Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Asante.sasa hizo chapati za nazi zinakuwaje?una maanisha unakandia nazi badala ya maji?
Ndiyo maana yake, hakikisha unapata tuwi zito ndo ukandae unga wa chapati, ili kupata tui zito baada ya kukuna nazi yako ibrendi na maji kidogo katika brenda kwa muda mrefu, kisha kanda unga na chumvi, usikawie papo hapo sukuma chapati na uchome.

Kumbuka chapati iive vizuri mpaka ndani lakini kamwe isiunguwe wala kuonyesha arama yeyote nyeusi. kama utahitaji kula baadaye kidogo zihifadhi katika hotpot.
 
Nitafanya practical soon.Ubarikiwe
 
Chef mkuu, mimi huweka mafuta ya moto sana kwenye unga wenye chumvi. Lakini nahakikisha nimechekecha unga (to add in air) kabla ya kuutumia. Then nachanganya unga na mafuta kwa kutumia vidole tu (inaitwa rub in, to add more air). Nakanda na maji ya uvuguvugu kiasi.

Nikishasukuma mara ya kwanza na kupaka mafuta kidogo, navuta kwa vidole gently kila upande napata mdabwada wenye unene mdogo sana, kisha nakamata kona moja na kukunja kamba (hapa napata layers nyiingi nyembamba kwenye chapati zangu).

Naziacha kama muda wa nusu saa hivi, kisha nasukuma miduara.
ili zisinyonye mafuta mengi, nakausha pande zote kikaangioni, then naweka mafuta kidogo ( nusu ya tea spoon) juu then naipindua. Inakuwa na rangi nzuri sana, laini na inasasambuka haswaa!
 
Nimependa upishi wako na inaelekea chapati zako huwa zinakuwa laini na tamu.Sasa niambie hapo kwenye air naona ni pageni kwangu.Faida za air kwenye chapati ni nini na kisayansi inakuwaje???
 
X-PASTER asante sana for this recipe
nilikuwa sijawahi pika chapati
nimetumia maelekezo yako na chapati zangu za kwanza watu wamezipenda kweli.

once again thanks
 
Last edited by a moderator:

Wifi kuna namna nyingine nilijifunza kupaka mafuta na kusokota kama ukiona kazi sana kufanya moja moja. Unakata donge kubwa kama la chapati 5-10 alafu unalisukuma mpaka liwe lembamba. Ukishapata wembamba unaotaka unapaka mafuta, unasokota kama kawaida alafu unakata vipingili pingili kwa kisu. Sinakua kama umesokota moja moja, kinachobaki kusukuma tu wakati wa kukaanga.

Natamani ningeweka picha ili na wengine wafaidi (haswa wale wasiojua/wanaokwepa kusokota kisa uvivu) sema hichi kimeo changu kinaleta pozz.
 
Last edited by a moderator:
Nimependa upishi wako na inaelekea chapati zako huwa zinakuwa laini na tamu.Sasa niambie hapo kwenye air naona ni pageni kwangu.Faida za air kwenye chapati ni nini na kisayansi inakuwaje???

Kumbuka chapati haiwekwi hamira kama maandazi. Hewa ndio inayoumua na kufanya ngano isigandamane. Na haswa nia ya kusukuma mara mbili ni introduction ya hewa zaidi. Vitu vitatu muhimu vinaongeza hewa: kuchekecha unga, kukanda, na ile kusukuma mara mbili.
 
Aaah, wifi nimekuaminia. This weekend lazma nifanye hii yako. Ila sasa ukishapaka mafuta, kata mistari, then please vuta mdabwada ndo ukunje uone layers zitakavyotoka nyembamba.
Asante kwa kunijuza, faida kweli kuoa vichwa hehehe!
 
Uchaga tu unakusumbua,lol!

Tatizo ni ukandaji kama alivyosema snowhite. Unatakiwa ukishachanganya maji na unga kiasi uanze kukanda from the edges towards the centre. Yaani unakamata donge pembeni unaleta kati, ukizungusha donge ili ukande pande zote.
Pili zingatia joto la maji. Inabidi yawe makali zaidi kidogo kuliko chakula cha mtoto. Namaanisha ukidondoshea nyuma ya kiwiko ustuke kidogo. Chapati za kumimina maji yanatakiwa ya baridi kabisa (mimi hutumia ya kwenye friji)
thanks kwa somo..
kitu gani kinafanya chapati kuwa ngumu?
 
Last edited by a moderator:
Aaah, wifi nimekuaminia. This weekend lazma nifanye hii yako. Ila sasa ukishapaka mafuta, kata mistari, then please vuta mdabwada ndo ukunje uone layers zitakavyotoka nyembamba.
Asante kwa kunijuza, faida kweli kuoa vichwa hehehe!

Naomba nikutembelee week end uwe mwl.wangu
 
Nazipenda kweli chapati...Nafurahi pia kujua kuzitengeneza, wiki haipiti bila kuzipika!! huh
 
Habari jf chefs,ninatatzo moja kila nikipika chapati za kusukuma zinakua ngumu nawakati mwingne znakatikakatika nataman nipike chapati yani ukiiweka mdomoni ufurah mwenyewe.plz nsaidieni nimsuprize huyu shemej yenu weekend hii afu namwekea na rost la maini

=================================================



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…