Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Unapoachwa na mtu umpendaye inauma.
Hasa ukifikiria kwamba huyo mtu mlikua mnaendana sana. Mlikua mnaelewana.
Mawazo huwa ni mengi, lakini kitu kinachotokea ni kwamba unajikuta huwezi waza kitu kingine zaidi ya mawazo ya kuachwa.
Kila ukiwaza unaumia.
Unaona mambo ni mabaya kila sehemu, hupati unafuu.
Huoni mwanga wa kupata mwingine mtu mwingine kama yeye.
Yani mawazo yanayokujia kichwani hayakupi ahueni/ amani hata kidogo.
Apo unakua umeshikamana/ umejifunga na mawazo yasiyokusaidia.
Njia nzuri ya kujitoa na hayo mawazo ni;
.
Kuwa na shukrani.
Shukuru umapata mlo leo.
Shukuru umeweza kuamka leo.
Shukuru una uwezo wa kusoma haya.
Kinachotokea ni kwamba mawazo/ maumivu ya kuachwa yanakufanya usione sehemu nyingine za maisha yako ambazo bado zipo vizuri.
Haijalishi umeumizwa vipi, kuna sehemu tu ya maisha yako ambayo bado Mungu amekupa nafasi na inaenda vizuri.
Shukuru kwa hilo.
Kwa kila wazo kwamba “maisha yangu ndo yameshaharibika…” liwekee na shukurani “nashukuru Mungu kwa … maishani mwangu”.
Na kama unaona mawazo ni makali/ mengi, basi shukuru zaidi.
Mshukuru mtu anayekuhudumia kwa ukitakacho maishani.
Itakusaidia kuona upande mwingine wa maisha unaoenda vizuri badala ya kuhangaika na mambo yaliyoharibika.
.
Kubaliana na hali.
Kubali umeachwa.
Kubali kuwa saivi mwenzio ameona hufai tena. Jana ni jana, leo ni leo ndo mana leo ameona hufai.
Kubali kuwa hamuendani tena.
Watu wanaoendana hawaachani, kama mmeachana ujue hamuendani tena. Haijalishi zamani mlikua mnaendana vipi.
Kubali mambo yanapobadilika.
.
Jitoe ulipo kimawazo.
Una uwezo wa kuendesha akili yako.
Una uwezo wa kubadilisha mawazo na ukawaza kile ukitakacho.
Kujitoa ulipo kimawazo ni kufikiria nje ya boksi. Unafikiria kama mtu wa nje/ rafiki yako/ ndugu yako.
Yaani ni kama vile unavyomshauri mtu, we unakua unaona mengi kuliko yeye. Kwa sababu wewe haujashikamana na mawazo/ haujafungwa na mawazo.
Unapojitoa ulipo kimawazo unakua unafikiria vitu kama;
Ni jambo la mpito tu,
Hii sio mara ya kwanza kuachwa,
Mungu atanipatia mwingine mzuri zaidi,
Hii ni sehemu ya maisha, kuna kupata na kukosa,
Baada ya miaka miwili sitakua hivi tena, (kama ukiwa ivo ivo ujue una shida), na,
Tulipata muda mzuri pamoja, nimefurahia kuwa naye kwa kuwa nimejifunza kitu hiki na kile.
Kadri unavyojitoa na kuangalia jambo lako kama mtu wa nje unazidi kujijua.
Unaona wapi ulikosea, wapi ulifanikiwa, nini chanzo cha kuachana, na utafanyaje ili usiyarudie.
Muda mwingine unaona kuwa kiukweli bora umeachana na huyo mtu.
Sababu alikua anafanya maisha yako kuwa magumu, mshukuru mola.
Mwisho wa siku unagundua kuachwa si kubaya ni jambo zuri.
Umepata nafasi mpya ya kuwa na mtu mwingine bora zaidi, na
Umepata nafasi mpya ya kukua na kujiboresha mwenyewe zaidi.
Hautaona mwanga, hautopata nafuu na utakua mtu wa kulaumu tu pale ukiendelea kushikamana na mawazo ya kuachwa.
Na kuyawaza hayo tu bila kujitoa na kufikiria kama mtu wa nje.
Utakua mtu wa huzuni na utapishana na fursa mpya zinazokujia.