Jinsi ya Kuongea na Ndugu Yako Aliyekufa

Hapana. Ukijikumbusha watu ambao wanajinasibisha na majini, utagundua kuwa ni uislam.
Duh! Mkuu mbona mada inahusu watu waliyokufa au mizimu na sio majini, mambo ya mizimu kufanyia matambiko au kuomba mizimu ni mambo ya kiafrika zaidi sio ya waislamu. Wazungu ndio wanaongoza kwa imani za kuongea na wapendwa wao waliyokufa.
 
Ndugu yako aliyekufa, anatamani kuongea na wewe, lakini wewe hufahamu njia ya kukuwezesha kuongea naye. Inawezekana mambo yamekuwa magumu na unaamini unahitaji ushauri wake, inawezekana umemkumbuka tu na ungependa uzungumze naye, na inawezekana alifariki mkiwa katika ugomvi sasa unataka mmalize tofauti zenu na pengine unataka ushauri kutoka kwake. Kwa sababu yoyote ile unaweza kuongea na ndugu yako aliyekufa!

Vifaa unavyohitaji ili kuwezesha kuongea naye

Mchele

Mchele ni zao pendwa katika nchi yetu. Ni mchele huu huleta chakula pendwa wali. Kwa hivyo mchele ni kifaa muhimu.

Pombe

Pombe itatumika katika kukuhamisha mawimbi (frequency).

Beseni lenye maji

Hii ipo kwa ajili ya kutuliza mawimbi na kufanya mtandao wa kiulimwengu ukamate vyema. Beseni la maji linafanya kazi sawa na dishi la kisimbuzi katika kuonesha channel za televisheni.

Boga la ukubwa wowote

Linasimama kama mtandao (Network).

Mziki wenye mapigo ya 520 Hz

Huu ni mahususi kwa kuondoa msongo wa mawazo na kuponya matatizo ya kisaikolojia. Ili kuweza kuongea na ndugu yako aliyekufa, unahitaji utulivu wa hali ya juu katika akili yako.

Ili kuweza kuupata muziki wa aina hii, utahitaji kukodi mpiga zeze mwenye uelewa, kama huwezi, utawasha muziki huu niliokuwekea.

View: https://www.youtube.com/watch?v=ZQkBmCJG9i8

Muziki wenye mapigo ya 852 Hz

Huu upo mahususi kwa ajili ya kuamsha jicho la tatu (pineal gland). huwezi kumuona aliyekufa bila kuamsha jicho la tatu. Ndiyo unalo jicho la tatu. Ni jicho hili ndilo hutambua mambo mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida, kwa mfano, inapofika usiku, jicho la tatu, hufahamu hilo na kukutengenezea usingizi. Mwanga ukiingia hata kama umelala jicho la tatu hutambua hilo na kukufanya uamke.

View: https://www.youtube.com/watch?v=joXu1AMzzWg&t=19s

Zoezi lenyewe

Hakikisha unasababu ya muhimu ya kumuita ndugu yako ili uongee naye. Usimuite akaja halafu ukabaki huna neno, hawezi kukudhuru lakini atakutisha! Kwa hivyo kuwa na hoja za msingi umuitapo.

Siku tatu kabla hujafanya zoezi la kuzungumza naye, mfikirie yeye tu. Kila unapotembea, unapofanya kazi mfikirie. Kumbuka mambo aliyowahi kufanya na muwaze sana. Ukimaliza hatua hii, ingia katika zoezi rasmi.

Saa sita usiku

Mchele kilo moja, weka katika beseni.

Pombe ya asili majagi mawili. Kama huna au huifahamu, nunua bia nne.

Beseni lenye maji liwe pembeni.

Boga.

Mpiga zeze kama ulimpata, au tumia simu yako kucheza miziki iliyoelekezwa.

Mpangilio

Kaa katikati ya mchele, beseni, na boga. Yaani, mchele uwe kushoto, beseni la maji liwe kulia na boga liwe mbele yako. Mpiga zeze kama yupo atakaa mbele ya boga. Kama unatumia simu kucheza muziki wa mapigo tajwa, kaa nayo simu hiyo. Pombe zako uwe nazo hapo ulipokaa.

Dakika tatu

Tumia dakika tatu kumfikiria ndugu yako. Kisha fungua pombe ya kwanza ili uanze zoezi rasmi la kuhama mawimbi (frequency) kunywa pombe zako ukiwa unasikiliza ule mziki tajwa. Bia ya kwanza na ya pili, sikiliza 520 Hz, bia ya tatu na nne sikiliza 852 Hz.

Ukimaliza, pombe zako, anza kumuita ndugu yako taratibu,usiwaze kitu chochote. Kama ndugu yako ataona wewe si muoga, atakuja. Ongea naye shinda yako bila kuogopa.

Endapo utamuita kwa dakika 20 mfululizo naye asije, maana yake ni kwamba, ndugu yako ameona wewe ni muoga. Ameamini kwamba akikutokea utakimbia na hutafanya chochote. Basi ndugu yako huyu anasubiri ulale ili akutokee ndotoni.

Kama ndugu yako hakutokea, kaa saa moja, kisha nenda msalani kutoa haja ndogo, halafu rudi kulala. Unapolala, mfikirie ndugu yako, fikiria umuhimu wa wewe kuongea naye.

Basi utakapokuwa umelala, saa la kwanza utakuwa katika usingizi mwepesi, saa la pili utazama kidogo, saa la tatu utakuwa ndani kabisa usingizini, nalo saa la nne, utakuwa katika ndoto, utamuona ndugu yako katika ndoto, mweleze shida yako, mweleze jambo lako.

Nakutakia kila la heri.

Kama Una Swali, Uliza Nitajibu, au Wasiliana Nami Moja Kwa Moja Kwa Kugusa Hapa.

Mimi sifanyi haya ila mara kwa mara nawaona wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki kuja kunisalimu na kunipa mwongozo pale ninapokuwa na matatizo. Mshana Jr hili limekaaje?
 
Duh! Mkuu mbona mada inahusu watu waliyokufa au mizimu na sio majini, mambo ya mizimu kufanyia matambiko au kuomba mizimu ni mambo ya kiafrika zaidi sio ya waislamu. Wazungu ndio wanaongoza kwa imani za kuongea na wapendwa wao waliyokufa.
Kwani kuna tofauti gani kati ya majini na mizimu wakati yote ni mizimu?
 
Umejuaje?
Hizi mambo za kuongea na Marehemu nimezikuta South Africa, Mimi pia nilishiriki nikijua naongea na Wapendwa wangu waliokufa....!

Ila baada ya miaka mingi macho yangu ya kiroho yakafunguka, nikaanza kuona vile ambavyo macho ya kawaida hayawezi kuona....! Nikaujua Ukweli.
 
Hiyo kwa kiafrika zaidi ila ni tofauti na kwa wenzetu huko ambako wanaenda kwa mediums ili waweze kuwasiliana na ndugu zao waliyokufa na wala hakuna huko mambo ya mizimu kutambika.
Kila sehemu Shetani ana namna yake ya kuwafikia Watu wake....!
 
Ndugu yako aliyekufa, anatamani kuongea na wewe, lakini wewe hufahamu njia ya kukuwezesha kuongea naye. Inawezekana mambo yamekuwa magumu na unaamini unahitaji ushauri wake, inawezekana umemkumbuka tu na ungependa uzungumze naye, na inawezekana alifariki mkiwa katika ugomvi sasa unataka mmalize tofauti zenu na pengine unataka ushauri kutoka kwake. Kwa sababu yoyote ile unaweza kuongea na ndugu yako aliyekufa!

Vifaa unavyohitaji ili kuwezesha kuongea naye

Mchele

Mchele ni zao pendwa katika nchi yetu. Ni mchele huu huleta chakula pendwa wali. Kwa hivyo mchele ni kifaa muhimu.

Pombe

Pombe itatumika katika kukuhamisha mawimbi (frequency).

Beseni lenye maji

Hii ipo kwa ajili ya kutuliza mawimbi na kufanya mtandao wa kiulimwengu ukamate vyema. Beseni la maji linafanya kazi sawa na dishi la kisimbuzi katika kuonesha channel za televisheni.

Boga la ukubwa wowote

Linasimama kama mtandao (Network).

Mziki wenye mapigo ya 520 Hz

Huu ni mahususi kwa kuondoa msongo wa mawazo na kuponya matatizo ya kisaikolojia. Ili kuweza kuongea na ndugu yako aliyekufa, unahitaji utulivu wa hali ya juu katika akili yako.

Ili kuweza kuupata muziki wa aina hii, utahitaji kukodi mpiga zeze mwenye uelewa, kama huwezi, utawasha muziki huu niliokuwekea.

View: https://www.youtube.com/watch?v=ZQkBmCJG9i8

Muziki wenye mapigo ya 852 Hz

Huu upo mahususi kwa ajili ya kuamsha jicho la tatu (pineal gland). huwezi kumuona aliyekufa bila kuamsha jicho la tatu. Ndiyo unalo jicho la tatu. Ni jicho hili ndilo hutambua mambo mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida, kwa mfano, inapofika usiku, jicho la tatu, hufahamu hilo na kukutengenezea usingizi. Mwanga ukiingia hata kama umelala jicho la tatu hutambua hilo na kukufanya uamke.

View: https://www.youtube.com/watch?v=joXu1AMzzWg&t=19s

Zoezi lenyewe

Hakikisha unasababu ya muhimu ya kumuita ndugu yako ili uongee naye. Usimuite akaja halafu ukabaki huna neno, hawezi kukudhuru lakini atakutisha! Kwa hivyo kuwa na hoja za msingi umuitapo.

Siku tatu kabla hujafanya zoezi la kuzungumza naye, mfikirie yeye tu. Kila unapotembea, unapofanya kazi mfikirie. Kumbuka mambo aliyowahi kufanya na muwaze sana. Ukimaliza hatua hii, ingia katika zoezi rasmi.

Saa sita usiku

Mchele kilo moja, weka katika beseni.

Pombe ya asili majagi mawili. Kama huna au huifahamu, nunua bia nne.

Beseni lenye maji liwe pembeni.

Boga.

Mpiga zeze kama ulimpata, au tumia simu yako kucheza miziki iliyoelekezwa.

Mpangilio

Kaa katikati ya mchele, beseni, na boga. Yaani, mchele uwe kushoto, beseni la maji liwe kulia na boga liwe mbele yako. Mpiga zeze kama yupo atakaa mbele ya boga. Kama unatumia simu kucheza muziki wa mapigo tajwa, kaa nayo simu hiyo. Pombe zako uwe nazo hapo ulipokaa.

Dakika tatu

Tumia dakika tatu kumfikiria ndugu yako. Kisha fungua pombe ya kwanza ili uanze zoezi rasmi la kuhama mawimbi (frequency) kunywa pombe zako ukiwa unasikiliza ule mziki tajwa. Bia ya kwanza na ya pili, sikiliza 520 Hz, bia ya tatu na nne sikiliza 852 Hz.

Ukimaliza, pombe zako, anza kumuita ndugu yako taratibu,usiwaze kitu chochote. Kama ndugu yako ataona wewe si muoga, atakuja. Ongea naye shinda yako bila kuogopa.

Endapo utamuita kwa dakika 20 mfululizo naye asije, maana yake ni kwamba, ndugu yako ameona wewe ni muoga. Ameamini kwamba akikutokea utakimbia na hutafanya chochote. Basi ndugu yako huyu anasubiri ulale ili akutokee ndotoni.

Kama ndugu yako hakutokea, kaa saa moja, kisha nenda msalani kutoa haja ndogo, halafu rudi kulala. Unapolala, mfikirie ndugu yako, fikiria umuhimu wa wewe kuongea naye.

Basi utakapokuwa umelala, saa la kwanza utakuwa katika usingizi mwepesi, saa la pili utazama kidogo, saa la tatu utakuwa ndani kabisa usingizini, nalo saa la nne, utakuwa katika ndoto, utamuona ndugu yako katika ndoto, mweleze shida yako, mweleze jambo lako.

Nakutakia kila la heri.

Kama Una Swali, Uliza Nitajibu, au Wasiliana Nami Moja Kwa Moja Kwa Kugusa Hapa.

Ishi na Watu vizuri, pia wapeni watoto wenu majina mazuri yanayovutia hata waliotangulia mbele za haki. Kuna wengine huongea nao hata bila hayo mambo yote
 
Ahsante sana Mkuu.. Umeeleza vizuri sana kuhusu hizi mambo zinavyooperate.. Nimeelewa vizuri. Mwenye akili na aelewe.
Shukrani....!

Kile watu hawaelewi, Binadamu wenyewe ndiyo wanawapa Nguvu hayo Majini wakijua ni Mizimu.

Mfano:
Babu Yako alikua na Majini akiamini ni Mizimu ya Ukoo, Babu kafa, katika Watoto wake, hakuna hata mmoja anayeenda kutambika, yale Majini Sasa yanakosa Nguvu, coz majini yaahitaji Damu na mambo mengine ili yawe na Nguvu na kuweza Survive, yaachofanya ni kutafuta Wajukuu watoto, wanaangalia nani wamwingie, hawaingii Kwa Yeyote tu, wanaangalia mwenye Channel ama mwenye Nyota Kali (That's why sio Kila Mtu tu anaweza kuwa Mchawi ama Mganga, lazima uwe na chanell)

Unakuta Mtoto mdogo ana Akili anafanya vizuri shuleni, ghafla anaanza kupandisha Mapepo, masomo yanashuka, kosa Wazazi wanafanya wanampeleka Kwa Mganga, kumbuka nguvu iliyo nyuma ya Mtoto, na Nguvu iliyo nyuma ya Mganga, source ni Moja.

Mganga anasema Mizimu ya Baba inataka mkatambike, then mnaamua kwenda kutambika, hapo ndo mmekua mmelipa nguvu lile Jini, mmeliimarisha, mtakua Watumwa, Makosa kidogo, Ukoo Mzima utateseka.

Kuna Koo Leo Zina Laana Kwa sababu ya kuabudu hizi mambo za Mizimu, Kuna familia hazitoboi, ikitokea ni mmoja ama wawli tu, na Hawa walitafuta msaada.
Kuna familia Wanawake hawaolewi.
Kuna familia Kila wakifika Umri Fulani wanakufa.
Yote ni sababu ya kuabudu Majini mikijua ni Mizimu.
Shetani hanaga Nisamehe sirudii Tena, Shetani hanaga huruma.
 
Kwani kuna tofauti gani kati ya majini na mizimu wakati yote ni mizimu?
Kama ni hivyo sasa kwanini unahusisha waislamu na mizimu wakati imani ya mizimu imekuwepo tangu na tangu ulimwenguni kote na hadi sasa waafrika bado wana mambo ya kutambikia mizimu, iweje wewe leo useme ni mambo ya waislamu?
 
Kwani kuna tofauti gani kati ya mizimu na dini?
 
Mizimu inaaminika ni roho za watu waliyokufa sasa inahusiana na vp dini? Imani za mizimu zimekuwepo kitambo sana sasa smnashangaa unaposema ni mambo ya waislamu.
 
Back
Top Bottom