Jinsi ya kupika Kabichi la nyama

Jinsi ya kupika Kabichi la nyama

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,683
Jamani hii mboga ni nzuri kwa ladha na nzuri kwa afya kwasababu ina nutrients zote za muhimu.

Mahitaji

  • Nyama ya ngombe 1/2 kilo
  • Vitunguu maji viwili
  • Nyanya nne
  • Pilipili hoho nusu
  • Kabichi 1
  • Viazi vinne
  • Karroti 1
  • Njegere nusu kikombe
  • Mafuta vijiko vitatu vya supu
  • Kitunguu saumu
  • Pilipili manga kiasi
Jinsi ya kutayarisha

  1. Kata nyama,osha,weka chumvi,kitunguu saumu na pilipili manga acha chemsha na uikoroge ili viungo vikolee,ongeza maji kuifunika nyama,acha iive
  2. Kata kabichi kama vile unavyokata la kachumbari lioshe na maji ya vuguvugu,Tayarisha kitunguu,nyanya,karoti,viazi vigawe mara mbili.
  3. Injika chungu jikoni,weka mafuta yapate moto,kaanga kitunguu mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi,weka nyanya,viazi,supu ya nyama na nyama uloichemsha,acha nyanya iive mpaka ipondeke.Na mchuzi uwe mzito.
  4. Weka carrot na njegere pamoja na kabichi.Acha viendelee kuiva sosi ya kwenye kabichi ikikaribia kukauka weka pilipili hoho acha vichemke dakika kadhaa kisha epua.
  5. Ongezea chumvi ikiwa haijatosheleza
Msosi huu ni mzuri ukiula na wali wa nazi au chapati.Bon apetitt

20140222_180533.jpg
 
gorgeousmimi samahani kama ntakua nimeingilia upishi wako

Hapo ukiweka na tangawizi ladha inaongezeka alafu ni nzuri sababu kabichi linatia tumbo gesi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
gorgeousmimi samahani kama ntakua nimeingilia upishi wako

Hapo ukiweka na tangawizi ladha inaongezeka alafu ni nzuri sababu kabichi linatia tumbo gesi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Sure....tangawizi inaweza kuwekwa kwenye nyama!
 
Last edited by a moderator:
Asante dada, leo nimepata upishi mpya...mimi nimezoea kulipika la nyama ila huwa siweki viazi na njegere, kwa hiyo ntajaribu hili pishi la kuchanganya na viazi na njegere ....naamini utamu wake HAUSEMEKI...Yam yammm yammm...
 
Yah inakuwa yummy!
 
Back
Top Bottom