Jinsi ya kupika ndizi nyama za nazi

Jinsi ya kupika ndizi nyama za nazi

Nafikir mna Weeknd nzuri sana nduguzangu
Leo tupike ndiz nyama za Nazi
Mahitaji
Ndizi mbichi mzuzu
Kitunguu nyanya moja(Huwa haipendez kutumia nyanya nyingi)
Karot na hoho
Nyama iliyochomshwa(usisahau kuchemsha na viungo kitunguu swaumu tangawiz na currypowder)

Nazi unaweza tumia ya pakt au ya kawaida

Hatua ya kwanza
Andaa mahitaji menya ndiz kata utakavyopenda saga nyanya,kwangua karot,kata vitunguu size upendayo
Chuja Nazi tui zito kama ya pakti acha kma ilivo
Hatua ya pili
Weka sufuria jikoni weka mafuta kidogo sana sababu tunatumia Nazi
Yakipata moto kaanga kitunguu kikilainika weka karot kaanga kidogo Kisha weka nyanya acha ziive kidogo

Zikiiva weka ndizi weka na chumvi Kwa ajili ya ladha changanya ndiz zako na nyanya vizuri Kisha weka nyama koroga pia acha zichemche pamoja na mchuz wa nyama kma mchuz ni kidogo ongeza maji au Nazi tui la jepes acha zichemke

Hatua ya Tatu
Zikiiva weka hoho kata size upendayo huleta harufu nzuri
Kisha weka Nazi changanya Kwa kuzungungusha sufuria kama unatumia mwiko koroga taratibu
Acha ziive baada ya dakika 5 zitakuwa tayari Kwa kuliwaView attachment 3136337View attachment 3136339View attachment 3136340
Nimeangalia hizi picha,njaa imeanza kuniuma ghafla...
 
Ndizi nyama....
Namba moja kwenye orodha ya vyakula vyangu pendwa😋
 
Nanunua vikontena tu navisambaza. Kimoja kwako, kingine kwa Evelyn Salt kingine kwa Makiwendo yaani nabakia na kazi ya kupasha tu.
Yaani utaenjoy sana
Ungekaa karibu na kwangu nimekwambia uviache kwangu kumi maana npikaga naanza kuita jirani tuje kula nisingepat tabu kabisa
 
Yaani utaenjoy sana
Ungekaa karibu na kwangu nimekwambia uviache kwangu kumi maana npikaga naanza kuita jirani tuje kula nisingepat tabu kabisa
Uko wapi? Niko tayari kuhamia karibu na wewe🤗🤗
 
Back
Top Bottom