mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Intellijensia.
Angalia documentaries za mauaji historia, ujasusi andaa notice zipangilie njoo tuandikie. Unaweza kwenda mbali kwa kusoma vitabu na maandiko ya watu waliofanyia utafiti wa kina mambo hayo.
MapenzI
Kuwa mtunzi mzuri wa matukio. Soma story za mapenzi jivike uhusika jitwalie utukufu jf.
Siasa.
Hata kama sio ccm au chadema. Chagua upande kama utani. Ponda sana upande mmoja, ikiwezekana weka avatar ya chama hicho. Mwezi mwingi utakuwa umekwisha jitwalia utukufu na sifa zitakazosindikizwa na matusi kemkem. Ila kuwa makini kuna baadhi ya upande unaweza kujikuta adui wa kitaifa.
DINI
Tafuta mijadala, makabrasha ya mabishano ya kidini kwenye mitandao ya kidini huko.
Kuna watu wamewahi kuwa maarufu kwenye jukwaa hilo tata la dini lililoko mafichoni, wao hawajawahi kuongea lolote zaidi ya Copy paste ya maandiko ya wakubwa wao.
UPAGANI NA " Thibitisha Mungu yupo''
Hii ndiyo rahisi kuliko yote. Kuna radio Ulaya na Us lukuki zinatoa maswali elekezi ya jinsi ya kukabiliana na waabudu Mungu wa kweli. Kuna lecture lukuki youtube zitakazokufanya uive katika kutusumbua wacha Mungu, Kuna debate nyingi mno ambazo wacha Mungu wanagaragazana na Watu wa Mungu huku wakitoka kama walivyoanza. Hapa hujasoma vitabu elekezi vyenye nukuu za wazee wa kale wapagani na wanaphilosofia wa kigiriki. Nakuhakikishia ndani ya nusu mwezi utakuwa role model wa vijana wengi mno ambao wanatapatapa hawajui wasimamie lipi katika ulimwengu wa imani.
KIMATAIFA.
Huko unahitaji akili ya ziada, vinginevyo uwe unasoma na kubandikia watu mabandiko ambayo huwezi kutetea. inabidi uwe na mentality ya kimataifa.
ulimbwende, chit chat, udaku, huko sijui wanaishije sina neno.
Unaweza kuongeza na zako.
Sijaandika kwa sababu natafuta umaarufu au nautaka. Nimeandika kwa sababu shida kubwa sana ya waumini wa ulimwengu wa mitandaoni ni kutafuta umaarufu mkubwa kuliko uhalisia wao. Wengi wanaugua ugonjwa mbaya sana aliowahi kuugua kijana mmoja wa kigiriki na ukaitwa kwa jina lake Narcissism.