Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Chapati zinatiwa baking powder?
Niko tayari kwa darasa. Tiririkaaa
 
nataka kujua kupika chapati za kusukuma zenye backing powder mayai na blue bend kuna sehemu nilikula zilikuwa nzuri sana ila sijui kuzipika

Nilidhani ulitaka kutoa darasa lakini kumbe sivyo.
 
daaaaa baking powder na chapati ???
Bibie embu ulizie huko utupe darsa
 
Vipimo.

Unga vikombe 4 vikubwa.
Maziwa vikombe 2 kasorobo.
Chumvi kiasi.
Baking powder 1 tea spoon
Hamira 1 tea spoon
Yai 1
Ufuta kiasi
Samli
Siagi vijiko 2 vya kulia

Namna ya kutaarisha

1)Changanya pamoja unga,maziwa,chumvi,siagi,hamira na baking powder..
2)fanya madonge kama 8 kwa kipimo hicho cha unga
3)sukuma kila donge na upake samli na ukunje kama chapati.
4)ukimaliza kukunja zote 8 then sukuma duara kiasi na uweke kwenye trey ya kuchomea kwenye oven...
5)subiria mpaka iumuke then pakaa yai kwa kutumia brush then nyunyuzia ufuta
6)washa oven moto kiasi hadi iwive
7)pakaa mafuta juu na tayar kwa kuliwa.
 
Attachments

  • 1383987228847.jpg
    1383987228847.jpg
    15.8 KB · Views: 404
Mikate hii alishawahi kuipika dadaangu once nilienjoy kweli...nimefurahi kupata receipe yake farkhina
 
Last edited by a moderator:
You are God sent.
can you believe nilitaka kuulizia recipe ya hii chapati ya ufuta?! Manake kuna mahali nanunua na wamegoma kuniambia. Natengeneza recipes ya line za healthy baking na hii ni nambari wani kwangu.

Muaaah! Asante sana
 
kama mikate ya ufuta ndo chapat za hamira hapa ndo penyewe japo ananikandia kaka yangu maana shughuli kwennye kuukanda ni kubwa sana
 
kama mikate ya ufuta ndo chapat za hamira hapa ndo penyewe japo ananikandia kaka yangu maana shughuli kwennye kuukanda ni kubwa sana
Mikate ya ufuta niijua mie unga wake unaupiga piga unakua wa majiii na haukandwi unachanganya na mkono.
 
You are God sent.
can you believe nilitaka kuulizia recipe ya hii chapati ya ufuta?! Manake kuna mahali nanunua na wamegoma kuniambia. Natengeneza recipes ya line za healthy baking na hii ni nambari wani kwangu.

Muaaah! Asante sana

U welcome shosti.
 
Mhhhh! Ndio mara ya kwanza nasikia chapati za hamira, hongera zako fakhrina, ila kuna chapati za kukanda kwa kutumia samli nazipenda zaidi hizi ukilinganisha na zile za mafuta ya kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom