serious changes utaanza kuziona siku ya 15 toka uanze.
 
Maji ya vuguvugu na mazoezi pia punguza chakula unachokula na hakikisha asilimia 75 no matunda na mboga za majani utafanikiwa
 
Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural
Wewe ni ke au me?
 
Back
Top Bottom