Jinsi ya kupika Kabichi la nyama

Jinsi ya kupika Kabichi la nyama

Asante sana, hili limetulia mno, mimi hupenda kwa ugali hii kitu, sjawahi eka njegere na viazi, kumbe yapendeza hivyo ntajaribu mwenzang
 
Mie nimeanza diet kidogo menu za JF jamani mnanitamanisha ,
Nilijifungua nikaongezeka kilo mia mbili kasoro tatu ..yelewii i need my body back:smile-big:

Hahahahah ulikua wala sana nini? Mie nimegain kg 1 tu lol na zile za ujauzito zote zimepungua

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hahahahah ulikua wala sana nini? Mie nimegain kg 1 tu lol na zile za ujauzito zote zimepungua

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

jamani umepunguzaje mpendwa hebu nipe siri ,mie baby ana 9 month now lakini huu uzito hadi najishangaa
 
Jamani hii mboga ni nzuri kwa ladha na nzuri kwa afya kwasababu ina nutrients zote za muhimu.
Mahitaji
  • Nyama ya ngombe 1/2 kilo
  • Vitunguu maji viwili
  • Nyanya nne
  • Pilipili hoho nusu
  • Kabichi 1
  • Viazi vinne
  • Karroti 1
  • Njegere nusu kikombe
  • Mafuta vijiko vitatu vya supu
  • Kitunguu saumu
  • Pilipili manga kiasi
Jinsi ya kutayarisha
  1. Kata nyama,osha,weka chumvi,kitunguu saumu na pilipili manga acha chemsha na uikoroge ili viungo vikolee,ongeza maji kuifunika nyama,acha iive
  2. Kata kabichi kama vile unavyokata la kachumbari lioshe na maji ya vuguvugu,Tayarisha kitunguu,nyanya,karoti,viazi vigawe mara mbili.
  3. Injika chungu jikoni,weka mafuta yapate moto,kaanga kitunguu mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi,weka nyanya,viazi,supu ya nyama na nyama uloichemsha,acha nyanya iive mpaka ipondeke.Na mchuzi uwe mzito.
  4. Weka carrot na njegere pamoja na kabichi.Acha viendelee kuiva sosi ya kwenye kabichi ikikaribia kukauka weka pilipili hoho acha vichemke dakika kadhaa kisha epua.
  5. Ongezea chumvi ikiwa haijatosheleza
Msosi huu ni mzuri ukiula na wali wa nazi au chapati.Bon apetitt
View attachment 161961

ntapika agosti
 
Ulikuwa unakula nini mamito!?

nilipojifungua ukoo mzima ulihamia home kwangu aubuhi Uji wa Ulezi kwa lazima
saa nne mtori ,saa nane supu ya samaki au kuku yaani my mother alikuwa busy kunilazimisha..sina hamu
Nipeni tu diet gani nzuri itayonisaidia na mtoto aendelee kupata maziwa yake,,
Kingine huyo mtoto ananyonya usiku kucha kula yeye ni kumkamata mdomo na ukizubaa anatema chote:smile-big:
 
Jana nimepikia family Pishi hili ,ni tamu sana family walienjoy na Wali wa Nazi

thanks Gorgeusmimi
 
Last edited by a moderator:
hili pishi limekaa poa sana, ngoja nilishushe mchana, vipi kalimao ukiweka kidogo itakuwaje?? au ndo kuharibu ladha farkhina
 
Last edited by a moderator:
yaani itabidi nikapike hichi chakula nione test yake ikoje asante kwa pishi lako bestito
 
Back
Top Bottom