Jinsi ya kupata kazi za remote katika mashirika ya kimataifa yaliyo nje

Jinsi ya kupata kazi za remote katika mashirika ya kimataifa yaliyo nje

Leo ningependa kuzungumzia namna kijana yoyote wa Kitanzania ambae una utaalamu na/au ujuzi katika eneo fulani unavyoweza kupata kazi katika mashirika na makampuni ya kimataifa yaliyopo popote duniani na kuweza kufanya kazi remotely ukiwa hapa hapa nchini...

Naongezea kidogo, ili kupata kazi kwa urahisi kupitia linkedin hakikisha ume-verify account yako.

Kwa passport ya kusafiria inatosha kabisa (kuverify ni BURE), ukishaverify content yoyote utakayopost itawafikia watu wengi zaidi.

Kingine jiunge ma-group ya watu ambao mna interest moja eg. Digital marketing group ,inasaidia kutengeneza connection zaidi.
 
Naongezea kidogo, ili kupata kazi kwa urahisi kupitia linkedin hakikisha ume-verify account yako.

Kwa passport ya kusafiria inatosha kabisa (kuverify ni BURE), ukishaverify content yoyote utakayopost itawafikia watu wengi zaidi.

Kingine jiunge ma-group ya watu ambao mna interest moja eg. Digital marketing group ,inasaidia kutengeneza connection zaidi.
Shukrani sana mkuu kwa nyongeza kuntu hiyo!
 
Shukrani sana mkuu kwa nyongeza kuntu hiyo!


Mkuu ukitoa kazi zinazohusu mambo ya IT au computer

Je naweza kupata hizo kazi za remote Kama Therapist au psychologist ? Au mentor .

Naomba kupata insight hapo mkuu.

Nimekuwa nikifanya kazi ya therapist huku Tanzania na Kama consultant kwenye mambo ya mentorship mainly in personal growth .

Hivyo naomba unipe hints ukitoa kazi za computer je upande wa Afya ya Akili soko lake lipoje.

🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Leo ningependa kuzungumzia namna kijana yoyote wa Kitanzania ambae una utaalamu na/au ujuzi katika eneo fulani unavyoweza kupata kazi katika mashirika na makampuni ya kimataifa yaliyopo popote duniani na kuweza kufanya kazi remotely ukiwa hapa hapa nchini. Kwa mfano mimi nafanya kazi katika mradi wa kimataifa; makao makuu yao yako USA, lakini mimi nafanyia hapa hapa bongo. Kupata hii nafasi nilishindana na watu kutoka ataifa mbalimbali kama vile USA, Ehtiopia, Nigeria, na Kenya. Nilifanya raundi tano, nakumbuka hadi raundi ya mwisho tulibaki mimi na jamaa mwingine wa kutoka Ethiopia. Hivyo, inawezekana kabisa hata wewe kijana wa Kitanzania ukapata kazi za namna hii, you just have to be competent, and know where to look. Kufanya kazi remote kuna faida kubwa sana, kwani ukiacha kutokua na mizunguko ya kwenye magari/daladala kila siku asubuhi na jioni, pia unakua unalipwa kwa dola za Kimarekani, wakati wewe matumizi unafanya kwa pesa za madafu (Tshs), hakuna kitu kizuri kama kulipwa kwa $$ halafu unafanya matumiz kwa Tshs.

Nitaongelea kila kitu hapa hapa jukwaani, yeyote mwenye swali aliweke hapa hapa, nitalijibu hapa hapa, nitamaliza kila kitu kwenye uzi huu huu, hakuna cha PM wala wapi.
NItaongelea platforms ambazo unaweza pata kazi hizi, pamoja na nini ufanye ili uweze kuji position na kuwa competitive katika kupata hizi kazi.

Kitu cha kwanza kabisa ambacho ni muhimu kuliko vyote, lazima uwe VIZURI SANA kwenye kazi yako, yaani you have to be one of the best...!! Uwe COMPETENT kweli kweli, maana hizi nafasi unakwenda kushindana na mashine kutoka Nigeria huko, Kenya, USA, na kadhalika...! Na hao watu wako nondo kweli kweli, they do not joke, so na wewe inabidi uwe level hizo za hali ya juu! Ukienda kichwa kichwa, hata ukifanikiwa kuitwa interview utambwela balaa hadi utajiona bonge la kilaza!

1. Andaa resume yako na iwe imenyooka, iwe katika mfumo ambao ni very competitive. Kuna tools nyingi sana za kuandaa resume yako na kuifanya competitive. Kwa mfano, Canva:https://www.canva.com/resumes/templates/professional/; Novoresume, Free Resume Templates for 2024 [Download Now]
Ni muhimu sana uandae resume yako iwe ya kibabe kabisa, sio unaandaaa resume ya kichovu, hutafika popote katika competition ya kimataifa.

2. Hakikisha unakua na a very STRONG ONLINE PRESENCE: Unataka kufanya kazi remote na mashirika ya kimataifa halafu hata hauijui LinkedIn? Bro, are you serious? Kama hauna account LinkedIn, baada tu ya kusoma hii post, kitu cha kwanza unatakiwa kufanya haraka sana ni kwenda LinkedIn, kujisajili kule na kuhakikisha una profile very strong (5 star profile), baada ya hapo hakikisha unaomba connection na watu walio katika industry yako una connect nao as many as possible. Kisha, mdogo mdogo anza kupost masuala yanayohusiana na kazi yako au vitu unavyovifanya. Are you a tech wizard and you are working to solve a challenge through technology? Why not post what you are doing there? Are you employed somewhere and today you had a workshop with some stakeholders to discuss on something? Why not share over LinkedIn with some nice photos? Pamoja na LinkedIn, pia kuna platform zaingine kulingana na industry yako, mfano watu wa tech wana zile platform zao ambazo zinakua na communities, wana discuss ma solution, na ma code; wewe ni programer, kwa nini usijiunge huko?
Niwaambie kitu, hii kazi yangu niliyoipata, mimi hata sikuiomba, I was just contacted on LinkedIn na mtu ambae yupo huko, akaniambia kuna nafasi huku nilipo naona inakufaa sana based on what you have been sharing here on LinkedIn, akaniambia kama nipo interested aniunganishe na recruiter wao, ikawa imeisha hiyo.

3. Ongeza zaidi ujuzi wako:
Sawa, umemaliza degree ya Information, Communication, and Technology hapo UDSM; Lakini je, una nini cha ziada? Kuna platforms kama Coursera, Udacity wanatoa courses fupi fupi katika maeneo tofauti tofauti- Zipo za bure na za kulipia, anza na zile za bure angalia ipi itakuongezea kitu, zipige nyingi nyingi.... Ukijipanga pia ukapiga hata na zile za kulipia kwa kutoboka kidogo mfuko sio mbaya, YES. Kama unaweza kutoa hadi shilingi 150,000 - 200,000 kugharamia kumgonga demu why not usitumie gharama inayokaribiana na hiyo kujiongezea ujuzi na skills ambazo zitakusaidia pia? Pia, usisahau YOUTUBE kuna madini ya kutosha kule, bure kabisa. Badala ya kupoteza bundle lako kuangalia umbea wa insta, ingia kule ucheki madini ujiongezee SKILLS. Niwaambie tu, dunia ya sasa hivi skills na ujuzi wako ni muhimu sana sana, usije ukaingia kwenye mtego wa kukusanya vyeti huku huna unacho-gain...!! Mimi hadi nimepata hii kazi ya remote, hawajawahi kuniambia hebu tuone vyeti vyako hata mara moja..!! Kwa hiyo zingatia sana katika kuongeza ujuzi na skills zako, vyeti viwe ushahidi tu.

4. CONNECTION
Usijifungie tu chumbani kwako, connect na ongea na watu mbalimbali kwenye industry yako hasa walio katika nafasi za juu kimaamuzi na wale waliokuzidi uzoefu. Hkikisha wanajua ujuzi na skills zako na what you can bring on the table. Hii ianzie kote kuanzia kwenye mtandao, ndio maana kwenye point namba 2 nikaongelea presence yako kwenye mitandao kama LinkedIn, ukiwa kule unaweza ku connect na watu walio katika industry yako na wakiangalia posts zako na profile yako wanajua kuwa huyu ana skills hizi na zile. Pia, vile vile offline hudhuria zile events zinazohusiana na sekta yako na hakikisha unaongea na wale watu waliokuzidi na kubadilishana nao mawazo.. Ni rahisi mtu kukupa referral namna hiyo, kama ambavyo ilinitokea mimi alienipa referral alifanya hivyo kutokana na kuona posts zangu na profile yangu LinkedIn.

5. Platform unazoweza kupata remote jobs: Hapa chini nitapost link za platforms ambazo unaweza pata hizi kazi za remote zile ambazo nazifahamu. Wadau wengine wanaweza kuongezea links zaidi.
Jobgether is the Largest Remote Job Platform worldwide with more than 160k remote jobs available across the world.

Karibuni kwa yoyote mwenye swali au anaetaka kujua zaidi kuhusu chochote, nipo hapa, maswali yote yaulizwe hapa na nitajibu kila kitu hapa hapa sebuleni!!

DA HUSTLA karena
Stv Mkn
Mambo vipi mkuu, mimi ni education pro. Ni mwalimu by profession na pia nimewai fanya miradi ya elimu na kuandika Swahili articles za elimu, pia vitabu. Nina account ipo linked in nimejitahidi kufanya optimization lakini sijawai pata any contact ya mtu au shirika likiwa interested na mimi. Unaweza nishauri nifanye nini kuvutia recruiters wa mtandaoni? Na je hizo remote jobs mpaka sisi watu wenye background ya NGO zinakuwepo au ni IT jobs pekee?
 
My daily routine revolves around kutoa support katika nchi ambazo mradi unakua implemented kwenye issues za data pamoja na reporting of indicators. Kwa mfano leo I was working on an annual report ya mwaka jana, na pia nilikua na virtual meeting na our team in Nigeria kutoa technical support kwa issues zao za data, kuna data zao zilikua na discrepancies kidogo, so niliziflag ili waweze kuziangalia na kuaddress.
Morning_star
Data Officer nipo hapa kama watahitajika Mkuu.
 
Mfano huyu anayeongelea anataka kazi remote alafu zinakuja kazi za udereva.., Huoni hapo next step ni kuombwa pesa za kukamilisha Viza na Work Permit au Safari ya kwenda US for interview
Linkedin inatabia ya kutuma email alerts kwa kazi zinazoendana na skills na professional yako hata kama haziko eneo lako. So yeye ni driver, wakati mwingine atapokea alerts za kazi za drivers hata wa nchi nyingine. Mimi nilishawahi pokea alert ya kazi inahusiana kampuni ya Tiktok tukazungumza vizuri na recruiter only kuja kugundua kuwa siko Ireland niko TZ na hiyo kazi ilikuwa inahitaji niwepo physically japo ilikuwa inahusu mtu ambaye anazungumza Kiswahili kwa ajili ya kufilter content za Kiswahili
 
Screenshot_2024-04-19-07-29-25-348_com.linkedin.android.jpg

Nimejaribu kuverify account yangu linkedin nimekwamia hapa.
Anyone who can help me on how to enable NFC?
 
Mkuu asante kwa moyo wako wa ukarimu!
Jambo usilolijua! Mimi nina account linkedin,nimekuwa nikiitiwa kujaribu jobs mbali mbali kulingana na professional yangu lakini nimekuwa nikipuuza kabisa! Nimekuwa nikionyeshwa connections mbali mbali lakini kwa kutojua nimekuwa nikipuuza kabisa.
Mkuu nashukuru nitalifanyia kazi nione impact yake ikoje!
 
Mambo vipi mkuu, mimi ni education pro. Ni mwalimu by profession na pia nimewai fanya miradi ya elimu na kuandika Swahili articles za elimu, pia vitabu. Nina account ipo linked in nimejitahidi kufanya optimization lakini sijawai pata any contact ya mtu au shirika likiwa interested na mimi. Unaweza nishauri nifanye nini kuvutia recruiters wa mtandaoni? Na je hizo remote jobs mpaka sisi watu wenye background ya NGO zinakuwepo au ni IT jobs pekee?
Kuhusu cha kufanya kuvutia recruiters kwenye LinkedIn account yako:
-Post ukiongelea kuhusu kazi zako, post consistently... Zisipite siku 2 hujapost kule kuhusiana na kazi zako. Umesema wewe ni writer, umeandika arricles na vitabu mbalimbali. Je, umewahi kupost LinkedIn kuhusu articles zako? Kuelezea what you wrote, why is it important, what is it adding, etc?
Pia, unaweza kuinclude some photos labda ukiwa kwenye mkutano unaongea na watu, au unasikiliza muongeaji, then ukaandika kuhusu huo mkutano, ulikua ni wa kitu gani, na wewe umejifunza nini. Ukipost CONSISTENTLY, itafika muda people will start noticing you, na recruiters wataanza kukufuata.
Pia, kitu kingine unaweza fanya ni kuongeza RELEVANT connections-Mfano your fellow teachers & writers around the world- Check profiles, ukuona profile za watu wanaofanya kama unachofanya wewe, waombe u connect nao-Unavyp,idi ku grow your connections kwa watu wa field yako LinkedIn, unaongeza chances za wewe kuwa found na recruiter wa hiyo sector.
Issue ya pili, kwa vile umesema una ujuzi wa kuandika pia-Kwenye remote platforms kuna kazi nyingi sana kwa ajili ya watu wanaoweza kuandika (angalia mfano in the attached screenshot)-Hivyo unaweza kuomba kazi za mlengo huo wa mambo ya kuandika andika na content creation.
Samahani sana kwa kuchelewa kukujibu mkuu.
Digital Ticha
 

Attachments

  • Screenshot_2024-05-20-00-16-08-176_com.android.chrome.jpg
    Screenshot_2024-05-20-00-16-08-176_com.android.chrome.jpg
    468.8 KB · Views: 10
Mkuu asante kwa moyo wako wa ukarimu!
Jambo usilolijua! Mimi nina account linkedin,nimekuwa nikiitiwa kujaribu jobs mbali mbali kulingana na professional yangu lakini nimekuwa nikipuuza kabisa! Nimekuwa nikionyeshwa connections mbali mbali lakini kwa kutojua nimekuwa nikipuuza kabisa.
Mkuu nashukuru nitalifanyia kazi nione impact yake ikoje!
Karibu mkuu!
 
Linkedin inatabia ya kutuma email alerts kwa kazi zinazoendana na skills na professional yako hata kama haziko eneo lako. So yeye ni driver, wakati mwingine atapokea alerts za kazi za drivers hata wa nchi nyingine. Mimi nilishawahi pokea alert ya kazi inahusiana kampuni ya Tiktok tukazungumza vizuri na recruiter only kuja kugundua kuwa siko Ireland niko TZ na hiyo kazi ilikuwa inahitaji niwepo physically japo ilikuwa inahusu mtu ambaye anazungumza Kiswahili kwa ajili ya kufilter content za Kiswahili
Yes, ni kweli kabisa, imewahi nitokea pia mara kadhaa.
 
Back
Top Bottom