Jinsi ya kupika makande

Waungwana,

Nina hamu na makande na ninataka kuyapika.

Je niweke vitu gani ili msosi unoge? Pia, maharagwe na mahindi nayaweka pamoja au nasubirisha kuweka maharagwe?
Weka njugu na karanga au korosho.
 
Weka cement mkuu upate kitu pouwa kabisa
 
Jee inajuwa jinsi ya kupika makande?

Makande ni chakula cha mchanganyiko wa mahindi na maharage pamoja na vikorombwezo vingine kama vile vitunguu,karoti,hoho muda mwingine hata nyanya unaweza kuweka.
Katika mapishi ya makande unaweza kuunga kwa kutumia mafuta au ukaweka hata nazi.

Hivi ndivyo jinsi ya kupika makande ya nazi,karibuni sana

Mimi huwa nayapenda ya Nazi
na Hiriki...

Mahitaji:

*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa
*Kitunguu maji
*mafuta ya kupikia kiasi
*Karoti (ukipenda)
*Hiriki
*chumvi kiasi

Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni

Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata... Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo

Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja

Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja... Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa... Mimi huyaweka na sukari pia ... Hebu jaribu kumtagi na mwenzio aje naye ajuwe ni namna gani ya kupika makande.
 
Jamani kuna watu wanaweza kupika makande, yaani wee acha tu
 
Hiriki = hiliki. Makande ukiweka nyanya unaharibu
 
Asante sana! Makande matamu jamani, haswa yakiata mpishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…