Jinsi ya kupangalia chumba cha kulala kiwe na mvuto zaidi


Sijasema kuwa sia kazi nzuri. Ila nimesema hivyo kwa sababu tulikuwa hatufanyi hizo kazi kwa ajili ya kujipatia kipato bali tulikuwa tunafanya just for fun.
 
Young Master wewe hujaoa na huna watoto.

Unadhania unaweza kuweka hizo white ukiwa na watoto wadogo? Umetandika tu anakuja spidi kutoka nje na anarukia kitanda na kurukaruka hapo juu.

Unaishiwa nguvu lakini unabaki kukataza na kuangalia tu na hasa ukiona katoto kanavofurahia basi unamezea.

Hiyo ndiyo real life hata ukijifanya mzungu vipi.
 

Sasa li-tshirt nililopigilia saa hizo si la kwako? Bado halitakuvutia?

In short, hiki ni kipengele ambacho wengi wetu tunakipotezea!
 

Sasa hapo ndipo unapoona umhimu wa kuwatengea watoto chumba chao. Kwani wazungu inamaana hawana watoto ndio maana ni wasafi? Kwa nini sisi tushindwe?
 
Sasa li-tshirt nililopigilia saa hizo si la kwako? Bado halitakuvutia?

In short, hiki ni kipengele ambacho wengi wetu tunakipotezea!

Sasa hapo inategemea na wakati na mazingira. Mimi huwa napendelea au nashauri zaidi watu kuvaa nguo za wapenzi wao hasa pale wanapowamisi kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza zaidi mapenzi kwa kuonyesha ni jinsi gani unampenda na jinsi gani ulivyo muhimu katika maisha yake.

Haitopendeza wala kuvutia endapo kila siku nitakukuta ukiwa umevaa t-shirt yangu tu. Mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine hivyo yanahitaji ubunifu kama zilivyo sanaa nyingine ili kutokusababisha kuchokana haraka hali inayopelekea wengi wetu kutoka nje ya ndoa kwa kuwa penzi lenu lililokuwa na mvuto hapo zamani sasa limekosa mvuto.
 
...YM haya majambo.....
Ni kweli kabisa mabinti humzimika mwanaume wanapokuta geto limepangika...anaishia kuaga hata mara 10 lakin haondoki...
 
Sasa hapo ndipo unapoona umhimu wa kuwatengea watoto chumba chao. Kwani wazungu inamaana hawana watoto ndio maana ni wasafi? Kwa nini sisi tushindwe?

Na kwa wale tunaoishi chumba kimoja na kila kitu tunahifadhi humohumo.....bado na katoto kanaingiza mchanga mpaka ndani kitandani?
 
Na kwa wale tunaoishi chumba kimoja na kila kitu tunahifadhi humohumo.....bado na katoto kanaingiza mchanga mpaka ndani kitandani?

Kama uwezo wenu unawaruhusu kuwa na chumba kimoja basi hilo si tatizo kwani cha muhimu hapo ni chumba chako ni kuonekana kisafi na nadhifu wakati wote. Mnapaswa kumfunza mtoto wenu awe msafi na awe anaheshimu chumba na sio kuingiza ingiza mchanga chumbani hivyo kama chooni.

Pia pamoja na kwamba mnakaa chumba kimoja bado unapaswa kuhakikisha kila kitu kilichomo humo chumbani kinapangwa vizuri ili kukiweka chumba katika hali nadhifu na ya kuvutia na sio kuacha vitu shagalabagala eti kwa sababu uko chumba kimoja.
 
Najua asilimia kubwa ya Watanzania hapa nchini wanaishi kwenye Nyumba za kawaida, nyingi zinakuwa na vyumba kuanzia 2 - 4, pia vyumba hivyo vinakuwa ni vidogo kwa maana kwamba havitoshelezi mahitaji yetu. Watu wengi sana wanatamani kuweka vitu vizuri katika nyumba zao lakini wanakosa nafasi.

Sasa leo nakuletea picha ambazo zinaweza kukusaidia kupangilia vitu vingi katika chumba kidogo.

*Nyumba nyingi zinakuwa na muhonekano kama huu;





*Tuanzie sebuleni..




- Sebule nyingi kama unavyoziona zinaonekana zina mashelf mengi, hii ni kwa sababu ya kuweka vitu vidogo vidogo kama vile vitabu na viurembo vingine pia hata glass za wine na whisky.

*Pia kama sebule yako ni ndogo zaidi, unaweza tumia coffee table zenye drawers kama hizi;




*Kwa upande wa chumba cha kulala unaweza pangilia chumba chako namna hii;
Hii inawafaa sana wanandoa au couples.

Kwa upande wa wanafunzi au wafanyakazi wa ofisini unaweza pangilia hivi;



Pia kama chumbani kwako hakuna nafasi ya kutosha kuweza kuweka kabati la nguo, jaribu kununua kitanda chenye drawers ili uweze kuweka mashuka, blanketi na baadhi ya nguo zako hata vitabu.





*Kwa upande wa toilet and bathroom unaweza iga hii hapa;

Kama unavyoona mabafu mengi yameungana na choo, pia kuna drawers chache kwa ajili ya kuhifadhi mataulo.
 
Nataka ramani kama hizi , Nina kiwanja kidogo nataka nijenge kwa mfumo wa L au T
 
Sawa mkuu ila ajitahidi kukuza nyumba badala ya kubanana kwenye nyumba ndogo hivyo
Kumbuka kuwa maisha hubadirika, unaweza anza maisha na kipato kidogo lakini baadae kipato kikakua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…