Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Usile chakula chochote kizito baada ya 1900hrs.

Usiku kula matunda pekee.

Usinywe bia (kama unakunywa)

Kunywa maji lita 3-5 kwa siku

Nenda gym at least mara 3 kwa wiki. (eg. monday, wednesday, friday)

Tumia whey protein Supplements (napendekeza optimum nutrition gold whey, muhimu sana) utumie one scoop per day (asubuhi) hii itasaidia kujenga misuli yako. Misuli mikubwa huchoma mafuta kwa kasi zaidi.

Acha/punguza kula nyama nyekundu (ng'ombe, mbuzi, kitimoto) ule zaidi white meat (kuku, samaki)

Achana kabisa na soda. Tumia Yoghurt instead.

Mwisho kabisa, kama ukifanya kila kitu kama nilivyokuelekeza, utahitaji at least wiki 12 ili uone matokeo katika mwili wako.

Mazoezi ni wito. Jitume, jitese. Utapungua vizuri bila kuathiri afya yako.
Naomba muongozo, optimum nutritional gold ni kitu gani??
 
Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural

Pole sana na hongera kwa kutambua kwamba unahitaji kupunguza uzito ili kuboresha afya yako. Kwanza kabisa, ACHANA NA DHANA ya kupunguza uzito KWA HARAKA, tena kwa njia za 'artificial' kama ulivyoziita wewe. Kumbuka mpaka umefika hapo kwa uzito huo ulio nao, lazima itakuwa imechukua miaka kadhaa kupata uzito na kitambi. Unene na kitambi umekijenga polepole kwa miaka kadhaa sasa. Hivyo, kitu ulichokijenga kwa miaka kadhaa HAIWEZEKANI NA HUTAWEZA kukiondoka kwa wiki au miezi kadhaa. Ni hatari kwako, hata kama utaona umefanikiwa kupunguza uzito kwa kiwango fulani utakuja kupata madhara ya kiafya huko baadaye, maana kuna uwezekano wa unene na kitambi chako kujirudia tena. Muhimu unachotakiwa kufanya ni polepole KUBADILISHA TABIA NA MTINDO WAKO WA MAISHA. Jenga tabia na mazoea mapya polepole - ifanye iwe ajenda yako mpya ya maisha. Jipe muda wa kutosha - hata ikibidi miezi au miaka. Badilisha tabia na kuzingatia chakula, kiwango cha chakula, aina ya chakula, uwingi wa chakula, muda unaokula chakula, nk. Zingatia aina ya kazi/shughuli unazofanya ili uzingatia uwe unakula nini na kwa kiwango gani. Inategemea na umri na kazi au shughuli unazofanya. Kama unafanya kazi za ofisini unashauriwa ule kiasi kidogo maana mwili wako hautaweza kuchakata vizuri, lakini kwa wale wenye shughuli ngumu, kama za ujenzi, ubebaji mizigo n,k wanaweza kula zaidi maana chakula kinatumika kuchakatwa ipasavyo.

1) Jenga tabia na mazoea ya kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara, sio ukali/ugumu wa mazoezi bali ni kujenga mazoea ya kufanya mara kwa mara (Frequency) kama kutembea angalau nusu saa angalau mara tatu kwa wiki, kuongelea, n,k
2) Kula mbogamboga na matunda zaidi lakini kwa kiwango kidogo, achana na nyama, hasa nyama nyekundu, ukishindwa kuvumlia basi kula samaki zaidi
3) Kunywa maji kwa wingi ya uvuguvugu hasa muda wa kuanzia asubuhi hadi jioni
4) Lala mapema na amka mapema.

Kila la heri
 
asee nasikia kuvuta bangi nyingi kunapunguza uzito....Kama hutojali jaribu..😱😱😱
 
Punguza kula vyakula vya wanga,kwa kiasi kikubwa vinachangia uzito kuongezeka,angalia tu hii asubuhi umekula chapati,mchana ugali ,usiku wali
Pia pangilia mpangilio wako wa chakula kuanzia asubuhi mpaka jioni
Asubuhi unaeza kula sana,machana kidogo na usiku ni kidogo zaidi (yaani unakuwa unatengeneza kama triangle inayoangalia chini) ukiweza usiku unaweza kulalia matunda au glass ya mtindi
All the best
 
Punguza kula vyakula vya wanga,kwa kiasi kikubwa vinachangia uzito kuongezeka,angalia tu hii asubuhi umekula chapati,mchana ugali ,usiku wali
Pia pangilia mpangilio wako wa chakula kuanzia asubuhi mpaka jioni
Asubuhi unaeza kula sana,machana kidogo na usiku ni kidogo zaidi (yaani unakuwa unatengeneza kama triangle inayoangalia chini) ukiweza usiku unaweza kulalia matunda au glass ya mtindi
All the best
Kunywa bia 1 kwa bili yangu tafadhali
 
Hiku sindiyo kitambi chenyewe, au kitambi ni mlubdukano wa mavwi tumboni?
 
Fanya mazoezi ya cardio kama kuendesha baiskeli aka ingini kiuno. Pia acha kunywa bia kabisaa kaa mwaka hivi..acha kula samaki wa kuaanga, vutumbua, maandazi na lishe zote za namna hiyo utakuwa ok...fanya sana ngono ya kibabe eve day
Napenda vitumbua jmnii[emoji30] [emoji30]
 
Vitu vingi hapo juu nimeshajaribu lkn kitambi kiko pale pale
 
Hii mada iendelee wahenga, maana kakitambi naona kameanza
 
Mkuu muulize SETH yule Singasinga wa IPTL nilimuona Kisutu kitambi hakipo tena yuko flat, sijui katumia dawa gani?
 
Back
Top Bottom