Jinsi ya Kupika Vitumbua Vitamu kwa kutumia muda mchache

Jinsi ya Kupika Vitumbua Vitamu kwa kutumia muda mchache

Vitumbua ni aina nyingine ya Chakula kinachopendwa zaidi katika maeneo mbalimbali nchini.


Vitumbua vina aina mbalimbali ya Mapishi, kuna Vitumbua vya Nazi, Mayai, Nyama na aina nyinginezo.

Vifaa vya kupikia vinapatikana Sokoni kwa Gharama nafuu inategemea na ukubwa unaoutaka.

Ni vizuri kupika nyumbani kuliko kununua, kwani usalama wake ni wa uhakika zaidi.

Ni rahisi kuandaa na kupikia pia.

Mahitaji.

Unga wa Mchele Nusu/ Kilomoja.

Unga wa Ngano Kidogo.

Tui la Nazi (Sio Lazima)

Maji ya Uvugu vugu.

Hiriki.

Sukari.

Mafuta ya Kuchomea.

Kikaangio cha Vitumbua



Jinsi ya Kuandaa.

Changanya Mchanganyiko wako Vizuri kabisa usiwe mlaini sana Wala Mzito sana.
Hakikisha kila kitu umeweka katika Vipimo sahihi ili Vitumbua vyako viwe vitamu sana.
Baada ya Kuchanganya acha Mchanganyiko wako kwa muda wa Nusu saa au Saa nzima ili uumuke vizuri. Na muda huu ni kulingana na hali ya hewa ya sehemu ulipo.

Utaweka kikaangio chako kwenye Moto hadi kipate Moto kidogo kisha weka mafuta kidogo yakichemka vizuri Chota Unga wako na kuweka kidogo kigogo.

Pika hadi Vitumbua vigeuke rangi na kuwa vya kahawia. Kisha toa kwenye kikaangio.

Vitumbua huliwa wakati wote na Chai, Soda,Juice na kahawa.

View attachment 3091000
Mashallah 😍 😍 😋😋😋😋 hiki ukikiminya mafuta mengi 😎😎😎 Raha hizi vitumbua Vitamu sana upate chai yenye mchai chai iliyo na karafuu mashallah 😎 😋😋
 
Back
Top Bottom