Majibu yamekuja kutokana na vile umeuliza swali lako Mkuu. Sio vibaya kuwa na urafiki na watu wa mataifa mengine ila sasa umeuliza kimhemko sana hadi imetia shaka.
Ila ukitaka kutengeneza huo urafiki, sogea mahali wahusika wapo kwa wingi. Alafu usiwe na shobo nao. Kingine epuka kutaka urafiki kwa kukutana bara barani huwa haudumu na wengi wanaukwepa.
Tembelea sana coffee bars na hoteli za kitalii pia matukio yanayowahusisha mfano Kili Marathon hii nenda tena wahi kabisa pale Moshi, week before anza kujichanganya nao.
Urafiki wa maana ni gharama. Lazima uwe na pesa au kitu chakuwanufaisha hao marafiki.