Jinsi ya kuongeza umakini (mawazo) katika mipango ya maisha

Jinsi ya kuongeza umakini (mawazo) katika mipango ya maisha

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Wasalaam ndugu zangu waswahili,

Leo nina hoja nzito saana upande wangu naomba tupeane ushauri mzuri tafwadhali... uki comment kebehi utalaaniwa immediately.

Ni hivi kwanza nini siri ya kufanikiwa katika maisha??

Binafsi nilikua na ndoto kubwa saana kiasi kilinisukuma kuset appointment ikulu nikiwa napambania kutimiza ndoto zangu.

I have tried kufanya biashara za kimaifa pamoja na kushirikiana na makampuni ya kimataifa.

Nimejaribu tasnia kadhaa ambazo zilisemekana zinaweza kukupa network au mafanikio kama burudani, madini,kilimo, teknolojia na siasa.

Nilikua very strategically mwenye hasira ya mafanikio bila uoga, kwa waganga nikaenda, mashekhe na manabii.

Sasa nikiwa nimevuka zaid ya nusu ya umri wa kustaafu nahisi uwezo wa kufikiria, ndoto na mikakati sina tena kutokana na kutofanikiwa kwa jambo lolote lile nililo invest na kusifiwa na watu wakubwa na mashughuli kwa nilio wafahamu...

Nimekua nikiulizwa na watu niliokua nao wakafanikiwa kufikia malengo yao kwamba kwann mimi sijatoboa ?? Nakosa majibu kabisaa naduwaa

So now naona maisha yangu yapo autopilot naishi maisha yatakavyo na si nitakavyo kwasababu naona nikiweka mikakati isipotokea basi ikitimia inakuja na changamoto kubwa hata siwezi dumu katika hayo mafanikio...

Natamani kurudi kwenye fomu kua na ndoto, ambition na hasira za kupanga na kupambana kutoboa, je nitumie mbinu gani kurudisha matumaini mapya ya mafanikio????
 
Baba J relax, relax, relaxx.....

Plan na uplan vitu vilivyo ndani ya uwezo, usipange mambo makuuuubwa kiasi kwamba yanakutia ugumu na uvivu kuyatekeleza. Amka fanya.....

Maisha ni LEO
Kwa level nilifikaga alafu niishi kwa uwezo wangu sasa nna weza nikafa kwa kushangawa aiseeh 😔😔😔
 
For the kids?

Wewe mara ngapi umewakumbuka wazazi wako kwa yale mapenzi waliyokuonesha ukiwa mdogo na wanayoendelea kukuonesha Sasa ukiwa mtu mzima?
Na wasio na watoto sijui wa fight for whom??? Jamaa ajitafakari saana
 
Ondoa waumini wa mwamposa uone utakavyoshuhudia anguko lake.

Sema niweke utani pembeni😂 mafanikio ni bahati bwana, hakuna njia ya kuyafafanua.

Ukichapa kazi unaongeza uwezekano wa kupata bahati ila uhakika wa 100% haupo
Mwana wee acha utajiri ni bahati tuu na si ujanja wala akili... nakumbuka nikiwa nimemaliza form six niliaanda maandiko mawili ya miradi tofauti wasomi wenye masters hawakukubalu kama niliaandaa mimi ni vile mimi mwenyewe ndiye nilifanya presentation.... kuna dogo sasa yupo karibu na kina Elon mask ni kimasiara tuu fomula ya biashara kwenye teknolojia yake nilimpa mimi....

Mpaka nahisi sijui nimerogwa maana kila ninayeshirikiana nae lazima atoboe na kuniacha down downfall 😪😪😪
 
Pole mkuu usichikijua Mungu anaamua nature ya maisha ya mtu ww tafuta ugali ili usije kufa njaaa.....

Siku ukijua siri ya maisha hutaangaaika na mavitu makubwa makubwa relax brooo chilling......njoo tule sugura a.k.a smart baleke
 
Smart baleke sio mwanangu. Ilikua niingie huko ila baada ya kuona wana wanalala mtaroni nikasema stoooooop ntakunywa maji tuu
 
Katika maisha kuna ups and down, ulipofeli ilikua ni lesson.....simama anza tena na nguvu mpya. Usikate tamaa mkuu
Zile nguvu za kusimama tena ndo natafuta sijui ntazipata wapi, kwasababu naogopa mipango saana maana naona ka najitia nuksi nikiwa na mipango
 
Mwana wee acha utajiri ni bahati tuu na si ujanja wala akili... nakumbuka nikiwa nimemaliza form six niliaanda maandiko mawili ya miradi tofauti wasomi wenye masters hawakukubalu kama niliaandaa mimi ni vile mimi mwenyewe ndiye nilifanya presentation.... kuna dogo sasa yupo karibu na kina Elon mask ni kimasiara tuu fomula ya biashara kwenye teknolojia yake nilimpa mimi....

Mpaka nahisi sijui nimerogwa maana kila ninayeshirikiana nae lazima atoboe na kuniacha down downfall 😪😪😪
Ondoa hayo mawazo, kwa imani yako amini siku yako ipo.....
 
Smart baleke sio mwanangu. Ilikua niingie huko ila baada ya kuona wana wanalala mtaroni nikasema stoooooop ntakunywa maji tuu
Ukiona chuma imeingia mtaroni iyoo ajari tuu ila asubuhi akiipeleka gereji akaipa supu na chapati mbili ngoma inarudi mzigoni broo...
 
Back
Top Bottom