Hakuna shoti kati katika kutoa kitambi...njia nzuri na ni nzuri kwa afya ni kufanya mazoezi kama wadau wengine walivyopendekeza na kuachana na vyakula vya mkaango na kutokunywa vinywaji vyenye sukari...Sikushauri utumie madawa yeyote utaharibu afya yako...Hizo dawa daktari gani kazipitisha...TBS wamezipitisha ubora wake???
Kalori ambazo mwanamke inabidi ale kwa siku ni 2000 (umri wa miaka 19-30 na kama hufanyi mazoezi) na kama unafanya mazoezi kwa umri huo huo unahitaji kalori 2400....Kama utazidisha kalori hizo kwa siku basi lazima utakuwa mnene!!!
Kuna vitu kama mboga mboga, viazi vitamu ila usiweke mafuta hata ule kiasi gani huwezi kupata unene...Ningekushauri ule sana viazi vtamu zaidi sababu vinajaza tumbo na hutajisikia njaa mara kwa mara...utabaki kunywa maji kwa wingi...Wateja wangu wengi huwa ninawashauri njia hii na wanafanikiwa sana
Kama ingekuwa rahisi kutoa kitambi kwa kunywa dawa basi matajiri wengi na wenye pesa zao usingewaona "wakipoteza" mda wao ktk ma gym....
Sorry kitambi ni dalili ya unene!!! Hebu umewahi kumwona mtu mwenye 6 au 8 packs na ni menée??? Huwezi ukawa na flat stomack kama ni mnene!!! Unene unaanza tumboni baadae hips, mikononi etc....