Mkuu ulifanyaje nisaidie hili ni janga
Nianze kwa kusema mimi sio daktari ila tatizo la uzito lilinifanya nisome articles nyingi kuhusu kupungua nikagundua yafuatayo ;
1: Ini ni kiungo muhimu sana katika uchomaji wa mafuta , kwa hiyo ukiona mtu ana kitambi tafsiri ya haraka ni ini alichomi mafuta vizuri. Ndio kusema huwezi ondoa kitambi au kuchoma mafuta kwa mazoezi bila kutakua tatizo la ini.
- Kutatua tatizo la ini vitabu vinashauri 'detox diet' ila mimi nimetumia maji ya limau na vitunguu swaumu kila siku asubuhi kama detox agent. Unachukua vitunguu swaumu punje sita ,unakata kata vipande vidogo vidogo unameza kama dawa kwa kutumia maji glasi moja iliyokamuliwa limau,
2: Figo pia ni muhimu kwenye kupunguza uzito, figo hutumika kuchuja chakula na uchujaji unahitaji maji mengi kufanyika. Kwa hiyo kama sio mnywaji wa maji mengi kila siku mwili unatabia ya kuweka akiba ya maji mwilini ili figo likiyahitaji yatumike. Na maji mengi yanabaki maeneo ya tumbo 'waistline ' karibu na figo hivyo kutengeneza kitambi au unene.
- Kutatua hili utatakiwa unywe lita 3 za maji kila siku, sio kwa mara moja kidogo kidogo unaweza kunywa kila baada ya masaa kadhaa mwisho wa siku zifikie hizo lita. Kwa kufanya hivyo mwili utakuwa na uhakika na maji na utaanza kuyaachia maji ya ziada baada ya siku tano hivyo utapungua kiasi. Kwa maji pekee unaweza kukata kilo 5.
3.Usiache kula breakfast na lunch na usile wali usiku au kitu cha wanga. Mimi nilitumia tikiti kama dinner nusu au robo kipande.
Mimi niliachana na sukari kwenye chai na hakikisha hauli chakula cha usiku baada ya saa 1 usiku.
4:Achana na soda au pombe ,punguza wanga , vitu vya mafuta kula.
5: Kabla ya kulala kata kata vitunguu swaumu punje 3 meza na maji ya uvuguvugu glass moja kama dawa.
6: Ukiweza tembea kwa lisaa mara 3 au zaidi kwa wiki.
Nilikuwa na kilo 101 sasa nina 79 kitambi hakipo kabisa, ila serious changes utaanza kuziona siku ya 15 toka uanze.