Nimepunguza sana kula, but holaa uzito bado ni mkubwa
Ninafanyafanya mazoezi pia but still hola. Nina waswas naweza kuja kupata overweight related problems kama BP, kisukari! Nahitaji dawa yoyote whether artificial au natural
Pole sana na hongera kwa kutambua kwamba unahitaji kupunguza uzito ili kuboresha afya yako. Kwanza kabisa, ACHANA NA DHANA ya kupunguza uzito KWA HARAKA, tena kwa njia za 'artificial' kama ulivyoziita wewe. Kumbuka mpaka umefika hapo kwa uzito huo ulio nao, lazima itakuwa imechukua miaka kadhaa kupata uzito na kitambi. Unene na kitambi umekijenga polepole kwa miaka kadhaa sasa. Hivyo, kitu ulichokijenga kwa miaka kadhaa HAIWEZEKANI NA HUTAWEZA kukiondoka kwa wiki au miezi kadhaa. Ni hatari kwako, hata kama utaona umefanikiwa kupunguza uzito kwa kiwango fulani utakuja kupata madhara ya kiafya huko baadaye, maana kuna uwezekano wa unene na kitambi chako kujirudia tena. Muhimu unachotakiwa kufanya ni polepole KUBADILISHA TABIA NA MTINDO WAKO WA MAISHA. Jenga tabia na mazoea mapya polepole - ifanye iwe ajenda yako mpya ya maisha. Jipe muda wa kutosha - hata ikibidi miezi au miaka. Badilisha tabia na kuzingatia chakula, kiwango cha chakula, aina ya chakula, uwingi wa chakula, muda unaokula chakula, nk. Zingatia aina ya kazi/shughuli unazofanya ili uzingatia uwe unakula nini na kwa kiwango gani. Inategemea na umri na kazi au shughuli unazofanya. Kama unafanya kazi za ofisini unashauriwa ule kiasi kidogo maana mwili wako hautaweza kuchakata vizuri, lakini kwa wale wenye shughuli ngumu, kama za ujenzi, ubebaji mizigo n,k wanaweza kula zaidi maana chakula kinatumika kuchakatwa ipasavyo.
1) Jenga tabia na mazoea ya kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara, sio ukali/ugumu wa mazoezi bali ni kujenga mazoea ya kufanya mara kwa mara (Frequency) kama kutembea angalau nusu saa angalau mara tatu kwa wiki, kuongelea, n,k
2) Kula mbogamboga na matunda zaidi lakini kwa kiwango kidogo, achana na nyama, hasa nyama nyekundu, ukishindwa kuvumlia basi kula samaki zaidi
3) Kunywa maji kwa wingi ya uvuguvugu hasa muda wa kuanzia asubuhi hadi jioni
4) Lala mapema na amka mapema.
Kila la heri