Jee inajuwa jinsi ya kupika makande?
Makande ni chakula cha mchanganyiko wa mahindi na maharage pamoja na vikorombwezo vingine kama vile vitunguu,karoti,hoho muda mwingine hata nyanya unaweza kuweka.
Katika mapishi ya makande unaweza kuunga kwa kutumia mafuta au ukaweka hata nazi.
Hivi ndivyo jinsi ya kupika makande ya nazi,karibuni sana
Mimi huwa nayapenda ya Nazi
na Hiriki...
Mahitaji:
*Nazi (kubwa) yakikolea Nazi yananoga sanaaa
*Kitunguu maji
*mafuta ya kupikia kiasi
*Karoti (ukipenda)
*Hiriki
View attachment 477880*chumvi kiasi
Baada ya kuchemsha makande yako na kuiva vizuri, yaepue yaweke pembeni
Bandika sufuria jikoni, tia mafuta ya kupikia kiasi, yakipata moto tia vitunguu ulivyovikatakata... Kaanga vitunguu, vikianza kuwa brown tia karoti ulizokata katika shape uipendayo
Vikishachanganyika mimina makande ulochemsha tia na hiriki uchanganye pamoja
Kisha weka tui la pili la Nazi, na chumvi, koroga tui lichanganyike na makande, acha vichemke pamoja... Kisha weka tui zito, koroga vizuri, vikishachemka na kuchanganyika vizuri epua...Makande yako tayari kwa kuliwa... Mimi huyaweka na sukari pia ... Hebu jaribu kumtagi na mwenzio aje naye ajuwe ni namna gani ya kupika makande.