fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Kwakuwa kipato changu hakiniruhusu kununua maji ya kunywa, nimechukua hatua zifuatazo:
1. Kununua water dispenser na chupa zake 2, nikiweka chupa moja ya pili inabaki kuwa spea.
Pia nimenunua water boiler ya lita 30, hivyo nachemsha maji, nayachuja na kitambaa kisafi cha nailoni, yakipoa nayaweka kwenye chupa ya dispenser.
Shida nayopata hapa ni namna ya kuchuja uchafu maana haya maji ya bomba huwa yana uchafu, japo nachemsha kuua wadudu, nachuja na kitambaa, bado uchafu unakuwepo.
2. Kifaa cha kusafisha maji. Nimenunua kifaa fulani made in India ambacho chenyewe kinasafisha maji na kuua wadudu, ambacho kila baada ya wiki 2 nasafisha ule utumbo wa ndani unaosafisha maji na kila baada ya miezi 6 nanunua utumbo mpya. Kwa njia hizo nimedhibiti matumizi ya kununua maji, japo kuna kazi ya kuosha chupa za water dispenser kutoa uchafu ambao hubaki na kung'ang'ania kwenye chupa kwa ndani.
Wadau kama mna njia bora zaidi ya hizi, mchangie hapa